- Thread starter
- #41
Km giligilani ndo unakusudia kotmir basi itanoga ndio.
Yeah itanoga shosti unaujua mvuje? Mama angu anaupenda sana akipika badia lazima aweke hata mie napenda hususan kwenye chauro
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Km giligilani ndo unakusudia kotmir basi itanoga ndio.
Mahitaji
Unga wa dengu 1 cup
Kitunguu maji 1/4...kata ndongo ndogo
Pilipili kijiko 1 cha chai..
Hamira 1 tea spoon.au baking powder
Pilipili mboga 1/4...kata ndogo ndogo
Chumvi kiasi
Curry powder 1tea spoon
Maji 1/2 kikombe
Mafuta ya kupikia
Namna ya kutaarisha
Changanya unga wa dengu na kitunguu maji
Weka pipilipili mboga,pilipili ya kuwasha,chumvi,curry powder
Mimina maji kidogo kidogo huku wachanganya mchanganyiko wako kwa mikono safi
Ukimaliza weka sehemu ya joto kwa dakika 30
Weka mafuta kwenye karai na choma badia zako hadi ziwe brown..
Chatne
Nazi 1/2
Pilipili ya kuwasha
Chumvi kiasi
Ndimu/ limao
Namna ya kutaarisha
Kuna nazi yako
Weka pilipili,chumvi na maji kidogo saga kwa blender hadi iwe laini
Weka kwenye bakuli tia ndimu/limau.
Badia na chatne tayari kwa kuliwa
Hahaa...hamia kabisa kwa #Farkhina
Yeah itanoga shosti unaujua mvuje? Mama angu anaupenda sana akipika badia lazima aweke hata mie napenda hususan kwenye chauro
Alaa kumbe upo?mi nilidhani umefichwa?
Naujua mpnz. Na skuizi wameturahisishia kutuekea kwenye vichupa already prepared kwa ajili ya maakulat
Hahaa...nani anifiche?nipogooooooooo
Huyu mwenye kitambi afanye mazoezi tu lol
Ntakuja nidowee hizo bajia nataka na juisi ya pasheni 🙂
Yeah itanoga shosti unaujua mvuje? Mama angu anaupenda sana akipika badia lazima aweke hata mie napenda hususan kwenye chauro
Wapi huko kusikokua na dengu habibty?
Wapenda misosi ehhh haya tumeambiwa tuende jogging baada ya kujishindilia bajia na chatne tupunguze calories lol
Ntakuja nidowee hizo bajia nataka na juisi ya pasheni 🙂
Ahh...nkitaja vinavyopatikana huku hamtakula hata hizo bajia zenu...ni majanga tu huku! Huku ni wali na tambi full stop!hivyo ndo vna nafuu vingine mtatapika bajia zenu bure nkitaja. Dengu hakuna nlishatafta saana tu
Hahahaaa naskia umebeba na pilipili mkobani,kwa pilipili weye hujambo!recipe zako zote hapa lazima pilipili ndani😀😀😀😀😀😀😀😀 by the way na mimi ni mgonjwa wa pilipili, chakula bila pilipili nakiona doro
Hahahhaah unakula vijoka huko vijongoo lol
Mie bila ya pilipili hata tonge 2 simalizi ila kwa pilipili nakula sana hususan urojo