Na Bashir Yakub.
+255784482959.
1. Tokea mahakama kutengua matokeo ya rais, serikali iliwaondolea ulinzi mara moja jaji mkuu Maraga na makamu wake Philomena Mwiru. Wawili hawa kwasasa wanalindwa kampuni binafsi za ulinzi walizo ajiri wao wenyewe.
2. Ndani ya wiki mbili ambazo NASA ya Odinga wametangaza maandamamo tayari watu zaidi 35 wameshauliwa na polisi wakiwemo watoto wadogo wawili.
3. Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka nao wameondolewa ulinzi maalum kutoka serikalini. Raila anapata haki ya ulinzi maalum kwa mujibu wa sheria kwakuwa ni Wazir mkuu mstaafu na Kalonzo ni makamu wa rais mstaafu.
4. Jimmy Wanjigi ni tajiri anayemsapoti Odinga. Leo ni siku ya tatu amefungiwa nyumban kwake na familia yake na kikosi maalum cha usalama. Mahakama imetoa amri kikosi kiondoke kwake lakini wamekaidi amri hiyo.
5. Leo Kamisha wa tume huru ya uchaguzi Dk. Roselyn Akombe amejiuzulu na kukimbilia Marekani. Anasema serikali inaisukuma tume upande ambao yeye hawezi kuwa sehemu yake.
6. Bunge la Kenya linalooongozwa na Jubilee ya Uhuru limebadili sheria ya uchaguzi ktk kipindi cha uchaguzi ndani ya wiki moja ili itumike ktk uchaguzi huo huo kitu ambacho si tu ni kosa Kenya bali hata kwenye Sheria za Kimataifa .
7. Maandamano ya NASA ya Odinga yamepigwa marufuku kwenye miji mikubwa yote. Mahakama imetoa zuio kutaka maandamano kuendelea lakini serikali imekaidi zuio hilo.
8. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafura Chebukati mda mfupi uliopita amesema hataacha kujiuzulu kabla ya uchaguzi ndani ya siku 6 zilizobaki kulinda heshima yake na familia ikiwa Tume itaendelea kuingiliwa na mamlaka kama ilivyo sasa.
9. Haya yametokea ndani ya wiki tatu na ni mbali na yale ya kabla na baada ya tarehe 8 wakati matokeo ya kwanza yalipotolewa ambapo :
Taasisi mbili za haki za binadamu zilifungiwa.
Vifo ya watu 26 Kisumu.
Kumtishia jaji mkuu kuwa atakomeshwa baada ya uchaguzi, nk. nk.
Je bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki ???.