Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Tukumbuke kwamba kwa sasa mziki wa bongo ni kama vile siasa za mpira wa Simba na Yanga,hata ije Azam au Gwambina fc au Namungo bado mashabiki wa hizi timu watakua ni wale wale tu watokanao na Simba au Yanga.
Hii ni sawa kwa Muziki wetu umegawanyika kwa team Kiba vs team Diamond,hata wasanii wenyewe na media zetu zimeathiriwa na hizi team mbili wapo waliopo upande wa Kiba au Mond hata kama wanajificha lakini ukweli ndio huo.
Sasa kwa nini nasema back to back ua kiba muhanga ni Harmonize? ni kwamba harmonize hana mashabiki wapya bado hajajenga himaya yake mwenyewe mashabiki wake ni aidha wale wasiompenda Mond yan wanaompenda Kiba,au wale wa Mond wasiompenda Kiba yani ni kama vile mashabiki wa Azam ni wale wale wa aidha simba wasioipenda Yanga ni kinyume chake ni kweli.
Kwa mantiki hiyo ujio wa Ali ni anguko kwa Konde boy sababu mashabiki wa Kiba walikua hawana option ya zaidi ya kujinasibisha na Konde pale alipojaribu kuonyesha ushindani kwa Mond sababu tu pia boss wao ni hasimu wa WCB,ujio wake sasa unafanya mashabiki waonyeshe rangi yao halisi na kurudi kwa msanii wao na kumuacha Msanii wao wa Kambo(Harmonize) mkiwa.
Hii inaweza kumfanya konde kupoteza muelekeo na kujikuta hana Sapoti kwa vile tu mashabiki wa KAMBO wamerudi kwa msanii wao mzazi.😊.
Harmonize anatakiwa kwenye huu mtifuano uliopo sasa acheze smart sana asijiingize kichwa kichwa anaweza kupoteza kote,mashabiki wa Kambo wana gubu kama kuku kishingo mwenye kifaranga kimoja.
Anyway tufurahi jamani maisha ni mafupi weekend ndo hii hapa na Mama Samia katingisha mwembe dodo maembe kedekede.