Mimi huwa nawahurumia sana watoto wa kiume ambao kama mazombi huwa wanakuwa upande wa mama kumsema na kumlaumu baba bila hata kujua tabia za mama yao. Yaani kiafrika hakuna namna mama anaweza kuwa na kosa katika ndoa, kila pakitokea kutokuelewana ni lazima jamii na watoto watamuona baba ndio ana makosa na kama ulivyosema mtoa uzi, wababa huwa wanajikalia kimya tu.
Enyi watoto wa kiume au tuseme tu watoto wote, kukiwa na kutokuelewana kati ya baba yako na mama yako usipende kuchukulia lazima baba ana makosa! Ni mbaya sana na nyie watoto wa kiume mjue njia anayopita baba yako na wewe utapita humo humo kenge wewe!