Bado nampenda Sumaiya ingawa nimeshaoa - True Story

Bado nampenda Sumaiya ingawa nimeshaoa - True Story

SEHEMU YA SABA
#ILIYOPITA
Mimi:Ndo hivyo dada
Dada:Njoo ndani tukaongee
Nikawa nawaza mbona dada anataka tukaongelee ndani,
#ENDELEA

Baada ya kuingia ndani nikiwa nina hofu na kiu juu, ya kutaka Kujua nini anataka kuniambia dada
Dada:Kwahiyo nini kimetokea
Mimi:Ikabidi nianze tena kumwelezea nilivyokabwa usiku ,nikamuelezea tena upya
Dada : Unajua hili tulishaga limaliza,sasa kwanini tena limejirudia

Nikawa sielewe Dada ananiuliza Mimi au nini,kitu gani hicho wamekimaliza
Mimi: mlishamaliza nini?
Dada akanambia kwa sauti ya chini
Dada: anae yafanya haya hatoki mbali
Mimi: kwahiyo unamjua au?
Dada:Sisi zamani tulikuwa tunafinywa usiku

Mimi nikawa simuelewi dada,namuuliza kama mtu huyo mtu anamfahamu ila akawa anajibu vitu hata sielewi ikabidi nimwambie tu Mimi narudi chuo Siwezi tena kulala hapa leo,dada akanambia nisijari Kuna jamaa alikuwa anaitwa muga atanipa kampani atakuja kulala,sikuwa na nguvu ya kukataa maana plani yangu ilikuwa nimalizane kwanza na sumaiya,maana nilikuwa nakiu ya kuwa mtu wa kwanza kwake kuvunja nyongo yake aloitunza mpaka kufika form 2

Sumaiya sikuhiyo akawa amekuja,akawa kapika chakula,ilikuwa wali na maharage,nikamtumia sms kuwa ukipakua chakula Cha kwetu weka sahani Moja,akawa kanambia tutakulaje sehemu Moja akati watu wengi pale,nikamwambia wewe weka tu najua Kila mtu akila pale huwa anaingia chumbani kuchezea simu,Yani dada,mama mdogo na yule Jojo walikuwa nauraibu mkubwa sana wa simu,

Basi kweli walivyokula tu,wakaingia vyumbani,Mimi sikutaka kulia pale sebuleni,nikamwambia tukalie nie kabisa kulikuwa Kuna meza huwa ipogo tu nje muda wote,sikuhiyo nilikula na sumaiya,tulitumia nusu saa kula chakula Cha kula dakika 5,nilijisikia raha sana,nilijiapiza huyu mtoto lazima awe aje kuwa mke.

Basi siku zilienda nikawa nasubiri pale home labda kina Jojo na mamdogo wataondoka ila wapi,nikawa muda wote nashinda sebuleni nikienda pale kwa dada,mpaka naanza kufanya mtihani wa chuo na kumaliza nilikuwa Bado sijafanya chochote kwa sumaiya,muda wa field ukafika nilikuwa nimepangiwa morogoro Field,basi nilimuaga na kuhuzunika sana,nilimsihi sana asije kunisaliti kwani ninampemda sana,kweli alikuwa na bikra na nilimuomba sana anitunzie kwa miezi mitatu mpaka nitakaporudi,nayeye kwa mara ya pili niliona akitoa machozi na kuahidi mimi ni wake tu na bikra ni yangu,moyo ulikuwa unauma sana ila ndo hivyo sasa field.

Mwezi wa saba katikati nikawa nimewasili morogoro,nilipanda BM coach mpaka msavu,msamvu nikachukua daladala za Manyuki, nikashukia pale transformer karibu na st Denis,njia ya kwenda lukobe,basi moro ndo ikawa sehemu yangu ya field kwa miezi mitatu,sasa nilivyokuwa Moro nikawa muda mwingi namuhisi vibaya labda sumaiya nimemuacha dar ananisaliti,akichelewa tu kujibu sms basi namlaumu sana,ikafika kipindi nikawa namwambia maneno ya kejeli kuwa bikra aitoe wapi,

Akawa ananipigia analia,sasa namimi muda huo pale Moro nilikuwa Nina kisichana changu Cha muda mrefu tulikuwa tunapozana nako,nikawa siwazi sana kuhusu sumaiya

Kuna siku nikampiga sumaiya namba yake akapokea mwanaume,hapo nilidata, nikamwambia mpe simu mwenye hii namba
Jamaa:Sawa
Mimi: Hallo
Sumaiya:unataka nini kwangu
Mimi:Sumaiya Yani Mimi nimekupima tu kidogo umeenda kutolewa bikra na huyo mpuuzi,hapo machozi yakaanza kunilenga,nikakumbuka nilivyooanza na sumaiya mpaka sasa,nikawa nawaza tu jamaa lililopokea simu limeshaniwahi
Sumaiya:Mtu nayempenda usimuite mpuuzi
Mimi: Mungu wangu ushampenda mtu mwingine teyari,sumaiya nimekukosea nini?
Sumaiya: Mabiki umenitukana sana,kuwa Mimi Malaya,bikra naitolea wapi,umenikebehi nikakuvumilia kwaajili yako,ila sasa nimepata tulizo la moyo wangu

Moyo wangu ulishituka sana kusikia hivyo,ikabidi nimuulize jamaa yako anaitwa nani,akajibu anaitwa samali,

Je samali atakuwa kashafanya kweli kwa mtoto sumaiya tukutane sehemu ya nane
Muendelezo lini mkuu!?
 
Onh... atarudi lini Huyu kiumbe kumalizia story yake.
 
Back
Top Bottom