Bado kuna mambo yanahitajika ili kumuenzi kwa dhati hayati Magufuli na wazalendo wengine

Bado kuna mambo yanahitajika ili kumuenzi kwa dhati hayati Magufuli na wazalendo wengine

Mzalendo wa sasa hivi🐒🐒🐒
 
Mkapa kafanya lipi la maana? Kujiuzia migodi ya dhahabu na kubinafsisha kila kitu?
Akili ya dudumizi haiwezi ikajua mambo ya uchumi. Yawezekana wewe umezaliwa after 1995 ndiyo maana hujui Benjamin William Mkapa alifanya nini kwa nchi hii
 
Habari zenu wana JF wenzangu

Kwanza kabla ya yote ningependa niwe mkweli kwamba katika nchi yetu Tanzania toka tupate uhuru hadi leo, moyo wangu unaamini au kumchukulia hayati Magufuli kama mzalendo namba mbili baada ya hayati mwl Nyerere.

Ninapozungumzia wazalendo namaanisha mtu au wale watu ambao wana mapenzi ya dhati kwa nchi zao, yani upendo uliopitiliza kiasi kwamba wapo tayari kupoteza chochote including their life kwa ajili ya nchi yao.
Nchi yetu toka tupate uhuru tumefanikiwa au kubarikiwa kuwa na wazalendo wachache sana (ukiachana na wale wazalendo wa kujitengeneza au kutengenezwa na kundi la wapambe wake). Mzalendo wa kweli hupatikana by nature.

Yani mtu anazaliwa akiwa tayari amepewa moyo wa kizalendo, anasoma akiwa na moyo wa kizalendo, anapata uongozi wa nchi, wizara, chama au kitengo fulani akiwa na moyo wa kizalendo, anapambana na changamoto mbalimbali zikiwemo zile zinazo cost maisha yake akiwa na moyo wa kizalendo na matokeo yake anastaafu au hata kufa akiwa na moyo ule ule wa kizalendo.

Hapo chini ni list ya sita bora ya wazalendo wa kweli niliowakubali nchini kwetu.
1. Mwl Julius K. Nyerere
2. Dr John P. Magufuli
3. Hayati Sokoine
4. Bibi Titi Mohammed - japo huyu hakudumu serikalini muda mrefu, lkn juhudi zake za mapambano kwa nchi yake dhidi ya mkoloni na maadui wengine wa taifa zinampa uhalali wa kuwa miongoni mwa wazalendo wa kweli.
5. Kambona.
6. Kawawa.

Na siku zote mzalendo wa kweli huonekana kwa matendo yake, maneno yake na uongozi wake.

Mwl Nyerere kwa vile alikuwa mzalendo wa bara lake na nchi yake, aliwahi kukumbana na vikwazo mbali mbali vya ndani na nje ya nchi yake, ikiwemo wabaya wake wa ndani na nje kupanga mapinduzi mara mbili dhidi ya utawala wake. Lakini kwa vile alikuwa mzalendo wa kweli, hakuogopa mapinduzi hayo, bado alisimama imara kwa ajili ya taifa lake na wananchi wake, na kamwe hakuwahi kubadili misimamo yake hadi siku ya kufa kwake.

Ndio maana leo hii popote pale iwe ndani ya nchi au nje ya nchi tunapozungumzia wazalendo wa kweli wa bara letu na nchi zetu basi mwl Nyerere huwa hakosi katika list za mwanzo.


Nije sasa katika mada.. binafsi namuona hayati Magufuli kuwa mzalendo namba mbili kutokana.. maneno yake, matendo yake na uongozi wake katika nchi yetu.

1. Magufuli alipambana kwa ajili ya nchi yake, bila kujali athari ya kupoteza uhai wake.
2.Magufuli aliweka bond maisha yake, ili kuleta maendeleo ya kweli katika taifa lake.
3. Magufuli alisimama kidete kutetea uhai, na uhuru kamili wa nchi yake.
4. Kwa muda mfupi wa uongozi wake tumeweza kuona hatua kubwa ya maendeleo imepigwa kupitia uongozi wake.

Kama mimi ningekuwa raisi wa Tanzania, basi ningefanya mambo haya matano ili kuuenzi mchango wake mkubwa na wa dhati kabisa wa taifa letu.

1. Tarehe 17/03 ya kila mwaka ingeitwa "Magufuli day". Hata kama siku hii isingekuwa ya mapumziko, kutokana na nchi yetu kuwa na sikukuu nyingi za kitaifa na kimataifa. Mimi ningeifanya siku hii ya "half day". Yani watu wanafanyakazi hadi saa sita ofisi zote za serikali zinafungwa, huku radio na television za taifa zikionesha hotuba, historia ya maisha yake na uongozi wake kwa ujumla.

2. Ikulu ya chamwino Dodoma ingeitwa "Magufuli State House" ili kuuenzi mchango wake mkubwa uliosababisha ikulu hiyo ikajengwa chini ya uongozi wake, baada ya viongozi wa awamu ya kwanza hadi ya tano kushindwa kuijenga.

3. Ningeshauri au kupendekeza hayati Magufuli aitwe mjomba wa taifa 😀😀😀 baada ya mzalendo namba moja mwl Nyerere kuitwa baba wa taifa.

4. Ningejifunza baadhi ya mambo kutoka kwake kama vile kusimamia miradi ya kimaendeleo, kupiga vita ufisadi, kupinga rushwa kwa watoaji na wapokeaji, kufukuza wazembe, wavivu na watoro makazini.

5. Mama Janet Magufuli ningempa ubunge wa viti maalum afu ningemteua kuwa naibu waziri wa elimu, (i hope) kwa elimu na uzoefu alio nao ange fit katika nafasi hiyo.

6. Kutokana na mabadiliko makubwa ya kimiundombinu aliyoyafanya katika barabara ya Migogoro road, basi ningeibabilisha jina na kuitwa "Magufuli road" badala ya hili jina la sasa la Morogoro road.

Haya ni baadhi ya mengi ambayo ningeyafanya ili kumuenzi kiuhakika mzalendo wetu namba mbili.
Je wewe ungefanya yapi zaidi ya hayo?

RIP to wazalendo wote, pamoja na watanzania wengine waliotangulia mbele ya haki.

Eid Mubarak to all Muslims na watanzania kwa ujumla.
wewe juha hakuna anayetaka kumkumbuka yule shetani wako, eti alijitoa kwa ajili ya nchi, yule alikuwa tapeli, mbaguzi, katili, muuaji, mtesaji wa watanzania, mshamba. Hatutaki kumkumbuka kwa lolote mkumbuke we na mke wako. Hakuna jambo la maana alilokamilisha. Akija rais jasiri hata miradi yote yaliyoitwa kwa jina lake, atafuta majina yake hana tofauti na Mobutu Sese Seko wa Zaire.
 
Naunga mkono hoja. Ukimtaja Magufuli mwili mzima huwa unasisimka. Nilimpenda sana tena sana huyu mtu.
Alijitoa sadaka bila kujibakiza. Alijua kabisa kwamba, kwa anayoyafanya na kuyasimamia kwa vyovyote vile hawezi kudumu lakini hakuogopa, alisonga mbele.

Mimi huwa namwita"MTAKATIFU JOHN MAGUFULI".
we zuzu kweli, labda km alijitoa kwa ajili ya mamako
 
Kwa kweli tunahitaji kumuenzi vizuri zaidi ya sasa. Huyu Mzee alikuwa ni Rais hasa. Sasa ndio tunajionea mazuri yake.
 
Basi hii kesi tuipeleke kwa wakili msomi TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU ili tuone namna ambavyo angependa dikteta wako aenziwe.
Lisu ashasema kwamba raisi Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli ndio maana hakuwahi kusaini mikataba mibovu.
 
Back
Top Bottom