Mzee Mohamed,
Vitu kama hivi uwe unatupia hapa JamiiForums nasi tupate kufaidi historia ambayo haijaandikwa ktk maandishi na watu wa Enzi yako au kipindi kabla cha kwako, ikiwemo kisa hiki cha Mwl. Nyerere kugaa gaa chini tumbo likimuuma baada ya kupata mlo huku Bi. Nyangombe Mgaya akipiga kelele kwa Kizanaki na Kiswahili kuhusu mwanae kuumwa ghafla tumbo....
Mohamed Said On Women Leadership Summit
Mohamed Said, mwanahistoria nguli kutoka Tanzania. Hapa alikuwa kama mgeni mwalikwa katika kilele cha mkutano wa Women Leadership Summit. Hapa anatoa kisa cha Nyerere kuhusu dhana ya kulishwa sumu, mchango wa mwanamke katika uhuru - hasa alitazamwa hayati Bibi Titi Mohamed.
Source: Muddyb Mwanaharakati
Bagamoyo,
Historia ya TANU ina mambo mengi sana na sikuweza kuyaandika yote katika
kitabu cha Abdul Sykes kwa sababu hii na ile.
Kuna mengine yanatisha kabisa na kuna mengine yanahitaji utulivu kuyaandika
katika hali mwandishi utaeleweka.
Kulikuwa na visomo vya Qur'an vingi katika kupambana na Waingereza na pia
kulikuwa na ''ndumba.''
Si unajua sisi Waafrika na mizimu yetu?
Sasa vipi unaandika mambo haya?
Baba wa Taifa katika ile hotuba yake kwa Wazee wa Dar es Salaam kagusia haya
na akasema kuwa yeye alikuwa ''mkaidi,'' kidogo katika mambo haya lakini walifanya.
Ile dua aliyofanyiwa
Nyerere ya komkomoa
Gavana Edward Twining si kama
alifanyiwa yeye peke yake.
Abdul Sykes alifanyiwa pia baada ya kutokea matatizo kati yake yeye na Mzungu
mkubwa wake aliedhamiria kumfukuza kazi kama Market Master baada ya
Abdul
na huyu Mzungu kupambana pale sokoni kwa maneno makali watu wakishuhudia.
Kisa cha ugomvi huu ni kuwa Mzungu alimfuma
Abdul anauza kadi za TANU sokoni
na kadi zenyewe kaziweka ofisini kwake.
Hili jambo lilikuwa kubwa sana kutosha mtu kupoteza ajira.
Mfano wake ni kama leo ukutwe unauza kadi za CHADEMA au CUF katika ofisi za
serikali.
Kisa hiki kanihadithia
Mzee Abdallah ambae yeye alikuwa mhudumu katika ofisi ya
Market Master
Abdul Sykes, siku hizo wakiitwa ''messenger.''
Mzee Abdallah anasema yeye alishuhudia ugomvi ule wote lakini bahati mbaya
walikuwa wanazungumza Kiingereza hakujua nini kinasemwa lakini ugomvi ulikuwa
kuhusu kadi za TANU.
Abdul alijaaliwa ulimi mzuri sana wa lugha ya Kiingereza ilikuwa starehe sana kumsikia
akizungumza Kiingereza.
Wazee baada ya kusikia taarifa hii waliamua, ''kumshughulikia,'' Mzungu kwa kumfanyia
Abdul kisomo.
Hiki kisa kirefu na kina mengi ambayo naona tabu kueleza hapa kama nilivyokwisha
kusema hapo awali.
Historia ya TANU ina mengi sana...