Baba wa Taifa na Wazee wa Dar es salaam waliomuunga mkono wakati wa kupigania uhuru

Mwanahistoria nimesoma kitabu chako life and times of Abdul Sykes ,hongera sana kitabu kizuri sana ila kuna kitu kimepungua,nilitaka Nijue maisha ya Abdul baada ya uhuru yaani ili kuwaje hadi Nyerere alimtupa
Mukizahhp,
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika sikuandika kwa dhamira ya kuangalia
nani kapata nini baada ya uhuru.

Nimeandika kusahihisha historia ya Chuo Cha Kivukoni ambayo iliacha mengi.
 
M-mbabe,
Kuwa Waislam watoe maoni kuhusu kauli ya Kanisa Katoliki na KKKT...

Kaka hayo mambo ya hatari ghafla yanaweza yakageuka na vyombo
vya habari vikaingia katika shughuli nzito ambayo Waislam hawana
uwezo wa kupambananavyo.

Aliye pembeni haangukiwi na mti.
Waislam wana uzoefu mkubwa katika haya.
 
Ni bahati mbaya sana serikali zetu baada ya uhuru ziliendeleza poropoganda dhidi ya waislam kama ilivyokuwa enzi za ukoloni na hata zaidi,ndio maana waislam wanajua vifo vyao havichukuliwi kwa uzito sawa na kifo cha mtanzania mwingine mfano leo masheikh wapo gerezani miaka zaidi ya minne lakini hakuna vituo vya haki za binadamu vinawazungumzia kwa kuwa poropoganda zimewafanya watanzania wenzao wawachukulie kama nusu watu
 
duh!
 
Mukizahhp,
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika sikuandika kwa dhamira ya kuangalia
nani kapata nini baada ya uhuru.

Nimeandika kusahihisha historia ya Chuo Cha Kivukoni ambayo iliacha mengi.
Nami pia nimekisoma kitabu cha maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes toleo la Kiswahili .
Naomba nikuulize Abdul baada ya uhuru alikuwa anafanya shughuli gani?
 
Nami pia nimekisoma kitabu cha maisha na nyakati za Abdulwahid Sykes toleo la Kiswahili .
Naomba nikuulize Abdul baada ya uhuru alikuwa anafanya shughuli gani?
Kitulo,
Siku zote yeye alikuwa akifanya biashara hata kabla ya uhuru.
 
Kumbe hawa wameru walianza zamani na vita ya ardhi!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…