Baba Yako alipokuwa anakwambia Hana Ulimuona Mchoyo, vipi sasa unaionaje Hali?

Baba Yako alipokuwa anakwambia Hana Ulimuona Mchoyo, vipi sasa unaionaje Hali?

Baba yangu amechangia pakubwa niwe hivi nilivyo. Ninaenda shule bweni Ifunda kutokea Arusha. Dingi kanipa pocket money Tsh 1000/= (buku) na maneno mengi ya kishujaa kuwa usijali hela nitatuma. Huwezi amini kwa yale matumaini nakuja kukutana na pocket money nyingine imeunganishwa na nauli karibia na kufunga shule. Ukubwani nilikuja kumwelewa sana kuwa kile kidogo alichokuwa nacho aliwekeza zaidi kwa Dada aliyekuwa kanitangulia darasa moja na yeye akiwa sekondari boarding. Option ikawa ni mimi kupitia moto mkali na dada apitie unafuu. Mtoto wangu wa kiume lazima akinywee kikombe nilichonywea hata kwa 25%.
 
Ngoja niseme kwa watoto wangu.....
Kwanza hawajawahi kujua kama sina ama baba anaishiwa, na kama sina hua nawaahidi kwamba siku flani nitatimiza na lazima nitimize.
Lakini pia kwa namna nilivyo walea, hawa madogo wanamuamini baba yao (mimi) kuliko mtu yeyote duniani...😊
👏🏽👏🏽👏🏽 safi sana, wewe ni kama baba yangu (Mungu amrehemu) kwa kweli hakuwahi kuniambia hana wala kutunyima chochote. Wakati mwingine ilikua tukiomba hela, atasema nitakupa kesho au wikiendi, ila jibu la sina sikuwahi kulisikia.

Naamini pia kwako, watoto wako wamebarikiwa sana 🙌🏽🙌🏽
 
Nakumbuka sebureni kulikua na sofa maalumu la kukaa mshua tu, ilo sofa hata asipokuwepo linabaki bila kukaliwa na yoyote. Nilikua namwona mzee dikteta ila badae sana nikaja kujifunza mwanaume bila kuwa na element za kidikteta watu watakuchukulia poa
Ipo hivyo mkuu, hata mimi dining table kuna kiti hakuna anakalia, madogo wanaambiana wasikae kiti cha baba.

Kuna namna baba ana nguvu sana ndani ya nyumba, bahati mbaya wengi hata hawaelewi.
 
😅😅na litoto apa naona lisha anza kunipiga vizinga ambavyo najua kabisa ni vya uongo ,sasa nimejua kwa nini hata mzee alikua akinipa tu pesa hata pale napo danganya nikizani nime muweza kumbe alikua akijua pia bhana
 
Ndiyo!

Nakukumbusha wewe, ulipokuwa mdogo uliona kama baba yako anakunyima Hela😅😅

sasa ni zamu yako kuzitafuta, Unaionaje Hali?

Ukiombwa Hela Unaitoa Kirahisi?
Endelea kupumzika mzee hakika sikuwahi kukosa kbsaa kipindi cha uhai wako😘😘😘
 
Una uhakika gani kwamba kila mtu alikuwa anaomba pesa kwa baba yake? Kikawaida baba humpa hela mtoto akiamua tu, kumbe wengine mlikuwa mnaomba kabisa. They say experience builds character.
 
Ngoja niseme kwa watoto wangu.....
Kwanza hawajawahi kujua kama sina ama baba anaishiwa, na kama sina hua nawaahidi kwamba siku flani nitatimiza na lazima nitimize.
Lakini pia kwa namna nilivyo walea, hawa madogo wanamuamini baba yao (mimi) kuliko mtu yeyote duniani...😊
Mimi Kama sehemu ya watoto wako, nasema hili ni kweli kabisa. Ushimen
 
Back
Top Bottom