Badia za dengu na chatne

Badia za dengu na chatne

Km giligilani ndo unakusudia kotmir basi itanoga ndio.

Yeah itanoga shosti unaujua mvuje? Mama angu anaupenda sana akipika badia lazima aweke hata mie napenda hususan kwenye chauro
 
Mahitaji

Unga wa dengu 1 cup
Kitunguu maji 1/4...kata ndongo ndogo
Pilipili kijiko 1 cha chai..
Hamira 1 tea spoon.au baking powder
Pilipili mboga 1/4...kata ndogo ndogo
Chumvi kiasi
Curry powder 1tea spoon
Maji 1/2 kikombe
Mafuta ya kupikia

Namna ya kutaarisha
Changanya unga wa dengu na kitunguu maji
Weka pipilipili mboga,pilipili ya kuwasha,chumvi,curry powder
Mimina maji kidogo kidogo huku wachanganya mchanganyiko wako kwa mikono safi
Ukimaliza weka sehemu ya joto kwa dakika 30

Weka mafuta kwenye karai na choma badia zako hadi ziwe brown..

Chatne
Nazi 1/2
Pilipili ya kuwasha
Chumvi kiasi
Ndimu/ limao

Namna ya kutaarisha
Kuna nazi yako
Weka pilipili,chumvi na maji kidogo saga kwa blender hadi iwe laini
Weka kwenye bakuli tia ndimu/limau.

Badia na chatne tayari kwa kuliwa

Wallahi da #farkhina umentoa mate! Niliko siwezi kupata dengu...natamani sana bajia! Hiyo Chatne ndo kabisaaaaaa chachandu mujarab!!
 
Yeah itanoga shosti unaujua mvuje? Mama angu anaupenda sana akipika badia lazima aweke hata mie napenda hususan kwenye chauro

Naujua mpnz. Na skuizi wameturahisishia kutuekea kwenye vichupa already prepared kwa ajili ya maakulat
 
Yeah itanoga shosti unaujua mvuje? Mama angu anaupenda sana akipika badia lazima aweke hata mie napenda hususan kwenye chauro

Basi ntatengeneza chatne ya hivyo, manake katika vitu ambavyo sivipendi ni kuboronga mapishi, yani chakula kikitoka vibaya nitanyweaaaa, nitanunaaaaa.....lol.
 
Wapi huko kusikokua na dengu habibty?

Ahh...nkitaja vinavyopatikana huku hamtakula hata hizo bajia zenu...ni majanga tu huku! Huku ni wali na tambi full stop!hivyo ndo vna nafuu vingine mtatapika bajia zenu bure nkitaja. Dengu hakuna nlishatafta saana tu
 
Wapenda misosi ehhh haya tumeambiwa tuende jogging baada ya kujishindilia bajia na chatne tupunguze calories lol

Hahaaaa nendeni nyie, mimi mtanikuta hapa hapa mezani na bajia zangu.kimbaumbau mie sina diet wala jogging
 
Ntakuja nidowee hizo bajia nataka na juisi ya pasheni 🙂

Hahahaaa naskia umebeba na pilipili mkobani,kwa pilipili weye hujambo!recipe zako zote hapa lazima pilipili ndani😀😀😀😀😀😀😀😀 by the way na mimi ni mgonjwa wa pilipili, chakula bila pilipili nakiona doro
 
Ahh...nkitaja vinavyopatikana huku hamtakula hata hizo bajia zenu...ni majanga tu huku! Huku ni wali na tambi full stop!hivyo ndo vna nafuu vingine mtatapika bajia zenu bure nkitaja. Dengu hakuna nlishatafta saana tu

Hahahhaah unakula vijoka huko vijongoo lol
 
Hahahaaa naskia umebeba na pilipili mkobani,kwa pilipili weye hujambo!recipe zako zote hapa lazima pilipili ndani😀😀😀😀😀😀😀😀 by the way na mimi ni mgonjwa wa pilipili, chakula bila pilipili nakiona doro

Mie bila ya pilipili hata tonge 2 simalizi ila kwa pilipili nakula sana hususan urojo
 
Mie bila ya pilipili hata tonge 2 simalizi ila kwa pilipili nakula sana hususan urojo

Lol..urojoooo...nakukumbusha ahadi yako ya kunikusanyia recipe za urojo! Urojo mwenzie pilipili tena upate na ile mishkaki duuuh....nomaaa
 
Back
Top Bottom