Mwendazake alikuwa hapendi watu wenye akili.Nilishangazwa sana kwa kuachwa Adadi aliyekuwa ameshinda kura za maoni, na kuchukuliwa Mwana FA!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwendazake alikuwa hapendi watu wenye akili.Nilishangazwa sana kwa kuachwa Adadi aliyekuwa ameshinda kura za maoni, na kuchukuliwa Mwana FA!
Dr Babu taleKuna muda huwa najiuliza tu kama watanzania tulianza anzaje kuwa na mbunge kama Babu Tale
Mwendazake alifanya kazi ya ubunge iwe ni kama kazi ya kubeti tu. Wanatangaza nafasi mwenye pesa anachukua Form mwenyekiti akimkubali basi ndio anakuwa mbunge, maana hakuna uchaguzi wa haki uliotokea ilikuwa one man say.
Mwendazake alikuwa anasema tu nileteeni huyu na huyu, jaji Lubuva na washirikia wake huko wakurugenzi na kina Polepole wanapitisha tu.
Leo hii tuna mbunge kama babu tale asiye jua ata Bunge lina kazi gani?
Mwendazake alikuwa anatupeleka kuleee shimoni kabisa.
Babu tale, Babu tale, Babu tale nimekwita mara tatu, tumia vuzuri pesa zako za posho 360k za kila siku unazopata hapo bungeni kwa ajiri ya mitano ya baadae.
Tumia vizuri hiyo 10 M ya kila mwezi kama mshahara wako wa ubunge kwa ajiri ya mitano ijayo. Pia utumie vizuri kiinua mgogo chako cha karibia 250M ya ubunge wako punde tu baada ya Rais wa JMT kuvunja Bunge mwaka 2025.
Usidhubutu, usidhubutu, usidhubutu, kurudia tena kuutaka ubunge utamaliza pesa zako za posho, mshahara na kiinua mgogo buree na Ubunge hautaupata tena.
Utapata wafuasi wengi wa kukushawishi ugombee tena. Hao hawana wema watakuwa tu wanataka kuchuma mali kutoka kwako wapuuze waambie tu Mitano uliyohudumu kazi ya ubunge kwako yatosha unaenda kupumzika.
Ukifanya hivyo utanishukuru baadae.
CCM imerudi kwa wenyewe na soon mtaona makucha yao.
Cc Zero IQ