Ndugu wanajamii forum baba yangu alikuwa afanyiwe upasuaji mdogo kwenye ziwa kulikuwa kuna uvimbe alipochomwa sindano ya nusu kaputi mapigo ya moyo yakasimama ghafla na akapoteza fahamu toka jumatano asubuhi yupo icu hajitambui anapumulia mashine!tukiwauliza madaktari hawana majibu sahihi!swali langu nikwamba atakuwa amepata tatizo gani?naombeni ushauri wenu kwayoyote anayejua ishu kama hii!natanguliza shukrani.