Badia za dengu na chatne

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

Unga wa dengu 1 cup
Kitunguu maji 1/4...kata ndongo ndogo
Pilipili kijiko 1 cha chai..
Hamira 1 tea spoon.au baking powder
Pilipili mboga 1/4...kata ndogo ndogo
Chumvi kiasi
Curry powder 1tea spoon
Maji 1/2 kikombe
Mafuta ya kupikia

Namna ya kutaarisha
Changanya unga wa dengu na kitunguu maji
Weka pipilipili mboga,pilipili ya kuwasha,chumvi,curry powder
Mimina maji kidogo kidogo huku wachanganya mchanganyiko wako kwa mikono safi
Ukimaliza weka sehemu ya joto kwa dakika 30

Weka mafuta kwenye karai na choma badia zako hadi ziwe brown..

Chatne
Nazi 1/2
Pilipili ya kuwasha
Chumvi kiasi
Ndimu/ limao

Namna ya kutaarisha
Kuna nazi yako
Weka pilipili,chumvi na maji kidogo saga kwa blender hadi iwe laini
Weka kwenye bakuli tia ndimu/limau.

Badia na chatne tayari kwa kuliwa
 

Attachments

  • 1384674794025.jpg
    71.3 KB · Views: 1,033
  • 1384674826412.jpg
    54.4 KB · Views: 694
.
Shosti Aaaa aa aa.... hapo Toronto nasikia umechuwa chain of Fast Food line hiyo inapeta " tuje kujibwaga huko ?" Bajia hizo umezipatia 100% !! MashAllah mkono wako wa kheri!
 
Sie tunawekaga pia mabiringanyi yale madogomadogo na tunagawanya info two halves!
 
Hlf sijala siku nyingi hizo badia, tushazoea Ramadan mpm Ramadan.
Thnx habibty
 
Siku moja nataka tupikeee mpaka mkeka ujae mahanjumati
 
.
Shosti Aaaa aa aa.... hapo Toronto nasikia umechuwa chain of Fast Food line hiyo inapeta " tuje kujibwaga huko ?" Bajia hizo umezipatia 100% !! MashAllah mkono wako wa kheri!

Hahahahahahaha ahsante shosti...
 
Sie tunawekaga pia mabiringanyi yale madogomadogo na tunagawanya info two halves!
Halafu unafanyaje shosti?
Maana kuna wengine pia hukisaga saga viazi vya vile vidude vya kuparia....ntaiweka recipe yake inshaallah
 
Halafu unafanyaje shosti?
Maana kuna wengine pia hukisaga saga viazi vya vile vidude vya kuparia....ntaiweka recipe yake inshaallah
Yaani hayo mapande ya biringanya wachovya kwenye huo mchanganyiko wa dengu kama unavyochanganya mapilipili mboga na vingenevyo
 
Hapa nlipo harufu ya Badia imenimaliza, Pumzi zimesimama je, nikiona kwa macho sintazimia.... akill haniyaa, siha wa Afya !!
 
mpenzi! mandazi nilipika tena basi! lol na ndo hadi weekend! thanx farkhina kwa mapishi motomoto unachangamsha jamvi na kutupa apetite
 
Ahaahahahahha kwani hujawahi kuona?
Ukhtii ..Maakulati yako unapamba kaDhahabu (multiculture) kwani kila mtu hupenda dhahabu... hivo taswira za maakulati zavutia. mie badia nshaziona ila kuzikaanga sijawahi..
kind thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…