Badala ya kununua Toyota Harrier nunua hii gari

Hayo magari Ili ufanikiwe nunua brand new.
Kinyume chake umenununua mke wa mtu ambaye ni mzee na Ana Watoto 9.
Matajiri wananunua hizo machine warranty ikiisha wanachukua chuma kingine, wajerumani weusi wa hapa kazi Yao Ni kununua magari ya ujerumani ya miaka 10's huko iliyopita halafu anakuuliza kwa kebehi 'unajua mziki wa mjerumani wewe' in Polepole voice
 
Weka tu gari ingine,kama nia yako si Harria. Lakini si Range Rover. Hiyo sio gari. Inahitaji umakini kwa kila kitu. Haitakiwi kumuachia mtu mwingine asielijulia, litarudi linavutwa kwa gharama yako.

Sina mzuka kabisa na huyo mdudu. Kuna kile JEEP WRANGLER. Naikubali sana ile ngoma. Mwenye hela aniazime mara moja jamani. Nikavute huyu mnyama huyu. Kama nachelewa hivi
 
Jeep Wrangler (TJ) nimeiendesha Sana ,haina u-luxury wowote na kwa mwendo mrefu wa kila siku inachosha, Nilikua naipendea Ile kua topless,hii gari ukiizoea Ina bond 1 ya hatari Sana.

Hiki kizazi Cha Rubicon/JL sijaiendesha lkn naona Kama itakua na u-luxury.
 
Basi wameziboresha. Nimekutana nayo Dubai anaiendesha mzungu mmoja,nzuri sana. Tulienda nae mpaka airpot. Iko vizuri. Tukaongea nae zilivyo. Ziko vizuri. Japo ile ni reft hand lakini naamini hata right hand za sasa zitakuwa hivyo

Naitamani sana hii ngoma JEEP WRANGLER
 
Dude lenyewe ukiliona tu linavutia kishenzi mzee,all the best.
 
Bei kupunguzwa Sana si kigezo cha kukimbia kununua gari. Nilishawahi kununua gari imepunguzwa 67% ya Bei ya awali na bado inatembea fresh tu

 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kuna fuga ipo modified nayo ina cc 4200 engine invo unguruma tu, Na harrier yako utakiri hapa mwanaume kapita
Hiyo itakuwa haili,bali inabwia,hivi wazungu kututengenea migari yenye miinjini kubwa hivyo lengo lao hizo gari tuzione barabarani tu tusizimiliki waendeshege wao tu auuu?
 
Hiyo itakuwa haili,bali inabwia,hivi wazungu kututengenea migari yenye miinjini kubwa hivyo lengo lao hizo gari tuzione barabarani tu tusizimiliki waendeshege wao tu auuu?
Starehe tu kama unauwezo unavuta kitu safii. Siku izi watu wanaagiza gari na spare zake muhimu kabla hazijaaribika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…