Badala ya kuilipisha Simba, tuhoji zoezi la kubadili viti vya Uwanja wa Mkapa limeishia wapi?

ukiacha unazi pembeni sisi mashabiki wa simba sc hatukuwa na sababu za kufanya uharibifu ule na kuwapiga wapinzani wetu sababu:

1. mpira umeisha na point 3 tumechukua.

2. tulipaswa kuwaacha wageni waingie matatizoni kwa kumpiga mwamuzi.

3. kwa vurugu zile tumeiweka timu yetu matatani itakapokwenda tunisia maana washabiki wao wanaweza kuwashambulia wachezaji wetu.
 
Mashabiki wa simba sc ni washenzi toka tafsiri ya kimombos, "simba sc fans are savages"

A savage means a brutal person
 
Upumbavu mkubwa.Sipendi kabisa mtu atetetee ujinga kama huo.Lazima wote waliofanya uhuni huo wakamatwe na wachukuliwe kama wahujumu uchumi.

Huo uwanja hautumii pesa za wajomba wao bali sisi watanzania tunaolipa kodi nyingi tu kila mwezi.

Serikali isicheke kabisa na wahuni hao.
Mimi ni Simba ila nilichukizwa sana na huo uhuni.Kama mtu alikuwa na hasira za kipuuzi,kwa nini asirushe simu yake?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Ama kwanini hawakujirusha na kujipasua pasua, kama hawakuwa.na hizo simu
 
Haihalalishi matendo ya simba; siyo mara yao ya kwanza kun'goa viti hivyo; walifanya hivyo miaka kadhaa iliyopita sikumbuki ilikuwa mechi ganii. Simba ina mashabiki wajinga na wapumbavu sana wanaodhani kubomoa viti vya uwanja ndiyo kuonyesha ubora wa timu.

Sasa hivi inatakiwa serikali iweke utaratibu wa kuwafunga pingu mashabiki wa SImba wanapoingia uwanjani ili wasitumie mikono yao kufanya uharibifu wa uwanja. Baada ya mchezo wanaondolewa pingu hizo wakiwa mlangoni kutoka nje ya uwanja.
 
Mambo ya siasa. Hujaanza kuwa kumshukuru mama
 
Hauna hoja wewee. Ungekuwa na hoja ningekujibu.
 

Ukiacha wachezaji na staff wa Sfaxien waliohusika na vurugu, mashabiki waliohusika na vurugu ni wachache sana, hawafiki hata 50. Hauwezi kuhukumu tukio kama hilo kwa klabu nzima. Tukio hili lingeweza kuwa controlled vizuri tu na walinzi wa uwanjani.

Pia ukiangalia vizuri marejeo ya video mbalimbali utagundua wale waarabu waliliamsha makusudi ili kupata reaction ya mashabiki na hata walinzi walipokuwa wanawatuliza na kuwatuliza mashabiki, wao ndiyo zaidi pepo la vurugu likawa linawapanda. Kuna video moja staff wa Sfaxien alimpiga ngumi ya kichogo mlinzi wa uwanjani aliyekuwa anatuliza mashabiki wa jukwaani bila sababu yoyote halafu akajificha ili asijue ni yeye. Katika hili mnalaumu watu wasio sahihi.
 
Hiyo haiwapi haki wahuni wachache kung'oa viti
 
Timu ya mpira ni taasisi,ikumbukwe kila taasisi ina miundombinu yake, viwanja(vya mazoezi na vya mechi) inapotokea taasisi kubwa kama simba kukosa uwanja wake wa nyumbani haya ndio matokeo yake.
 
Hamna sababu ya msingi ya kung'oa Viti
Kama walikarisirika mbona hawakurusha simu zao, kwanini wasitumie mikanda.

Yaani huu uhuni haukubaliki
 
Timu ya mpira ni taasisi,ikumbukwe kila taasisi ina miundombinu yake, viwanja(vya mazoezi na vya mechi) inapotokea taasisi kubwa kama simba kukosa uwanja wake wa nyumbani haya ndio matokeo yake.
Kukosa uwanja siyo sababu ya msingi, tatizo ni nidhamu binafsi, (self discipline or self-control
 
Na wewe unawatetea wahuni waliokula bilioni 30 ukarabati wa uwanja walisema watabadilisha viti mimi nawasapoti fans wa Simba unaona uchungu wa viti 256 ila huna uchungu na waliotafuna b 30 uenda na wewe upo kwenye mgao.
 
Mkuu hapa unajaribu kumaanisha kwamba kama viti vingebadilishwa basi mashabiki wasingeweza kuviharibu?
 
Mkuu hapa unajaribu kumaanisha kwamba kama viti vingebadilishwa basi mashabiki wasingeweza kuviharibu?
Hilo pia linawezekana ingawa haikuwa lengo la uzi huu. Inawezekana uchakavu ulipunguza thamani ya vile viti katika macho ya wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…