Naona wazi Simba, Yanga na Azam wamechagua kuipuuza hii michuano tajwa, tena hii ni mara ya pili mfululizo...
Kama hoja ni zawadi zinazotolewa kuwa ni ndogo, mbona wakialikwa kushiriki Mapinduzi cup ni lazima waende iwe mvua iwe jua tena katikati ya ligi...Je ina maana SMZ wanaweka mzigo mkubwa kuliko cecafa?
Kama Tatizo ni ufinyu wa muda/ ratiba...Kwanini wasipeleke junior squads.
Hizi timu zina wachezaji wa U-20.....lakini pia zina wachezaji ambao hawakutumika kikamilifu kwenye msimu uliomalizika.
Kwanini wasingepeleka wale unused substitutes... kama akina Abtwalib Msheli & etc wakiungana pamoja na wale U-20 kuliko kuacha kabisa.
Haya mambo yanawezekana under smart technical director.
Kuna kitu nimekifurahia sana kinachofanywa na baadhi ya vilabu vya ulaya.....Wanakuwa na timu A, B, sometimes hadi C..na zote zipo kwny ligi tofauti tofauti za ngazi tofauti....nchi hiyohiyo.
Mfano pale ureno, ipo Fc Porto unayoijua wewe, ipo ligi kuu...Hapohapo ipo Fc porto B...hii ipo championship ya palepale ureno,
Ipo Fc porto C, yenyewe ipo third tie..daraja la 3.
Hizo Porto 1,2,3 zipo chini ya umiliki mmoja na kiuhalisia timu ni ileile ila wachezaji wanaweza kutumika interchangeably...ila hizo Porto 2&3 zimetengenezewa kanuni ya kutopanda daraja isipokuwa kushuka.
Faida yake ni kwamba timu inaweza kuteremka dimbani mara 2 ama zaidi katika viwanja tofauti tofauti siku hiyohiyo...
Faida nyingine inawahakikishia wachezaji wote kutumika...
Farid Mussa aliwahi kusajiriwa na CD Teneriffe kule Spain....baada ya kiwango chake kutowaridhisha ilibidi ahamishiwe Tenerife 2 ambayo nayo ilikuwa ndani ya ligi fulani hukohuko Spain.
Huu mfumo ungekuwepo Tanzania.. ungeleta tija kamahv timu hazishiriki wakati zimejaza wachezaji wasiopata nafas ya kutumika hadi msimu unaisha.