#COVID19 Babu wa Loliondo: Nileteeni wachache wenye Corona waone!

#COVID19 Babu wa Loliondo: Nileteeni wachache wenye Corona waone!

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Asema watu waende wapate kikombe amesema hakuna ugonjwa unaoshindikana kutibika kwa dawa zake alizooteshwa na Mungu.

---

WAKATI Dunia ikiwa kwenye taharuki kubwa ya kupambana na maradhi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona baada ya kuendelea kuua maelfu ya watu duniani, Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo ameibuka na kuiomba Serikali kupeleka wagonjwa wa Corona kupata kikombe cha dawa.

Akizungumza jana Aprili 22, 2020 katika mahojiano kwa njia ya simu na kituo cha redio cha Clouds Fm kupitia kipindi chake cha Jahazi, Babu wa Loliondo amesema anashangazwa na ukimya ambao Serikali imekuwa ikiufanya wakati yeye amekuwa akitoa dawa inayotibia magonjwa yote.

“Ndugu mtangazaji hii dawa ninaitoa kwa masharti ya Mungu, na imekuwa ikitibia watu wengi sana na magonjwa yote wanayoumwa, lakini tangu ugonjwa huu kuibuka nashangaa Serikali haileti watu, mimi nawaomba walete watu wachache kwa majaribio wataona maajabu ya dawa hii,” alisema.

Hata hivyo amesema hali ya ukimya ambayo imekuwa ikiendelea kwa watu kutofika kunywa dawa kujitibia maradhi ya corona umekuwa ukisababishwa na chuki ya baadhi ya watu dhidi yake ambao wamekuwa wakimuonea wivu kwa kumtangazia mambo mabaya.

Alipotakiwa kuwataja watu hao wabaya alisema muda ukifika atawaweka hadharani lakini kwa hivi sasa ataendelea kukaa kimya na kwamba bado watumiaji wa dawa yake wataendelea kutoa Tsh500 kwa kuwa bei hiyo ndio aliyooteshwa na kuagizwa kuitoza na sio vinginevyo.

Aidha alipoelezwa kuwa ugonjwa wa Corona hauruhusu watu kusafiri kwa kuwa utasababisha maambukizi mengi na hivyo kwanini yeye asisafiri kuwapelekea dawa wagonjwa huko walipo, alisema kuwa tangu alipooteshwa na Mungu na kupewa dawa hiyo aliagizwa iwe inatolewa Loliondo katika eneo lake pekee na hivyo hatoweza kusafiri.

“kwanini waendelee kufungia watu huko na wasiwalete hapa kupata dawa? Kama mtu anaumwa sasa ni bora afungiwe au afike kunywa dawa?,”alihoji Mchungaji Ambilikile Mwasapile.

Mchungaji Mstaafu wa KKKT, Ambilikile Mwasapile maarufu kama ‘Babu wa Loliondo’ anayeishi katika mji wa Samunge Loliondo, Wilayani Ngorongoro katika miaka ya karibuni amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kutangaza kuoteshwa kupata dawa ya kutibia maradhi yote sugu ikiwemo Ukimwi, saratani na sukari na hivyo maelfu wa watu kutoka ndani na nje ya nchi kufika kwake kupata tiba hiyo.
 
Leo katika moja ya kipindi kupitia Radio cloudsfm baadhi ya watangazaji akiwemo Dr Isack Maro, Musa Hussein na Mina Ally waliongea na Babu wa Kikombe wa Loliondo Mchungaji Ambilikile Mwasapile kwa njia ya mawasiliano ya simu kuhusu ugonjwa wa korona na Babu alisema:“anashangaa hadi sasa hakuna kiongozi wala mtu yeyote ambae aliyemuuliza suala la dawa ya korona bali anayo na inafanya kazi”

Akiwa anaongea na Jahazi ameombwa awafuate wagonjwa ili akawape dawa,ila amesema hawezi kufanya hivyo bali wampelekee hao wagonjwa kule awape kikombe na watapona“angalau wachache tuu,ili watu waamini kupitia dawa yake aliyooteshwa na Mungu”,hawezi kutoka kule kwenda kutafuta watu.

Na pia amesema watu wanampiga sana vita ni kwa sababu dawa yake aliyooteshwa na Mungu inaharibu biashara zao.

Amesisitizia sana nileteeni wachache muone!!

Pia amesema“huu ugonjwa umeonekana umeanzia kwa watu wakubwa na maarufu ndio maana watu wanaogopa”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clouds FM radio ya jijini Dar wamezungumza na Babu wa Loliondo. Akihojiwa na watangazaji Dr Isack Maro, Musa Hussein na Mina Ally kwa njia ya simu, amekiri kikombe chake kupitia mti aliooteshwa na Mungu kinatibu pia Corona.

Alipoulizwa kwanini Asihamishie kikombe chake kwenye kambi au wodi za quarantine za corona, akadai kikombe kinafanya kazi huko Samunge Loliondo alipooteshwa na sio kwingineko. Amedai hatoi kinga kwa watu ambao hawaumwi bali anataka wagonjwa wa corona waliothibitishwa na daktari.

Ameulizwa kuhusu watu kuambukiza wenzao njiani wakati wakiletwa kwake lakini hata hivyo hakusikia vizuri hivyo kushindwa kujibu swali hilo. Amedai baadhi ya watu wanamuonea wivu kutokana na kikombe chake.
 
Anasema mti ni ule ule, siku za kupona hazijulikani ila ni muda mfupi. Kuna watu anawanyima mkate ndio maana wanampiga vita. Mungu hajamruhusu kwenda nje ya Loliondo.
 
Back
Top Bottom