Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
BABU AKASEMA; PESA INAMAADUI WAWILI, JE WAWAJUA?
Anaandika , Robert Heriel.
© Maandishi ya Robert Heriel Kwa lugha ya Kiswahili.
TAIKON Anawasilisha.
" Upepo unapotoka hatuuoni na wala unakoelekea hatupajui, ndivyo ninyi Vijana wa Zama hizi mlivyo, mmejigeuza upepo, hamtaki kujua wapi mlipotoka na bila Shaka hamjui ni wapi muendako, kukumbuka nyumbani ni Dalili ya mtu mwerevu, yeyote akumbukaye nyumbani huyo yunaakili. Kukumbuka ulipotoka ni kujua mahali Ulipo, na kujua mahali Ulipo ni kujua unakoenda. Ni kweli mwanadamu hakupewa macho ya kisogoni lakini hakunyimwa shingo ya kugeuka ili aangalie alipotoka akiwa kasimama pale alipo" Babu akasema kisha akanitazama na Uso wake wenye ngozi iliyojikunja. Sikupendezwa na Sura yake lakini nilijikaza, sisemi ili nionekane sina Radhi Bali nasema iliyokweli. Uso wa Babu ulikuwa hauvutii hata kidogo, ulichukiza,
Babu akaendelea;
" Ungalipo kijana linda mambo matatu, Mosi, Akili yako, nguvu zako, na pesa zako.
Hayo matatu yalinde kuliko chochote Kwa maana ndio yatakayoulinda Uanaume wako. Mwanaume huthibitika kwa hayo manne.
Akili ndio nguzo kuu ya yote hayo, nguvu pasipo akili mi UTUMWA, nguvu pasipo akili mi Mateso Kwa mwili"
Babu akakohoa kidogo kisha akaendelea,
". Nguvu ya mwanaume zipo tatu, Ile ya Mwili, hisia na Ile ya kiroho"
Babu akanitazama kisha akawasha Kiko yake, alafu akavuta pafu ndefu akiwa kafumba macho yake, kisha akaachia fumba la Moshi toka mdomoni mwake, Moshi ukatapakaa mbele ya USO wake kisha akafumbua macho yake kunitazama; alafu akasema;
" Mapenzi ni nini?" Akaniuliza
Nikamtazama nikamjibu.
" Mapenzi ni nguvu za ndani za hisia ya mtu a kuvutiwa na mtu au kitu Fulani.
" Umejibu vyema. Ukiweza kuweka uwiano Sawa baina ya nguvu hizo za hisia na akili yako basi utayafurahia mapenzi. Akili isitumike zaidi ya hisia halikadhalika na Hisia zisizidi akili uwapo katika anga la Mapenzi.
Nimeyataja mapenzi Kwa sababu wengi yanawapelekesha, wengi wameumizwa na kuumizana. Kama wangejua hili huenda wasingefika huko" akameza fumba.
" Mapenzi hujengwa na mambo matatu, Hisia, muda na wajibu; mambo hayo yakiwa na uwiano mzuri mapenzi hayatakushinda. Kumpenda mtu ni hisia, ambapo itanitajika muda kutelekeza wajibu ili wote mufurahiane.
Vijana wa Zama hizi mnafikiri mapenzi ni ngono tuu, yeyote anayefikiri Kwa mtazamo huu kamwe hawezi fanikiwa kuyamudu mapenzi. Mara zote wanaofikiri mapenzi ni ngono hushindwa kuwaridhisha wenza wao, halikadhalika wanaofikiri mapenzi ni pesa hushindwa na Mapenzi mapema mno.
Hata hivyo sikatai umuhimu wa tendo la ngono katika mahusiano ya wanandoa.
Nilitaka Kueleza namna ya kuzitambua pattern na lock za UKE wa mwanamke lakini hiyo nitakueleza siku nyingine"
Mzee alivuta koki kisha akaendelea;
" Kila mtu anaweza akawa na pesa nyingi mno. Lakini ili uwe na pesa lazima uwajue maadui wa pesa. Kwa maana pesa hawezi kukubali uwe naye wakati umeungana na adui zake, ukifanya hivi pesa nayo itakuona adui yake.
Adui wa pesa wako wawili tuu, nitawataja, mmoja anaitwa MATATIZO na Wapili anaitwa STAREHE Bin ANASA.
Ili uipate pesa, tumia pesa kuondoa matatizo, tumia pesa kufukuza matatizo na sio utumie matatizo kufukuza pesa.
Pesa anapenda Sana ukimtumia kufukuza matatizo.
Ili uyafukuze matatizo lazima uitumie pesa kuungana na akili kuyafukuza matatizo, pesa na akili ni marafiki wa siku nyingi.
Pesa itangulie kabla ya matatizo, na sio pesa ikute Matatizo. Na ili hili litokee lazima akili awepo. Penye akili kuna uhaba WA magonjwa, Ajali, na matatizo mengine.
Zamani akili watu walizaliwa nazo, wengine walivuviwa na miungu yao, wengine Kwa kujifunza Kwa uzoefu lakini siku hizi wengi hupata akili kupitia kusoma maandiko na nyaraka mbalimbali, mnaita Elimu ya kusoma,
Akili ni Akili mjukuu WANGU.
Usiwaze kutumia pesa kuliondoa tatizo linalokuzunguka ikiwa huna akili ya kutosha kuliondoa, kwani hapo utakuwa huondoi Hilo tatizo Bali utakuwa unaiondoa pesa.
Sio ajabu kuna watu huuliza; hivi Kati ya pesa na matatizo Nani anammaliza mwenzake?. Swali hilo itategemea Kama akili ilitumika au laa.
Adui wa mwisho ni STAREHE mtoto wa ANASA.
Pesa hapatani na ANASA zisizo za akili.
ANASA zisizo na akili ni zile mtu anaitafuta pesa ili azipate, yaani mtu anafanya kazi kichwani akiwaza kuwa siku bingo likitiki atakula Bata la kufa mtu. Pesa haiji Ng'ooo!. Pesa humtaka mtu anayechukulia ANASA Kama Jambo la ziada na wala sio kipaombele chake.
Watu wote wenye pesa kwao ANASA ni Jambo la ziada, usishangae Kwa wiki au mwezi akawa anastarehe siku moja, au Kwa mwaka anamwezi mmoja wa kustarehe. Lakini wale wasio na pesa hujikuta wakitaka kustarehe na kila Bata kila siku"
Babu akatema mate chini, kisha akamalizia;
" Adui wa pesa ni wawili tuu mjukuu wangu, MATATIZO na ANASA"
Akamaliza.
Ni Yule Mtibeli
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam