Babati: Viongozi wa CCM wilaya ya Babati wamshamburia askari Polisi kwa mateke na fimbo, kisa tu kuulizwa kibali cha mkutano

Babati: Viongozi wa CCM wilaya ya Babati wamshamburia askari Polisi kwa mateke na fimbo, kisa tu kuulizwa kibali cha mkutano

Ifike mahali watu waache kudharau wenzao hivi kuonesha tu kibali walichopewa kulikuwa na shida gani,soldier akomae nao mpaka hatua ya mwisho vinginevyo mtu akipata kanafasi kidogo anaanza kuona wenzake hawana thamani.
 
Daah, hii ni below standard!

Walikua wamevaa yale mashati yao?

Sasa mimi na Saint Anne tutaambia nini watu? 🤣🤣🤣
Haki ya nani🤣🤣😂😂😂😂😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌🙌🙌
Bwana niache🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣


Hali ni tete huku kijani kibichi
 
  • Kicheko
Reactions: Pep
#HABARI KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) wilayani Babati Filbert Mdaki (52) na Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM wa Wilaya hiyo, George Sanka (46) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga Askari Polisi mateke na fimbo. /https://t.co/la4H3dEJXX https://t.co/4JAdYqRdUT
View attachment 2052547
Kwa dhalau za mama na chuki anazoonyesha dhidi yenu mtapigwa sana. Kwanza na mzee wa MIPA kazi out

Na bado matajili wana uoga wa jiwe. Ukiwaisha tu nao wanaanza kuwazaba vibao. 2025 mtakuwa mmepata akili
 
Katibu wa CCM Wilaya ya Babati, Filbert Mdaki (52) na Katibu wa jumuiya ya vijana UVCCM wa wilaya hiyo, George Sanka (46) wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga askari polisi mateke na fimbo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea kijiji cha Kirudiki wilayani Babati Desemba 16 saa 11 jioni.

Kamanda Kuzaga alisema watuhumiwa hao walimshambulia Koplo Baraka wa Kituo kidogo cha Polisi Kiru kwa kwa mateke na fimbobaada ya kufika kwenye mkusanyiko wa wananchi wa Kijiji cha Kirudiki.

“Askari huyo baada ya kuona mkusanyiko alifika ili aulizie juu ya kibali cha mkusanyiko huo, ndipo viongozi hao wakamshambulia maeneo mbalimbali ya mwili,” alisema kamanda Kuzaga.

Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

Kada wa CCM wa mjini Babati mkoani Manyara, Cosmas Masauda, ameeleza kusikitishwa kwa kitendo cha viongozi hao kukamatwa na kupelekwa mahabusu wakiwa kazini.


Masauda alisema mkutano huo ulikuwa na kibali na viongozi hao walikwenda kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro wa shamba baina ya wanakijiji na mwekezaji.

Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara, Simon Lulu alisema atazungumzia jsuala hilo baada ya ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumalizika.

“Tumepanga kuwa baada ya ziara ya
Waziri Mkuu Majaliwa ndipo tutazungumza juu ya tukio hilo la viongozi wetu kukamatwa,” alisema Lulu.
Yani KILA kitu kiko WAZI ,alafu uchunguzi bado unaendelea, ila bora ni ccm ingekua chadema taarifa isingekua imetolewa
 
#HABARI KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) wilayani Babati Filbert Mdaki (52) na Katibu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM wa Wilaya hiyo, George Sanka (46) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga Askari Polisi mateke na fimbo. /https://t.co/la4H3dEJXX https://t.co/4JAdYqRdUT
View attachment 2052547
UVCCM miaka 46? Hili lichama ndo maana linatuletea hata Marais wa hovyo hovyo
 
200 (10).gif
 
Back
Top Bottom