Bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki?

Bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki?

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,609
Na Bashir Yakub.
+255784482959.

1. Tokea mahakama kutengua matokeo ya rais, serikali iliwaondolea ulinzi mara moja jaji mkuu Maraga na makamu wake Philomena Mwiru. Wawili hawa kwasasa wanalindwa kampuni binafsi za ulinzi walizo ajiri wao wenyewe.

2. Ndani ya wiki mbili ambazo NASA ya Odinga wametangaza maandamamo tayari watu zaidi 35 wameshauliwa na polisi wakiwemo watoto wadogo wawili.

3. Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka nao wameondolewa ulinzi maalum kutoka serikalini. Raila anapata haki ya ulinzi maalum kwa mujibu wa sheria kwakuwa ni Wazir mkuu mstaafu na Kalonzo ni makamu wa rais mstaafu.

4. Jimmy Wanjigi ni tajiri anayemsapoti Odinga. Leo ni siku ya tatu amefungiwa nyumban kwake na familia yake na kikosi maalum cha usalama. Mahakama imetoa amri kikosi kiondoke kwake lakini wamekaidi amri hiyo.

5. Leo Kamisha wa tume huru ya uchaguzi Dk. Roselyn Akombe amejiuzulu na kukimbilia Marekani. Anasema serikali inaisukuma tume upande ambao yeye hawezi kuwa sehemu yake.

6. Bunge la Kenya linalooongozwa na Jubilee ya Uhuru limebadili sheria ya uchaguzi ktk kipindi cha uchaguzi ndani ya wiki moja ili itumike ktk uchaguzi huo huo kitu ambacho si tu ni kosa Kenya bali hata kwenye Sheria za Kimataifa .

7. Maandamano ya NASA ya Odinga yamepigwa marufuku kwenye miji mikubwa yote. Mahakama imetoa zuio kutaka maandamano kuendelea lakini serikali imekaidi zuio hilo.

8. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafura Chebukati mda mfupi uliopita amesema hataacha kujiuzulu kabla ya uchaguzi ndani ya siku 6 zilizobaki kulinda heshima yake na familia ikiwa Tume itaendelea kuingiliwa na mamlaka kama ilivyo sasa.

9. Haya yametokea ndani ya wiki tatu na ni mbali na yale ya kabla na baada ya tarehe 8 wakati matokeo ya kwanza yalipotolewa ambapo :
Taasisi mbili za haki za binadamu zilifungiwa.

Vifo ya watu 26 Kisumu.

Kumtishia jaji mkuu kuwa atakomeshwa baada ya uchaguzi, nk. nk.

Je bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki ???.
 
Mi si mtu wa dini ila kwa hayo uliyoandika hapo nadhani kale kapepo ka marais wa afrika kameanza kumuandama jamaa polepole. Ila angalau yeye anakosolewa, na hata ukimwita kilaza hulipishwi milioni tano, atakuangalia atacheka kidogo then ataenda kupoozea na bangi pembeni.
 
Kama kipimo ni huyu wetu Uhuru si tu baba wa demokrasia ila babu wa demokrasia kwa ukanda wetu...Odinga anastahili mastaka kwa kuwatongoza wakenya, kuwashika shika hisia zao kisha kuwaacha hewani!
 
Hiyo inaitwa "try me to do you"! Sentensi ya kijinga inayomaanisha" niguse nikubusu "!
 
Nenda Kaishi Kenya halafu ujambe jambe mitandaoni kama hujarudi hapa matako kama ya Nyani
Sio kosa lako...nafikiri ni zao la shule zetu za kata...na lishe duni iliyofubaisha ukuaji wa akili yako!
 
Kama kipimo ni huyu wetu Uhuru si tu baba wa demokrasia ila babu wa demokrasia kwa ukanda wetu...Odinga anastahili mastaka kwa kuwatongoza wakenya, kuwashika shika hisia zao kisha kuwaacha hewani!


hahahahahaha !!!!!!!!!!!!!!!! kuwatongoza wakenya
 
Hii hutokea Africa tu.

Sijui madaraka yana ushetani ndani yake maana kila mtu mwenyewe madaraka huwa mgumu sana kuyaachia yupo tayari hata kuua ili mradi abaki katika nafasi aliyonayo.

Kenya imeshajiunga na nchi nyingine za Africa mashariki ambazo demokrasia yao ipo kwenye maandishi na maneno tu ila utendaji ni bashite.
 
Hakuna Baba wa Demokrasia wala nini
Kenya kuna Ombwe la mauaji ya Wanasiasa wanao kinzana na Msimamo wa Uhuru
lakini kwa kuwa Watanzania tuna Tabia ya Kufuata mkumbo na ushabiki wa kijinga kizuri cha jirani tu
hili ningumu kuliweka wazi.



una akili kama mchwaaaaaaaaaaaaa
 
Wasiojulika ni mfano wako wewe
nani anaye kufahamu humu Jf!?
Hivi Akili mnazo kufanyia nini!!
Tunazo kukuelimisheni ninyi vuvuzela msiojitambua bado ambao bado mnamshangilia aliyewashikilia mateka kwa kuwa tu 'ana roho nzuri' na kwamba hajawaua!
 
Back
Top Bottom