Wadau wa JF.
Hiki ni kisa cha ukweli kilichotokea wiki iliyopita. Ninakiandika kwa huzuni sana na aibu kubwa. Nilikuwa safarini na niliporudi nimekuta kesi hii inafukuta ikiwa imetokea kama siku 2 kabla ya mimi kuwasili.
Baba yangu ana umri wa miaka 70 plus. Mama yangu yupo Mid 60s. Ilitokea kwamba wana housegirl wa umri wa miaka 18 hivi toka maeneo ambayo hutoa wasichana wengi wa jinsi hii.
Bila kupamba jambo hili, baba yangu amembaka huyu msichana wakati mama hayupo. Msichana alitaka kwenda kushitaki polisi ila aliombwa sana na ndugu zangu asifanye hivyo.
Jambo hili limeleta vurugu kubwa sana nyumbani. Hakuna anayetaka kungea na mzee na mama amesema anafunga mizigo yake arudi kwao (at that age?). Watoto tumebaki tunashangaa hatujui la kufanya maana wale ni wazazi wetu na tunaona aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo). Pia watu wa dini unaanzaje kuwaelezea? Tunajiuliza kama huyo binti amepata ujauzito je? Kama akiamua kushitaki polisi je?
Yani sijawahi kupata fedheha kama hii. Hata sisi kwa sisi hatutaki kulizungumzia jambo hili.
Tumsaidieje mama?
Tuokoeje ndoa yao? Mzee hataki kukaa nyumbani safari za hapa na pale haziishi!
Tumsaidieje yule binti wa watu na trauma hiyo?
Naombeni msaada, bila matusi tafadhali. Mbakaji akiwa mbali rahisi kusema - afungwe, ila baba yako unasemaje?
DA hivi wewe unatoka nyanda za juu? I always admire your contributions, keep it up. Hili suala si jipya, kumbuka maandiko katika Biblia takatifu. Huyo mama apate ushauri nasihi kwani hatakuwa na pa kwenda na asijidanganye, hapo ni kwake na aibu ni ya wote asimkimbie wala kumwachia huo mzigo mumewe na anaweza kuwa chanzo. Nakumbuka kuna wakati bibi yangu alipokuwa anaombwa na babu, alikuwa anakataa katakata, kisa? ni 'mchezo wa vijana, tuwaachie'.Dah mbombo ngafu hapa mpaka nimeishiwa maneno
We Chupaku,under any circumnstances usije ukarogwa kujaribu kumwinulia mzazi wako mkono,never never never,and I mean never,nshawaona mimi waliowabonda wazazi wao na walikoishia najua mie,usithubu,futa kabisa hiyo njozi!Nilitamani kumchapa. kweli anastahili adhabu ila ipi sasa? tumeamua kutoongea naye na kaamua kwenda kunywa pombe zake. Akipata ukimwi umri huo ARVs atazimudu?
Lizzy kesi za kubaka unatakiwa uripoti hapo hapo wakati mbegu bado ziko ndani na michubuko ni fresh,sasa mpaka Chupaku kapata muda wa kuingia kwenye kompyuta na kusema binti keshaondoka ila wana contact zake,kuna kesi tena hapo?Hapo kwenye ipi kushitakiwa anastahili....fikiria kibabu cha jirani kikikubakia mtoto utafanya nini???Mpeni huyo binti na familia yake haki ya kupata haki!Kama hatoshtaki iwe kwa mapenzi yake na sio shinikizotoka kwenu!
Mkuu kwenye red hapo,na anayetembea na waume wa watu unamhukumu vipi huyo? Au mzee ndo ile 'akipiga kelele chiriku anaimba ,akiimba bundi ni uchuro'?Huyu Mzee ana PEPO WA NGONO AU kitaalam SEXUAL MANIAC.
Kwanza ni kum-consell mama na mtoto wapone majeraha, kisha kudeal na MZEE WA MAPEPO.
Huyu mzee anastahili kwenda JELA kutumikia kifungo cha miaka 30, HUKO atakutana na wenye mapepo wenzake WANTAFUNE na yeye aone raha ya kutafuna kwa nguvu. Kisha pepo wake watamtoka au watashika adabu.
wabongo tumekuwa na tabia mbaya sana ya kulea maovu, tunalea na kukingia kifua maovu mengi kuanzia ndani ya familia zetu hadi kwenye ngazi za serikali, ufisadi, umalaya, ufataki,ulevi, n.k. Hii ni aibu kubwa, huyu anatakiwa kuhukumiwa kwa kosa lake hata km ni baba.
Mimi kuna watu ambao siwezi kuwasamehe:
1. MBAKAJI
2. JAMBAZI
3. ANAYETAFUNA WAKE ZA WATU
HAWA ni watu wa kuondoshwa kabisa ktk jamii. kungekuwa nauwezekano wa kuwapeleka sayari yao ingekuwa poa sana. hawafai, msiwaonee huruma.:bange:
Housegirl kaondoka ila tunazo contacts zake bado. Hivi babu wa hivyo unaweza hata kumuacha na mjukuu kweli? AArrrgggghhh
Mbona kawaida sana mkuu? humu tunashauriana mambo mengi tu na hata kwa ujumla wake ndio yanayoleta maana ya MMUKwanza kabisa naweza kusema wewe mtoa mada hii ebu niangalie jina lako kwanza... Ooh Chupaku, HUNA ADABU hata kidogo tena naweza kusema umemkosea adabu Mzee wako (I mean Baba yako Mzazi), napata wasi wasi kama huyo uliye muelezea hapa ni baba yako kweli au ni baba wa kambo au wa Kufikia.
Haiwezekani jambo kama ili la kifamilia mshindwe kulizungumzia uko uko nyinyi kwa nyinyi, mpaka ulilete hapa hadharani, kwani unafikiria watu hawakujui wewe Chupaku ni nani? Nikiangalia IP tu hapa najuwa unaandika kutokea wapi na unatumia mtandao gani.
Hivi uko kwenu ukufunzwa adabu na heshima? Ukuambiwa kuwa mambo yanayo husu familia huwa yanatatuliwa kifamimilia!? Hakuna wazee kwenye ukoo wenu, au mzee aliye baki hai ni Baba na Mama Chupaku tu!?
Siku mkeo akikunyima unyumba pia utaleta humu JF ili kupata ushauri? Grow up my friend, this is not funny.
Alafu unadai eti nanukuu "...aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo)...."
Sasa unataka kosa la mtu mmoja kuhumiwa ukoo mzima, unacho kiogopa kuongea na wake zenu nini na unacho kifanya hapa ni nini.
Yaani hapa unataka kudhihirisha kuwa wewe unamini watu walioko JF kuliko spouses wenu, familia yako wewe na ndugu zako na hata wazee wa Ukoo wanu.
Maybe you better think twice next time my friend before you just post mambo ya kifamilia.