Baba wa Taifa na Wazee wa Dar es salaam waliomuunga mkono wakati wa kupigania uhuru

Baba wa Taifa na Wazee wa Dar es salaam waliomuunga mkono wakati wa kupigania uhuru


Mzee Mohamed,
Vitu kama hivi uwe unatupia hapa JamiiForums nasi tupate kufaidi historia ambayo haijaandikwa ktk maandishi na watu wa Enzi yako au kipindi kabla cha kwako, ikiwemo kisa hiki cha Mwl. Nyerere kugaa gaa chini tumbo likimuuma baada ya kupata mlo huku Bi. Nyangombe Mgaya akipiga kelele kwa Kizanaki na Kiswahili kuhusu mwanae kuumwa ghafla tumbo....

Mohamed Said On Women Leadership Summit
Mohamed Said, mwanahistoria nguli kutoka Tanzania. Hapa alikuwa kama mgeni mwalikwa katika kilele cha mkutano wa Women Leadership Summit. Hapa anatoa kisa cha Nyerere kuhusu dhana ya kulishwa sumu, mchango wa mwanamke katika uhuru - hasa alitazamwa hayati Bibi Titi Mohamed.

Source: Muddyb Mwanaharakati
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Mzee Kissinger na Mohamed Said
Mzee Kissinger na Mohamed Said wakiwa Kigamboni, Dar es Salaam. Kissinger anajaribu kumdokezea Mohamed Said baadhi ya mambo ambayo katika kitabu chake kuhusu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes" ameandika kiasi tu kuhusu Mwinyi Baba wa Mombasa. Sasa Kissinger anajaziajazia nyama zilizobanduka mwaka 1963......

Source: Muddyb Mwanaharakati
 
Utata wa Mwalimu kuanzisha TANU, wazee wa Dar-es-Salaam watetemeka kwa simanzi na kumuomba Mohamed Said kuweka mambo sawa kwa kuandika kitabu chenye historia inayotambua wahusika haswa wa vuguvugu la kudai uhuru wa Tanganyika.

Kwanini Mwalimu Nyerere hakutaka kuandika biography.....ya maisha yake ikiwemo harakati zake za kisiasa kabla ya Tanganyika kupata uhuru. Tumpe hongera Mzee Mohamed Said kwa kuweza walau kwa uchache kufahamu maisha ya harakati za Mwl. Nyerere ktk wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika..


Source: MzeeBarwani
 
UPANDE MWINGINE WA SHILINGI WA KUELEZEA ''HISTORIA'' YA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JK NYERERE : Mwalimu Nyerere ni kama Nabii :

Source: George Nyambo
 
Mzee Mohamed,
Vitu kama hivi uwe unatupia hapa JamiiForums nasi tupate kufaidi historia ambayo haijaandikwa ktk maandishi na watu wa Enzi yako au kipindi kabla cha kwako, ikiwemo kisa hiki cha Mwl. Nyerere kugaa gaa chini tumbo likimuuma baada ya kupata mlo huku Bi. Nyangombe Mgaya akipiga kelele kwa Kizanaki na Kiswahili kuhusu mwanae kuumwa ghafla tumbo....

Mohamed Said On Women Leadership Summit
Mohamed Said, mwanahistoria nguli kutoka Tanzania. Hapa alikuwa kama mgeni mwalikwa katika kilele cha mkutano wa Women Leadership Summit. Hapa anatoa kisa cha Nyerere kuhusu dhana ya kulishwa sumu, mchango wa mwanamke katika uhuru - hasa alitazamwa hayati Bibi Titi Mohamed.

Source: Muddyb Mwanaharakati

Bagamoyo,
Historia ya TANU ina mambo mengi sana na sikuweza kuyaandika yote katika
kitabu cha Abdul Sykes kwa sababu hii na ile.

Kuna mengine yanatisha kabisa na kuna mengine yanahitaji utulivu kuyaandika
katika hali mwandishi utaeleweka.

Kulikuwa na visomo vya Qur'an vingi katika kupambana na Waingereza na pia
kulikuwa na ''ndumba.''

Si unajua sisi Waafrika na mizimu yetu?
Sasa vipi unaandika mambo haya?

Baba wa Taifa katika ile hotuba yake kwa Wazee wa Dar es Salaam kagusia haya
na akasema kuwa yeye alikuwa ''mkaidi,'' kidogo katika mambo haya lakini walifanya.

Ile dua aliyofanyiwa Nyerere ya komkomoa Gavana Edward Twining si kama
alifanyiwa yeye peke yake.

Abdul Sykes alifanyiwa pia baada ya kutokea matatizo kati yake yeye na Mzungu
mkubwa wake aliedhamiria kumfukuza kazi kama Market Master baada ya Abdul
na huyu Mzungu kupambana pale sokoni kwa maneno makali watu wakishuhudia.

Kisa cha ugomvi huu ni kuwa Mzungu alimfuma Abdul anauza kadi za TANU sokoni
na kadi zenyewe kaziweka ofisini kwake.

Hili jambo lilikuwa kubwa sana kutosha mtu kupoteza ajira.

Mfano wake ni kama leo ukutwe unauza kadi za CHADEMA au CUF katika ofisi za
serikali.

Kisa hiki kanihadithia Mzee Abdallah ambae yeye alikuwa mhudumu katika ofisi ya
Market Master Abdul Sykes, siku hizo wakiitwa ''messenger.''

Mzee Abdallah anasema yeye alishuhudia ugomvi ule wote lakini bahati mbaya
walikuwa wanazungumza Kiingereza hakujua nini kinasemwa lakini ugomvi ulikuwa
kuhusu kadi za TANU.

Abdul alijaaliwa ulimi mzuri sana wa lugha ya Kiingereza ilikuwa starehe sana kumsikia
akizungumza Kiingereza.

Wazee baada ya kusikia taarifa hii waliamua, ''kumshughulikia,'' Mzungu kwa kumfanyia
Abdul kisomo.

Hiki kisa kirefu na kina mengi ambayo naona tabu kueleza hapa kama nilivyokwisha
kusema hapo awali.

Historia ya TANU ina mengi sana...
 
Mm pia nimevutiwa na elimu hii mpya sijapatapo pahala pengine.
 
Nnangale...
Usiwe na haraka yalikuja mambo ya kusikitisha kuanzia 1963 baada ya Muslim Congress ya 1962 na 1963...

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utayakuta humo.
title ya kitabu umecop&paste hapa na kuweka neno ally sykes tu.

dzavpharaoh-20180323-0001.jpg
 
Unachoshangaa kipi sasa?

Unashangaa Mjamaa hajatoa umuhimu kwa watu binafsi na kawashukuru kwa mpigo wakati itikadi ya ujamaa inamtaka awaangalie watu kwa mpigo na asiwaangalie mmoja mmoja kama watu binafsi?

Unashangaa mjamaa kufanya itikadi ya ujamaa inavyomtaka kufanya na kutofanya ubepari unavyomtaka kufanya?

Unashangaa Muarabu kuongea Kiarabu na kutojua Kiingereza?

Kruschev hakuwa mjamaa, alikuwa Mkomunisti aliyeuchukia Ukomunisti baada ya Stalin. Kruschev ndiye aliyeweka misingi ya kuvunjika kwa USSRambayo Gorbachev akaja kuimaliza. Sasa kumlinganisha Kruschev, a reformed Communist, na Nyerere, a Fabian Socialist, kamawote ni wajamaa, ni kutoelewa kwamba unachanganya mambo, hilo lakwanza.

Halafu lapili, hoja si Kruschev, ni Ujamaa. Inawezekana kabisa hata Kruschev angekuwa mjamaa wa jina akaendekeza kutajana majina, na Nyerere akaishikwa kanuni za Ujamaa za kushukuru kwa mpigo, mfano wa Nyerere ndio ungeonesha Mjamaa halisi.

Huwezi kusema kuiba kunaruhusiwa na Wakatoliki kwa sababu Papa kaiba, inawezekana Papa kaiba kwa sababu kapotoka,ukiwa na Mkatoliki Padre hataki kuiba, kwa sababu Katekisimu na Biblia vimekataza kuiba, hutakiwi kusema huyu mbona anakataa kuiba wakati Papa ameiba? Unatakiwa kusema mbona Papaanaiba wakati Biblia na Katekisimu vinakataza kuiba.

Vivyo hivyo, misingi ya Ujamaa haitaki ubishoo wa kutajatajamajina yooote ya watu, inasisitiza collective kuwa muhimu kulikoindividual, hivyo atatajwa mzee mmoja au wawili tu hapo, wengine watashukuriwa collectively kama "wazee" tu.

Sasa ukishakubali kwamba misingi ya Ujamaa inasisitiza kuangalia watu kwa mafungu kama collective, na Nyerere alikuwa mjamaa, itabidi ukubali tu kwamba alipowashukuru watu jumla jumla alikuwa anaishi kijamaa tu.
hii konki hoja kwa hoja na kurekebisha palipotoka.[HASHTAG]#falsafa[/HASHTAG] inafanya kazi.
 
Mtanganyika...
Hapana imegongana siwezi kufanya jambo kama hilo...angalia ''full title.'' ya mswada wa Ally Sykes na kitabu cha Abdul Sykes.

Kazi ngumu ni kuandika kitabu siyo kupata jina la kitabu.
 
Mm pia nimevutiwa na elimu hii mpya sijapatapo pahala pengine.
Kawombe,
Sijui kama umepatapo kusoma habari hizi hapo chini:
Mohamed Said: TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952

"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":

"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."

“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended
by leading members of the Mwanza Branch...”

(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda).
 
UPANDE MWINGINE WA SHILINGI WA KUELEZEA ''HISTORIA'' YA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JK NYERERE : Mwalimu Nyerere ni kama Nabii :

Source: George Nyambo

Bagamoyo,
Nimefurahi kumsikia Chris Peter.
Chris Peter ni msomi makini sana.

Nakumbuka siku hiyo mwaka wa 1998 kitabu cha Abdul Sykes kilikuwa
kimeingia nchini kutika Uingereza nilikutana na Chris Peter Zahir Hotel
tukakaa meza moja.

Chris akaniuliza kama nina nakala ya kitabu changu anunue.
Nikamuuzia.

Historia ya Mwalimu Nyerere katika uongozi wake baada ya uhuru, Azimio
la Arusha na Siasa ya Ujamaa hii ni historia inayofahamika vizuri kabisa sioni
kama inaweza kuleta mzozo wowote.
 
Nnangale...
Usiwe na haraka yalikuja mambo ya kusikitisha kuanzia 1963 baada ya Muslim Congress ya 1962 na 1963...

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utayakuta humo.

Mwanahistoria nimesoma kitabu chako life and times of Abdul Sykes ,hongera sana kitabu kizuri sana ila kuna kitu kimepungua,nilitaka Nijue maisha ya Abdul baada ya uhuru yaani ili kuwaje hadi Nyerere alimtupa
 
Back
Top Bottom