Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.
Kufuatia ujumbe uliotumwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kwenda Loliondo kwenda kuangalia uhalali wa matibabu yanayo tolewa na babu inasemekana babu hakuwa tayari kuruhusu wataalam hao kuipima dawa yake. ndugu wanajamii je hiyo imekaaje?
Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.
Hii ni sawa, lakini kama serikali inabidi/ni muhimu ijiridhishe pia kwamba dawa hiyo licha ya kuponya kama inavyodaiwa haina madhara mengine makubwa kwa mtumiaji (sasa na baadae). kumbuka ni maelfu ya watu wanapatiwa tiba hii na wengine wanatolewa mahospitalini kwenda huko kwa ajili ya tiba, sasa kama ina madhara ni watu wengi wataathirika na serikali ina jukumu la kulinda afya na maisha ya watu wake.Wawachukue wagonjwa wa ukimwi, kisukari na kifua kikuu kama "sample" wawapeleke na baada ya kunywa wawapeleke maabara kupima kama bado wanasumbuliwa na magonjwa yao. Hili halihitaji PHD kulithibisha, kupima dawa ni kutaka kuiba formular ya Babu bila idhini yake.
ha hahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!
mkwere nae nasikia ataenda kuzindua jiwe la shule ya msingi huko loliondo!!!
mmhh!! nahisi lbd anataka apate gia ya kumpitia babu apate kikombe kimoja.