Baba yangu kachomwa nusu kaputi Jumatano hajazinduka mpaka leo, bado yupo ICU

manka kim

Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
31
Reaction score
27
Ndugu wanajamii forum baba yangu alikuwa afanyiwe upasuaji mdogo kwenye ziwa kulikuwa kuna uvimbe alipochomwa sindano ya nusu kaputi mapigo ya moyo yakasimama ghafla na akapoteza fahamu toka jumatano asubuhi yupo icu hajitambui anapumulia mashine!tukiwauliza madaktari hawana majibu sahihi!swali langu nikwamba atakuwa amepata tatizo gani?naombeni ushauri wenu kwayoyote anayejua ishu kama hii!natanguliza shukrani.
 
Pole sana mkuu kilichobaki ni kumuomba mungu ampe uzima kwani yeye ndio ajuae kila kitu.
 
Pole sana, swala lililobaki ni kumwomba mwenyezi Mungu na kumwombea.
 
mhh,kuna kitu hakipo sawa hapo!
pole kwa matatizo makubwa yaliyowakuta!
 
Pole sana mkuu, kuna daktari mmoja aliwahi kuniambia kitaalamu kuna vipimo huwa vinatakiwa kuchukuliwa kabla mgonjwa hajachomwa sindano ya nusu kaputi ila madaktari wengi huwa hawazingatii hilo na inaweza kua na reaction mbaya kwa mgonjwa ila kwa sababu ni makosa yao hawawezi kukwambia. Kikubwa muombe mungu mkuu yeye ndo muamuzi wa kila jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…