Baby Kabaye na Hassani Ngoma tambueni Chato haina Ikulu ndogo, Ikulu ipo Geita Mjini

Baby Kabaye na Hassani Ngoma tambueni Chato haina Ikulu ndogo, Ikulu ipo Geita Mjini

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Jamani, tuelimishane kidogo Chato ni Makazi ya Rais, sio Ikulu ndogo Ikulu ndogo ipo hapa Geita mjini na Chato ni miongoni mwa Wilaya zilizopo mkoani Geita.

Ninachokijua mimi ni kuwa Rais wa Tanzania alitambua mapema yakuwa akiwa ndani ya Ikulu kubwa hizi kwa maana ya DSM na Dodoma miingiliano inakuwa mikubwa sana kuepuka ilo ndio maana aliamua kwenda kufanyia kazi Wilayani Chato Nyumbani kwake na si Ikulu ndogo Rais wa Tanzania hayupo ikulu yupo nyumbani kwake.

Ni muhimu ili lieleweke vyema, Rais hayupo Ikulu ndogo wala Ikulu kubwa yupo nyumbani kwake akiendelea na shughuli zake za kulijenga Taifa.

Binafsi mimi sipingani na yeye kuwa kwake maana na yeye ni mtu ana roho, na hata angekuwa ndani ya hizo Ikulu bado yeye sio nesi kama ambavyo watu tunataka awe, yeye ni Rais angebakia hivi hivi tunavyo muona.

Angalizo, na ninachokipinga kama ni kweli kutokumuona akishirikiana na Marais wenzake katika vikao vya mikakati ya kujikinga na maradhi haya ilo mimi siungani naye kama anashindwa yeye kulingana na mazingira au miundo mbinu ya Chato haiko sawa angeteua wawakilishi

Ingawa siamini katika miundombinu maana nakumbuka hapo alipo mandenge yalisha wai kutua yametua.

KUHUSU NYINYI WATANZANGAZAJI KUITWA VIBARAKA!
KATIKA ili mimi sio Mtanzania niliyopo ng'ambo lazima tukubaliane kuwa mmekuwa mashabiki wa vitu vingi vya ovyo, kuliko enzi za yule bwana alie kula uteuzi na yule bwana sijui kama alishawai kuwa mwanachama wa chama cha mapinduzi kwani aliweza kuwahoji vizuri sana pasipo kujali nafasi zao na hata alipoteuliwa MH Rais katika uapisho alisema kabisa kuwa huyo bwana alikuwa akiwahoji wenzake maswali magumu sasa amempa nafasi ili nae akahojiwe kama alivyokuwa akiwakaanga wenzake.

Sasa hivi kweli Hassani Ngoma kweli wewe ni msomi mwandishi unashindwa kujua kuwa Chato sio ikulu na haina Ikulu pale?

Nyinyi kama wanahabari mntakiwa kwenda mbali zaidi na kujifahamisha na kuwajuza watazamaji ni shughuli gani ambazo Rais wa nchi anaweza kuzifanya akiwa kwake na zipi hawezi, je sheria za nchi yetu zinamruhusu yeye kufanyia kazi nyumbani kwake?

Je, kwanini Rais, hashiriki vikao na marais wenzake?

Je, kamati iliyoundwa kuchunguza Mahabara inatakiwa kufanya kazi muda gani? je wakati kamati inafanya uchunguzi na tunajuzwa mahabara iko moja je zanzibari inapimia wapi mbona wao wanatangaza? wanapimia WAPI?

Leo namwona Hassan Ngoma anatetea Mh Spika kwa mambo ya hovyo anayo yasema hivi ni nani hasiyejua kuwa huyo Spika anafanya mambo ya ovyo? kimsingi nilitegemea hapo kipindi kinawaoji wanasheria manguri, maspika waliopita na kuoji pande zote, hivi mnajua kuwa Mwanahabari nguli anaweza kuwa chanzo cha habari kwa nini hamtaki jukum ilo?sio mnajadiri hata vitu vinavyokinzana katika taifa.

Nianzie hapo.
 
Mkuu kila media inasera zake za utangazaji ili kuendesha biashara yao

Huwezi kufurahishwa na kila media, chagua inayokufurahisha uangalie

Ukitaka kuona Chadema inapambwa Angalia Chadema t.v.
 
Hao watangazaji wanadhani watz wote ni hamnazo kama ndugu zao waliwaacha huko vijijini.
Hawajui tu kuwa wanajipotezea credibility ya kipindi chao na wao wenyewe.
 
Media zapaswa kuwa objective siku zote yaani zisiegemee upande mmoja. Ndio maana wanaambiwa kubalan e story.

Sasa issue Kama ya spika ilipaswa kutafutia wanasheria nguli mmoja au wawili former spika say Makinda mwanachadema na mwanazuoni walau wakupe maoni yao.

Based kwenye maoni yao utaona wapi wanakubaliana na wapi wanatofautiana.

Hilo ndio watangazaji wangetolea maoni na sio kuamka walikolala na kusema fulani yupo sahihi au wrong pasipo kupata independent opinion.
 
Wengi wa wanahabari nchi hii ni wasaka vyeo na waoga wa maisha kinoma na kwa hilo si walahumu sana sababu hii awamu nayo sio salama kwa wananchi wake wenye mawazo tofauti.. .lakini wanachosahau ni watanzania wanaelewa sana kinachoendelea na tunapuuzia na kuwapotezea tu.
 
Hakuna msomali anaitwa baby. Wasomali hawaiti mandazi mahamri. Watu wa mombasa ndio wanaita mahamri. Tatizo la watu wa nyagwale wakiona mtu mweupe wanaita mwarabu au msomali

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu majina ya siku hizi hayapo kama zamani ndio maana tuna waha wanaitwa precious , Msukuma anaitwa Princess nk
na kuhusu Mahamri mimi nimewahi kuwasikia Wasomali wakiita hivo
 
Back
Top Bottom