Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Babu wa Loliondo afungiwa kwa muda kutoa huduma...

Wao wenyewe wapige kikombe kimoja hapo kwanza mana wengine sio wazima halafu wakirudi dar waandike kwenye report sasa ule mti ni noma usiupimie...
 
kuna sample ya huo mti hapo kwa babu.....wapime huo

Kuna sample ya wafanyakazi wengi tu pale Wizara ya afya/Muhimbilli/NIMR/TFDA ya watu wenye magonjwa Sugu, TAFADHALI TUMIENI HAO JAMANI NA SI KUMBUGUDHI BABU WA WATU
 
Ina maana babu hajatoa hata namba ya account tuchangie huduma! Anyway tenda wema nenda zako usitizame nyuma. Anachofanya babu ndiyo utumishi wa kweli yeye hayuko kibiashara na hii inadhihirisha babu kweli katumwa na Mungu kuokoa watu. Zidumu harakati za babu. Vipi mustakabali wa akina ndodi??

Babu hana account na kila 500 inayoingia 300
kanisani 200 kwa wasaidizi wake 6 wanaogawa dawa hivyo anabaki na umasikini wake
 
Babu anatakiwa kuingia kwenye records za dunia kwa kusaidia watu bure! Kweli babu anasaidia Watanzania bure. Inabidi ukokotoaji wa watu ambao amewatibu ukichukuliwa magonjwa sugu kama kisukari, cancer, pumu, pressure na ukimwi kuwa mtu huwa anatumia shilingi ngapi (on average) mpaka atakapoitwa maisha ya milele halafu kukisia kuwa babu ameokoa shs ngapi kwa taifa na Watanzania. For sure itakuwa hela ndefu sana. Ukichukulia tu kuwa mtu mmoja on averaga anacost serikali Shs10million, babu akiweza kuhudumia watu 100,000/= atakuwa ameliokolea taifa zaidi ya Tshs1trillion. Haya ni mahesabu ambayo ni ya kubuni kwani in actual sense gharama ni zaidi ya hapo!!!!!
Ee Mwenyezi Mwingi wa Rehema umruhusu huyu Babu aishi muda mrefu aendelee kuwahudumia waja wako. Ee Mungu utunusuru.
 
Tena kanisani wanasisitiza sadaka yako ndiyo marashi kuwezesha baraka kushuka kwa wingi wanairemba fwezaaaaa mara wanaiita mbegu panda nyingi uvune nyingiiiii halafu wanamponda babu kuwa imeandikwa cku za mwisho watatokea manabii wa uongo wkt wao ndiyo manabii wa kimagumashi washindweeeeee
 
Kuna sample ya wafanyakazi wengi tu pale Wizara ya afya/Muhimbilli/NIMR/TFDA ya watu wenye magonjwa Sugu, TAFADHALI TUMIENI HAO JAMANI NA SI KUMBUGUDHI BABU WA WATU

Huwezi kutest dawa kwa binadamu bila kufuata taratibu zinazoeleweka kama dawa ina madhara je?. Watanzania tumechanganyikiwa kweli.
 
nlishawahi kwenda muhimbili kitengo cha madawa ya asili miaka ya 1999/2000.
Mambo niliyoambiwa labda kwa wazee hawajaenda shule ya kutosha ndio watakubali.
Na ajili hiyo hawawezi kutoa mchango mkubwa au sio ushirikiano mzuri.
1-Niliambiwa niwapelekee sample kwa kila dawa kilo moja. Aina ya dawa zangu ni mbegu.
2-Niwatajie zinapatikana wapi?
3-Niwatajie zina tibu maradhi gani?
4-Na taratibu ya dose!
....kwa maswali haya ilikua ni vgumu kuuza taaluma yangu.
Kwa upande wa sample nlikubali niwape unga uliosagwa...hayo maelezo mengine sikuweza kukubaliana nao.
Nao wakawa wananizungusha hadi nlipopewa ushauri na jamaa zangu madaktari kua niendelee na mambo yangu mengine.
Hapo niliachana nao.
Mara nyingine niliambiwa itaenda kupimwa ulaya kwe maabara nyingine.
Maswali niliojiuliza ni mengi.
Ndipo nkajua kwa utaratibu huo labda ambao hawajaenda skuli ya kutosha watakubali hayo masharti.
Nlikua nahitaji wagonjwa wa HIV kwa kua wengi waliokua na maradhi nyemelezi walikua wakipata nafuu zaidi kutokana na matatizo yao.
Hata hivyo niliendelea na utafiti wangu mwenyewe ila sijajitangaza tena kwa tiba hizo kwa sababu zangu binafsi.
Ambao waliotumia dawa hizo wamenufaika nazo....uzito uliopo ni gharama yake...japo si kubwa .
Waliotumia ni wenye
shinikizo la damu,kisukari,ukimwi(HIV).
Unaweza niuliza/ukajiuliza iweje sijaitangaza?
..jibu langu kazi ninazozifanya ni nyingi ni kusaidia jamii. Hata hiyo huenda ni njia nyingine ya msaada .
Watu wengine hua nikiwapa njia wakajitayarishia wenyewe japo imani zao kubwa huepo kwa ile dawa ninayo itayarisha mimi.
Hivyo ndio hali niijuayo .
Babu nae makini!. Asaidiwe kuwekewa mazingira mazuri ili jamii inufaike na tiba, hilo ndio la busara.
 
1-Niliambiwa niwapelekee sample kwa kila dawa kilo moja. Aina ya dawa zangu ni mbegu.
2-Niwatajie zinapatikana wapi?
3-Niwatajie zina tibu maradhi gani?
4-Na taratibu ya dose!
.

Sasa masharti hayo yamekushinda nini? Mbona basic kabisa. Unataka waipime vipi dawa yako kama hautawaambia inaponya nini na dosage yake ni nini? Uko serious kweli mkuu??
 
Ningemshauri Ndodi asitie maguu Arusha atapata aibu. Dozi ya minyoo 400,000 wakati ni mbegu za mapapai tu alizosaga. Laki 4 kweli?
 
Mimi nawambia wana JF kama una ndugu ni mgonjwa mpeleke loliondo maana nina ushahidi dada mmoja tupo naye kwenye mkutano hapa amerudi Jana alienda last week, AMEPONA MTOTO WAKE ALIKUWA NA TATIZO LA KIBOFU CHA MKOJO NA KISUKARI. KWA HIYO MSIPUUZE NA WATU NI WENGI WANAZIDI KWENDA HADA VIONGOZI WAMESHAENDA WAMEKUNYWA SIKU NYINGI SANA.

HABAGUI NA HANA TAMAA YA PESA AMESHAKATAA MAGARI NA HATAKI KUSIKIA MTU HAFUATI FOLENI, KWA SAA ANATOA MAGARI 200 kwenye foleni. Ukinywa unapona hapo hapo, MAGONJWA YOTE
 
Imani haipimwi jamani...huu ni uingiliaje wa haki ya kuabudu(dini)
 
Ujumbe mzuri. Thanks!

Lkn hili neno in bold lina-apply kwa Mungu pekee, at least in this case: "Loliondo ni uhakika".
 
Na huyu dada naye alikuwa alikuwa na matatizo ya kukosa hamu ya kula sasa yuko fiti na anasema mtoto wake alikuwa hospital kila mara mpaka amemaliza sh mil 6 lakini hakupona baada ya kupata ushuhuda wa baba yake huko arusha kuwa amekunywa ile dawa na alikuwa na hiv amepona naye akaambiwa mlete mtoto wako alienda last week na ametumia siku tano kupata tiba na mtoto wake ni tsh 500 tu. Kwa hiyo kama huaamini utabaki na ugonjwa na kuutibu kwa tsh mil 10 ili hali ukienda you can use laki tatu kwa safari maana gharama zimepanda..................
......................
Nenda
 
Na huyu dada anasema mtoto alikuwa akokojoa kila wakati na sasa hakojoi tena
 
Imani haipimwi ni kama tu wanasayansi wanavyoamini hakuna Mungu, ndivyo na nguvu ya Mungu ni ngumu kuithibitisha kwa maabara, utathibitisha uponyaji lakini huwezi jua inafanyaje kazi. Kwa hiyo imani ni kuamini mambo yasiyoonekana kwa macho.
 
Ama kweli ni nguvu za mungu hizi. Viongozi wenye visukari na hiv wameshaenda na wamepona
 
Back
Top Bottom