Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Watu wengi ambao lugha yao ya kwanza ni Kiswahili wenye matatizo ya kusoma, kuandika na kusema Kiingereza hawajaelewa jambo moja, na jambo hili ni kati ya vyanzo vya aibu katika kutojua kusoma, kuandika au kuongea kiingereza.So true!
She did a 360 to something that seemed as her weakness. To the point people suggested lucrative ideas to her, that she should make money out of her cheerfulness.
She's so funny, and she don't sweat it. It just comes out naturally.
Kumbe British council ndio walim approach!
That's nice. Vizuri cos Walipoa sana.
Kiswahili ni lugha yenye mantiki kuliko Kiingereza. Kiingereza ni lugha ambayo haijakifikia Kiswahili katika mantiki.
Nina maana gani?
Kwenye matamshi, katika Kiswahili, ukishajifunza matamshi ya msingi ya silabi tu, matamshi ni yale yale. Yanajirudia tu. Ni kama ukijifunza matamshi ya msingi, kwingine unaunganisha silabi tofauti kwa matamshi yale yale tu. Lugha ya namna hii inaitwa "phonetic". Huhitaji kujifunza kila neno jipya jinsi ya kulitamka. Kwenye Kiswahili, michepuko kutoka kanuni za matamshi ni michache sana.
Kiingereza kiko na michepuko mingi sana katika matamshi. Ni kama nusu ya lugha inafuata sheria za matamshi, halafu nusu nyingine inachepuka kutoka matamshi hayo. Kwa mtu aliyezoea lugha iliyonyooka kimatamshi kama Kiswahili, kujifunza Kiingereza ni kama kujifunza kutamka kwa makosa mengi sana.
Pia, kanuni za sarufi za Kiingereza nazo zinachepuka hivyo hivyo zikilinganishwa na Kiswahili ambacho kimejikita kwenye kufuata sheria sana. Kwa hiyo, tunapojifunza Kiingereza, tunakuta karibu nusu nzima ya lugha inafuata sheria za matamshi na sarufi, halafu nusu myingine haifuati sheria hizo. Ni lugha inayochanganya sana watu waliozoea lugha yenye mantiki na kufuata sheria kama Kiswahili.
Tatizo watu tunajiona dhalili kwa kutokujua Kiingereza, wakati kwa kiasi kikubwa, tunashindwa kujifunza Kiingereza kwa sababu kina makosa mengi ya kimantiki kwa michepuko karibu nusu nzima ya lugha kutoka kwenye sheria za matamshi na sarufi.
Kwa hiyo tunashindwa kwa sababu lugha yetu tuliyoizoea ni nzuri zaidi, si kwa sababu Kiingereza ni kizuri zaidi.
Ingawa siku hizi watu wengi tu hawajui Kiswahili wala Kiingereza.