AWAMU MPYA INAHESABIKAJE, WADAU TUJADILI HILI.
Na Bashir Yakub.
+255 714 047 241
Wadau, hii ni awamu ya sita ama awamu ya tano kipindi cha pili.
Kwani awamu inahesabikaje, je kila akiingia rais mpya ni awamu mpya, ama kila baada ya miaka 10 ndio awamu mpya huja.
Nikiri mapema kuwa katika Katiba hakuna kitu kinaitwa AWAMU, bali kuna ukomo wa nafasi ya urais baada ya miaka kumi.
Nimemsikia Madam Samia leo akiita hii awamu ya sita, yumkini tusimjali sana kwani naye aweza kuwa amekosea ama amepatia. Sisi tujadili tu.
Mpaka sasa wapo wanaoamini kuwa hii ni awamu ya tano lakini kipindi cha pili, hali wengine wakiamini hii ni awamu ya sita.
Wanaoamini hii ni awamu ya tano kipindi cha pili imani yao imefungamana na kipindi cha kikatiba cha rais cha ukomo wa miaka 10.
Maana ya hawa ni kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 10 ambayo ni awamu, inaweza kuongozwa na rais zaidi ya mmoja kama ilivyotokea sasa.
Kadhalika, wale wanaoamini hii ni awamu ya sita imani yao imefungamana na kwamba kila rais anatembea na awamu yake, yaani rais mpya awamu lazima nayo iwe mpya.
Ashakum si matusi, neno awamu hutumiwa zaidi na wanaccm, mnakumbuka hata zile nyimbo za Komba. Hata hivyo si neno leo.
Sasa tujadili, hii ni awamu ya tano kipindi cha pili, ama awamu sita.