Kwanza kabisa naweza kusema wewe mtoa mada hii ebu niangalie jina lako kwanza... Ooh Chupaku, HUNA ADABU hata kidogo tena naweza kusema umemkosea adabu Mzee wako (I mean Baba yako Mzazi), napata wasi wasi kama huyo uliye muelezea hapa ni baba yako kweli au ni baba wa kambo au wa Kufikia.
Haiwezekani jambo kama ili la kifamilia mshindwe kulizungumzia uko uko nyinyi kwa nyinyi, mpaka ulilete hapa hadharani, kwani unafikiria watu hawakujui wewe Chupaku ni nani? Nikiangalia IP tu hapa najuwa unaandika kutokea wapi na unatumia mtandao gani.
Hivi uko kwenu ukufunzwa adabu na heshima? Ukuambiwa kuwa mambo yanayo husu familia huwa yanatatuliwa kifamimilia!? Hakuna wazee kwenye ukoo wenu, au mzee aliye baki hai ni Baba na Mama Chupaku tu!?
Siku mkeo akikunyima unyumba pia utaleta humu JF ili kupata ushauri? Grow up my friend, this is not funny.
Alafu unadai eti nanukuu "...aibu hata ku-share na spouses wetu (tunaogopa kumbe nyiye ndivyo mlivyo)...."
Sasa unataka kosa la mtu mmoja kuhumiwa ukoo mzima, unacho kiogopa kuongea na wake zenu nini na unacho kifanya hapa ni nini.
Yaani hapa unataka kudhihirisha kuwa wewe unamini watu walioko JF kuliko spouses wenu, familia yako wewe na ndugu zako na hata wazee wa Ukoo wanu.
Maybe you better think twice next time my friend before you just post mambo ya kifamilia.