Bado haijawekwa wazi kama Serikali hii ni ya awamu ya 5 au 6?

Bado haijawekwa wazi kama Serikali hii ni ya awamu ya 5 au 6?

Nimesikiliza hotuba ya Mh.rais Leo kwa kinywa chake amesema hii serikali yake ni ya awamu ya sita. Pia nimesikiliza vyombo vya habari vya kimataifa kama vile BBC na DW vyote vinaripoti hii serikali kama serikali ya awamu ya Sita.

Wataalamu wa haya mambo wanasema kwa Tanzania awamu ya Rais hukoma mara tu Rais mpya anapoingia madarakani, hivyo dhahiri kua serikali ya Mh. Mama Samia ni serikali ya awamu ya Sita na sio ya Tano.
 
Serikali ya rais wa sita wa Tanzania ni awamu ya sita ya uongozi wa nchi.

Uongozi wa awamu ya tano uliisha siku ambayo mama Samia alipoapishwa.

Kwahiyo tunasema kuwa awamu ya tano ya uongozi wa nchi ya Tanzania ulidumu kwa miaka mitano, miezi 4 na siku 22.
 
Kimsingi Awamu ya uongozi ni dhana ambayo inatokana na wewe binafsi unaitumia vigezo gani.

Mfano wapo wanaotumia kigezo cha uchaguzi, wapo wanaotumia kigezo cha Rais mpya anapoingia madarakani.

Kigezo kinachotumika zaidi ni cha Pale mtu anaposhika madaraka hadi anapotoka bila kujali amekaa muda gani.

Mf. Biden ni Rais wa 46, kumbuka huko nyuma wapo waliouawa na ilihesabika ni awamu yake (administration). Mf, JFK ni Rais wa 35 (awamu ya 35, 35th administration), alipoua kabla ya kumaliza muda wake, Lyndon Johnson akawa Awamu ya 36.

mf 2. Zanzibar, ni Awamu ya 8. Kati ya hao, wapo ambao walipanda kwenye cheo hicho bila watangulizi ktmaliza muhula. Mf karume, then jumbe akawa awamu ya pili. Mwinyi pia ni mwaka mmoja tu alitawala.

Hivyo hii ni Awamu ya 6.
 
Mh. Samiah Suluhu ni rais wa kwanza mwanamke TZ, tiyari ni mama wa taifa yaani Mh. Mama Samiah Suluhu Hassan ktk serikali mpya ya awamu ya sita na akiwa rais wa sita ktk taifa hili.
 
Awamu inahesabika kwA kuhesabu kipindi Cha uongozi cha mtu na sio miaka
Kama tungekuwa tunahesabu miaka Basi Nyerere angekuwa ameshika awamu nne na myinyi awamu mbili na mkapa awamu mbili na kikwete awamu mbili na magu awamu Mona jumla tungekuwa na awamu 11 na hi ingekuwa awamu ya 12

Lakini awamu hi NI ya sitA kwa maana ya kipindi Cha sita. Cha uongozi was serikali ya Rais wa sita

Awamu ya magufuli imepita NI kipi di Cha uongozi wa magufuli
.mbona hili Jambo rahisi Sana kulielewa huhitaji kwenda darasan
 
Rais Samia kasema hii ni awamu yake ya sita,lakini hii haimaanishi kuwapiga kimya wenye msimamo wa hii ni awamu ya tano kama kuna fact.
Kuna wabunge pia niliwasikia wakisema ni awamu ya tano.
Mimi binafsi hii ni awamu ya sita na Rais wa sita.
 
Awamu inahesabika kwA kuhesabu kipindi Cha uongozi cha mtu na sio miaka
Kama tungekuwa tunahesabu miaka Basi Nyerere angekuwa ameshika awamu nne na myinyi awamu mbili na mkapa awamu mbili na kikwete awamu mbili na magu awamu Mona jumla tungekuwa na awamu 11 na hi ingekuwa awamu ya 12

Lakini awamu hi NI ya sitA kwa maana ya kipindi Cha sita. Cha uongozi was serikali ya Rais wa sita

Awamu ya magufuli imepita NI kipi di Cha uongozi wa magufuli
.mbona hili Jambo rahisi Sana kulielewa huhitaji kwenda darasan
Naam
Nilitaka kuandika hivi
 
Back
Top Bottom