Back to square one

Back to square one

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Ramadhan Kareem na ftar njema,

Ni kweli, jasiri haachi asili Leo nimejikuta nimerudi Misri. Ni yale yale ya Kasie hakuna jipya, this time ni Toyota Hilux T CST kama sijakosea ila maelezo hapa chini ndo yatamjulisha who was in that Toyota Holux double cabin.

As usual vioo sio tinted hivo kumuona dereva kiurahisi nilimuona akiwa nyuma yangu anataka ku overtake na ilikuwa baada ya kuvuka mataa ya mlimani city na barabarani ya kuelekea Sinza.

The guy anaita alikuwa amevaa Tshirt body tite nyeupe na alikuwa a naongea na simu sikuitambua simu gani ila ilikuwa na cover jeupe. Niliendelea kumchungulia kwa kuibia tukiwa sambamba kuelekea mataa ya Ubungo.

Double cabin Toyota hilux ilikuwa ya grey metallic bad luck alielekea stand ya mkoa mie nikanyoosha kuendelea na mihanjo yangu. Ni kuwa najiskia raha kumuona mtu nikamzimia na kama hajui inakuwa tamu zaidi ya bao.

Wherever u r Toyota hilux double cabin driver itakuwa umeshajua kuwa ni wewe na muda ilikuwa kwenye saa kumi na moja kasoro jioni Leo hii. Kasie alikuwa anakuchungulia na kutabasamu pekeyake bila wewe kujua. The driver alikuwa six pack kifua wastani rangi kama yangu.I love that.

Kasie
 
Watu wengi hukosea
wengine jasiri,wengine mjasiri
but 'mjaa asili haachi asili' ndo sahihi

meaning mtu ambae mambo ya asili yamemjaa hawezi acha moja kwa moja

Kuna hii pia 'Mja wa hiana ana laana'.
 
Nafikiri sahihi ni 'mjaa hiana ana laana'

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford, Toleo la Pili, ni 'Mja wa hiana ana laana'.

Hiyo 'mja' maana yake ni binadamu/ mtu.

Hivyo, maana yake ni kwamba mtu aliye mchoyo ni amejaa laana ya uchoyo.
 
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford, Toleo la Pili, ni 'Mja wa hiana ana laana'.

Kamusi zinaandikwa na binadaamu
baadhi ya methali na misemo zina asili ya maeneo fulani
mfano labda 'msemo' umetokea Zanzibar
halafu kamusi inaandikwa na wajaluo wa Kenya so mistakes zipo

nafikiri pia hiyo space ndo kosa lilipo
nafikiri sahihi ni 'mjawa hiana' na sio 'mja wa hiana'

maana ikiwa mtu alie na hiana nyingi atakua na laana
 
Kamusi ni vitabu ambavyo haviandikwi tu bila kufanyiwa tafiti za kutosha na wataalamu wa lugha na isimu.

Na mara nyingi, kama wewe ni msomaji mzuri wa hivyo vitabu, utagundua kuwa huwa vinaweka tofauti za kilahaja zilizopo kwenye neno au msemo.

Na sijawahi kuona kamusi ambayo imeandikwa na watu wa nchi moja tu au kabila moja tu.

Hii ya 'mja' ni sahihi kwa sababu 'mja' hapo haimaanishi kingine zaidi ya 'binadamu/ mtu'.

Na si 'mjaa wala mjawa' kama unavyodhani wewe.

'Mja' ni neno sahihi kabisa la Kiswahili limaanishalo mtu/ binadamu.

Kwa hiyo, 'Mja wa hiana ana laana' maana yake ni kwamba 'mtu mwenye hiana/ choyo ni mwenye laana ya hiyo sifa ya uchoyo/ hiana'.
 
You could be right na hiyo methali ndo maana nilisema 'nafikiri'

Kuhusu kamusi mistakes nyingi sana zinatokea

wakati fulani neno 'ukwasi' lilikuwa linatumika sehemu ya kutumia 'ukata'
hadi wazee wa BAKITA walikemea na kupinga kamusi zilizo andika hivyo
now utaona kuna mabadiliko

mfano wazee wa kiswahili walisema tena on the record kabisa kuwa
neno 'maboresho' ni makosa na sio kiswahili ingawa bado linatumika
na si ajabu likawepo kwenye kamusi

wenyewe walisema hilo neno 'bora' liko hivyo hivyo
makosa mfano kusema 'taifa stars itafanyiwa maboresho'
inatakiwa uweke neno lingine kama 'marekebisho'
labda iwe 'taifa stars itafanyiwa marekebisho iwe bora zaidi....
 
Kamusi zinaandikwa na binadaamu
baadhi ya methali na misemo zina asili ya maeneo fulani
mfano labda 'msemo' umetokea Zanzibar
halafu kamusi inaandikwa na wajaluo wa Kenya so mistakes zipo

nafikiri pia hiyo space ndo kosa lilipo
nafikiri sahihi ni 'mjawa hiana' na sio 'mja wa hiana'

maana ikiwa mtu alie na hiana nyingi atakua na laana

Ushawahi kuisikia hii methali?

'Mja hatendi rehema ali hai duniani'?

Au hii....

'Mja akiteswa hafanyi machungu, hupiga shahada. kashukuru Mungu'.

Na hapo 'shahada' haimaanishi ile shahada ya kitaaluma, ujue.....

Kama wewe ni Muislam mzuri basi utakuwa unajua maana ya 'shahada' katika muktadha wa kiimani [hususan ya Kiislamu].
 
Nafikiri 'kupiga shahada' hapo ni ile ya kiislam...
 
Kuhusu kamusi mistakes nyingi sana zinatokea

Na ndio maana huwa zinakuwa updated kwa kutoa matoleo mapya kila mwaka au kila baada ya muda fulani.

wakati fulani neno 'ukwasi' lilikuwa linatumika sehemu ya kutumia 'ukata'
hadi wazee wa BAKITA walikemea na kupinga kamusi zilizo andika hivyo
now utaona kuna mabadiliko

Ngoja kwanza, kuna kamusi ambayo ilikuwa inafasili hilo neno kwa hiyo maana? Au kilichokuwa kinatokea ni watu tu kulitumia vibaya hilo neno katika mazungumzo yao?

Manake hilo la kutumia neno au maneno vibaya au visivyo hutokea sana na sababu yake kuu huwa ni ujinga tu.

Mimi nimeanza kusoma kamusi zamani sana na ninazo kamusi za zamani [hata ile ya TUKI ya mwanzo kabisa ninayo] na hilo neno wala lilikuwa halifasiliwi kihivyo hata hiyo zamani. Na hata kwenye kamusi za sasa wala halifasiliwi hivyo.

mfano wazee wa kiswahili walisema tena on the record kabisa kuwa
neno 'maboresho' ni makosa na sio kiswahili ingawa bado linatumika
na si ajabu likawepo kwenye kamusi

Unajua lugha ni 'dynamic'. Wakati mwingine misamiati huongezeka na wakati mwingine maana za misamiati iliyopo nazo huongezeka.

Sasa hao wazee inavyoelekea wao ndo wamekuwa 'stuck' na dynamism ya lugha imewashinda.

Kama wewe ni mpenzi sana wa lugha na ukuaji wake basi utakuwa unajua kuwa kila mwaka kamusi za Merriam-Webster na Oxford, kwa mfano, huwa zinaongeza misamiati mipya ya lugha ya Kiingereza kwenye kamusi[mfano Selfie, Staycation, Twerk n.k.] na pia huongeza maana za maneno kwenye misamiati ya zamani pale inapobidi.

wenyewe walisema hilo neno 'bora' liko hivyo hivyo
makosa mfano kusema 'taifa stars itafanyiwa maboresho'
inatakiwa uweke neno lingine kama 'marekebisho'
labda iwe 'taifa stars itafanyiwa marekebisho iwe bora zaidi....

Hahahaa ndo maana kuna watu huwa wanaona kuwa lugha ya Kiswahili haikui wala kupanuka kwa sababu ya fikra za hao waitwao "wazee wa Kiswahili".

Kiingereza kila siku kinaongeza misamiati mipya na hiyo huwa inakuwa influenced na mambo mengi tu yakiwemo teknolojia [selfie], hip-hop [twerk], na kadhalika.

Sasa kwa nini kwenye Kiswahili iwe kufuru kuongeza misamiati au maana za maneno yaliyopo?

Ni kitu au jambo gani ambalo ndo huamua kuwa sasa neno fulani ni neno rasmi katika lugha ya Kiswahili?

Lugha ni kitu ambacho hukua, hupanuka, na kubadilika.
 
Nyani Ngabu kila lugha ina wazee wanailinda hiyo lugha isije badilika kabisa na kuwa na lugha ingine
nna uhakika kamusi za UK zina tofauti na kamusi za USA

kwa vyovyote vile watu wa UK kuna baadhi ya misamiati watakuambia ya kwao ndo 'sahihi'
hata kama yaliyo popular ni ya USA......
 
Last edited by a moderator:
Hapa msachepusha uzi...kasinde hongera kwa ku crash wengine hatupati hiyo kitu
 
Uzi wa kasinde umekuwa jukwaa la lugha.
Kasinde endelea ku crash tu hvyohvyo. YOLO
 
Back
Top Bottom