BAD NEWS: Coastal V Yanga kugeuka mechi ya kirafiki?

BAD NEWS: Coastal V Yanga kugeuka mechi ya kirafiki?

Hii si ndiyo kamati ile ya siasa aliyoisema Mzee Tibaigana kwamba haina mamlaka kisheria kutoa adhabu badala yake ni kuthibitisha (Yaani akina tibaigana wakishatoa adhabu wao wanathibitisha).

FIFA wako very against na ushindi wa mezani ndio maana chombo husika kinalazimika kuitaarifu timu husika kwa maandishi kama kuna mchezaji yeyote asiyestahili kucheza.

Wote tuliona uwanjani kwamba cannavaro haukumpiga mtu yeyote zaidi ya kukimbia kimbia. Kama ripoti ya refa imesema alipigana je ilikuwa shared upande wa Yanga ili wajue kadi ya Canavaro ni ya kupigana?

Hivi report ya refa tangu lini ikawa final? mbona hawatuelezi kamisaa na vishika vibendera nao wamesemaje?

Tenga, Tenga, kama unanisikia nakuomba akili ikurejee utambua jinsi unavyoleta matatizo ya soka hapa nchini. Unakataa mtu kujihudhuru kwa nini wakati amefanya makosa ya kufanya kitu ambacho hana mamlaka nacho? kama sio sahihi kwa nini usimfukuze basi Tibaigana? Wewe ni kiongozi gani usie kuwa na uelewa kiasi hiki?
 
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha mchezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Aprili 2 mwaka huu) kupitia ripoti mbalimbali za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza umezingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji.

Kanuni hiyo inasema: “Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi toka TFF.”

Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezaji amekosa mechi mbili tu.

Pia klabu za Coastal Union na Yanga zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1).

Kamati ya Ligi pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.

Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Chang’walu na Hassan Mwinchum. Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad, Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.
 
hivi ni kwa nini clouds or shafi dauda ndio vyombo vya habari vinavyokuwa vya kwanza kujua habari hizi? au clouds na tff wanafanya kazi pamoja? wana yanga tunahitaji kuonyesha ujasiri dhidi ya clouds fm. na hizi point wamenyanganywa na kamati ipi wakati ile ya ligi mwenyekiti alishajiudhulu. namchukia shafi mno!

kumbuka clouds wameingia mkataba na simba kuhusiana na masoko.thus why wanamekua aka simba tv.kama ulisikia jahazi ya clouds ungesikia kibonde akiikampenia yanga inyanganywe point.
 
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha mchezaji Nadir Haroub Cannavaro kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Aprili 2 mwaka huu) kupitia ripoti mbalimbali za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza umezingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji.

Kanuni hiyo inasema: Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi toka TFF.

Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezaji amekosa mechi mbili tu.

Pia klabu za Coastal Union na Yanga zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1).

Kamati ya Ligi pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.

Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Changwalu na Hassan Mwinchum. Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad, Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.

Yes ni kweli canavaro alikua na kadi nyekundu(straight red card)ambayo inamuweka nje kwa kukosa mechi tatu kwa kumpiga refa,ila kamanda Tibaigana alisitisha adhabu zote zilizohusu makonde,but wenye kadi watatumikia kama kawa,sasa kwa inshu ya Canavaro alitakiwa kukosa mechi3 but kwasababu kamanda alisimamisha adhabu zao sasa ilibidi akose mechi mbili tuu,sasa hapo mbona kama pale TFF kuna madudu?????????
Kama mpira umewashinda waende wakaombe kazi AZAM!
 
katib wa kamati iliyoihadhibu yanga ni kiongozi wa juu wa azam,kwenye hiyo kamati pia kuna katibu wa simba.watangazaji wa clouds tawi la simba so nimepata jibu.
 
KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), imeipoka
Yanga pointi tatu baada ya
kumtumia beki Nadir Haroub
'Cannavaro' katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal
Union. Hiyo ina maana kuwa Yanga
ambayo ilishinda bao 1-0 na
kufikisha pointi 46 sasa
inashuka mpaka pointi 43,
lakini inabaki nafasi ya tatu
huku Coastal Union iliyokuwa na pointi 29 sasa inakuwa na
pointi 32 na kushika nafasi ya
tano. Kamati hiyo ilikutana jana
Jumatatu usiku chini ya
Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Ligi ya TFF, Said
Mohamed, ambaye aliandika
barua ya kujiuzulu, lakini akakataliwa na Rais wa TFF,
Leodegar Tenga. Katika kikao hicho ilibainika
kuwa Yanga ilifanya kosa
kumtumia Cannavaro kwa
sababu alitakiwa kukosa
mechi tatu kutokana na
kupewa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwamuzi, Israel
Nkongo. Kamati hiyo ilifikia uamuzi huo
baada ya kupitia ripoti ya
mwamuzi Nkongo, ambaye
aliandika kuwa alimpa kadi
Cannavaro kutokana na
kupigana uwanjani. Cannavaro alichezeshwa na
Yanga katika mechi hiyo baada
ya adhabu yake ya kutocheza
mechi sita kusimamishwa na
Kamati ya Nidhamu na
Usuluhishi ya TFF chini ya Alfred Tibaigana. Hata hivyo, Coastal Union,
ilikata rufaa kupinga
kuchezeshwa kwa Cannavaro. Cannavaro alitakiwa kukosa
michezo mitatu dhidi ya
African Lyon, Villa Squad na
Coastal Union kulingana na
adhabu ya kadi aliyoonyeshwa. Kamati ya Ligi ya TFF hivi
karibuni iliwafungia Cannavaro
(mechi sita), Stephano
Mwasika (mwaka mmoja),
Jerry Tegete(miezi sita),
Omega Seme na Nurdin Bakari mechi tatu kila mmoja kwa
kosa la kumpiga mwamuzi
Israel Nkongo katika pambano
dhidi ya Azam FC. Tibaigana alitumia Kanuni ya
129 ya Kanuni za Adhabu za
FIFA, ambayo inaipa kamati
yake mamlaka ya kusitisha
utekelezaji wa adhabu yoyote
ile pale anapoona kwamba ukiukwaji unaolalamikiwa
hautaweza kupatiwa ufumbuzi
wa haraka, isipokuwa uamuzi
wa refarii. Yanga inaonekana walifuata
kanuni ya 25 kifungu (b)
ambayo inasema; mchezaji
atakayetolewa nje kwa kadi
nyekundu ya moja kwa moja
(straight red) atakosa michezo miwili. Lakini kifungu (f) kipengele
cha iii kinasema mchezaji
atakayepewa kadi nyekundu
kwa kupiga au kupigana
atakosa mechi tatu. Lakini jana Jumatatu mchana
Mwanaspoti ilipomtafuta
Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi,
Wales Kalia kabla ya uamuzi
huo wa usiku, kuhusu
mkanganyiko huo alisema: "Kama kanuni zinavyosema
mchezaji atakayetolewa nje
kwa kadi nyekundu baada
kupata kadi mbili za njano
katika mchezo wa ligi
hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu
yake. "Mchezaji atakayetolewa nje
kwa kadi nyekundu ya moja
kwa moja (straight red)
atakosa michezo miwili,
mchezaji atakayeonywa kwa
kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza
mchezo mmoja unaofuata na
mchezaji atakayeonyeshwa
kadi nyekundu ya moja kwa
moja( straight red) kwa kosa la
kupigana uwanjani, kupiga kiwiko au kuleta fujo yoyote
uwanjani atakosa mechi tatu
na faini ya Sh 500,000. " Sasa kulingana na ripoti ya
mwamuzi na kamisaa
iliyoletwa kwetu, ilionyesha
Cannavaro alipewa kadi
nyekundu kwa kosa la kuleta
fujo uwanjani hivyo anapaswa kukosa mechi tatu na faini ya
Sh 500,000 hiyo ni adhabu
kulingana na kanuni za ligi,
lakini baadaye Kamati yetu
ilipokaa ndipo tukamuongezea
adhabu nyingine ya kukosa mechi tatu zaidi kwa zile fujo
zilizotokea kwa hiyo
ikatangazwa kuwa atakosa
mechi sita. "Lakini Mwenyekiti wa Kamati
ya Nidhamu na Usuluhishi,
Alfred Tibaigana,
alizisimamisha adhabu za
kifungo cha wachezaji hao
lakini akasema adhabu za kadi uwanjani zinabaki pale pale,
hivyo Cannavaro alistahili
kukosa mechi tatu." Hivyo kanuni ya 25 kifungu f
kipengele cha (viii) ndicho
kinachoitia matatani Yanga
ambacho kinasema: "Timu
yoyote itakayomchezesha
mchezaji aliye chini ya adhabu kwa mujibu wa kanuni hii
itapoteza mchezo huo na timu
pinzani itapewa ushindi."
 
hahahahahahahahahaha ngoja aje yahoo na balatanda....kwisha kazi ubingwa ni SIMBA au AZAM
 
Wamsubiri Tibaigana labda atawarudishia tena. Mi nafikiri Tibaigana ni mchezaji wa 12 wa Yanga
 
Hizi habari nyingine za kipuuzi siyo hadhi ya JF, Yanga iliifunga Coastal goli 1 tu sasa hayo magoli matatu yanatoka wapi? this thread is total nonsense.

Hizo point na magoli yanakatwa kwenye point zake za jumla.
 
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha mchezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Aprili 2 mwaka huu) kupitia ripoti mbalimbali za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza umezingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji.

Kanuni hiyo inasema: “Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi toka TFF.”

Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezaji amekosa mechi mbili tu.

Pia klabu za Coastal Union na Yanga zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1).

Kamati ya Ligi pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.

Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Chang’walu na Hassan Mwinchum. Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad, Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.

Source: shaffihdauda.com
 
mimi viongozi wa mpira bongo pamoja na viongozi wa club za soka huwa napata wakati mgumu sana kuwaelewa kwanza TFF kabla ya mchezo huwa wanapewa orodha ya wachezaji ambao timu itawachezesha kwenye huo mchezo je wao hawakuwa na kumbukumbu ya kufungiwa kwa canivaro? pili vongozi wa yanga pamoja na kocha wao papic walijua kabisa canivalo ana kadi nyekundu lakini wakamchezesha. wanafanya makosa ambayo yako wazi kabisa ambayo mimi sijawahi kuyasikia hata siku moja kweli ligi za ulaya.
 
wakuu fuatilia.

[h=3]YANGA YAGOMA KUPOKWA POINTI[/h]

KLABU ya soka ya Yanga imepinga kupokonywa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu na kamati ya Ligi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
iliyokutana juzi jijini Dar es Salaam na kuipa klabu ya Coastal Unionya Tanga.
Kamati hiyo imefikia hatua hiyo kutokana na Yanga kumchezeshamchezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,
ambapo Coastal ilipinga kuchezeshwa kwa Cannavaro ambaye alikuwaakitumikia adhabu ya kutocheza mechi sita.
Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kuwa hawajaridhisha na maamuzi hayo kutokana na ukweli
kwamba kamati ya Ligi haikuwa na mamlaka ya kutoa uamuzi huo kwani kikanuni kamati ya Nidhamu na usuluhishi ndiyo ilipaswa kupiatia rufaa
hiyo.
Alisema wanasubiri maamuzi ya kikao cha kamati ya nidhamu na usuluhishi ya TFF kilichotarajiwa kufanyika jana jioni kwa ajili yakupitia rufaa inayohusiana na adhabu za wachezaji wa Yanga iliyotolewana kamati ya Ligi na ndipo watajua nini cha kufanya.
“Kwa sasa hatuwezi kuongea zaidi kwani tunasubiri maamuzi ya kikao cha kamati ya nidhamu na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya…kwa kweli
tumejipanga ipasavyo,”Alisema Sendeu.
Awali,ofisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema jana kwamba uamuzihuo ulifanywa na Kamati ya Ligi kwa kuzingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji.
Kanuni hiyo inasema: “Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu
(3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi
toka TFF.”
“Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibuwa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezajiamekosa mechi mbili tu,”Alisema Wambura
Wambura aliongeza kuwa kamati hiyo pia imezipiga faini ya shilingi500,000 kila moja klabu za Coastal Union na Yanga kutokana namashabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo.
Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1).
“Kamati hiyo pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye
orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake
ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni
kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa
Yanga, Hamis Kiiza”, Aliongeza Wambura.

Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba
wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni
Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Chang’walu na Hassan Mwinchum.
Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad,
Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.
 
Back
Top Bottom