Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Suala siyo DARAJA,

je, KIPAUMBELE KWA ENEO LA KANDA YA ZIWA NI DARAJA?
Kuna miradi mingine si rahisi kuona faida yake kwa wakati uliopo lakini kwa miaka ya mbeleni, ni rahisi kuona faida. Mfano, leo tunahangaika kujenga kiwanda cha kusindika nyama lakini tayri kulikuwa na aian hiyo ya viwanda kwa Dar es Salaam na Arusha. Lakin pengine muda muafaka ulikuwa haujafika niyo maana vilikufa mapema. Vile vile, kiwanda cha Magudumu ya magari pale Arusha, wakati kinajengwa ni Watanzanai wachache sana waliokuwa wanamiliki magari, leo magari yameongezeka lakini hatuzalishi magurudumu nchini, yote yanaagizwa. Kwa hiyo, daraja hilo litakuwa na faida tu, tusibeze juhudi za serikali.
 
Ningekuwa mimi hizo Bil 700 zingetosha kabisa kujenga vyuo vya kilimo na mashamba darasa ya walau hekari 10,000 kila wilaya (Halmashauri). Kila kijana aliyemaliza shule ya msingi ambaye hakuchaguliwa kuendeea na masomo ya juu angekuwa part of the project kwa kupewa robo hekari.. Kwa hiyo kila Halmashauri tungekuwa na vijana 40,000 kwenye hii project with average ya vijana 4 kwa hekari moja. Vijana wangepewa hela ya kujikimu kupitia mkopo wa mabenki ya kilimo wakati wanasubiri kuuza mazao yao.

Serikali ingehakikisha inawapatia wataaam wa kilimo, pembejeo na pia kutafuata masoko ya uhakika ya mazao haya pamoja na kujenga processing firms ndani ya maeneo ya uzalishaji. Kwa mpango huu nisingemwona kijana hata mmoja akizunguka hapa mjini akiuza soksi, vikombe na dawa ya nguvu za kiume.

Watanzania hasa vijana amkeni, wakati ni huu!!
 
Sera nyingi huwa hazina faida kwa watu wengi,
Mfano mfuko wa Tasaf,unaogawa pesa kwa kaya maskini,unawapa watu pesa ya kula tu,
Hizo pesa bora uwape vijana wajasiriamali,wanaotafuta mitaji ya kufungua kampuni,au uzalishaji mali,ambao wanaweza kutoa mchango mkubwa kwa kutengeneza ajira nyingi .
 
Umekosa ajira mpaka unalilia fedha za tasaf komaa kijana tafuta zako tasaf ni za vikongwe na wasiojiweza we zako ulilipwa kwa mtindo wa boom ukanunua sabufa ha ha ha saiv ndio umepata akili kuwa ukipata za tasaf utazalisha
 
Kigogo Busisi kuna kero kubwa sana ya usafiri hasa pale unapokuta pantoni zipo chache kitu ambacho ni cha kawaida
Kwa kujenga daraja la busisi unarahisisha usafiri kwa nchi za EA kama vile Burundi, Rwanda, Uganda hata Congo.
 
MAWAZO YAKO NI NADHARIA TU KAMA VILE WASIOKUNYWA POMBE WANAVYOWAPIGIA WANYWAJI HESABU ZA CHUPA ZA BIA WANAZOKUNYWA KILA SIKU, WIKI, MWEZI NA MWAKA NA KUHITIMISHA KWA KUSEMA WANGEFANYA MENGI, WAKATI WAO HAWANYWI NA HAWAJAFANYA LOLOTE. KWANI KABLA YA UJENZI WA HILO DARAJA HIZO HELA ZILIKUWA ZINATUMIKA WAPI?
 
Alikuwa mtu wa hovyo sana! Kingunge alikuwa anamwita nyapara wa barabara
 
Hiii ndio Tanzania bwana alie shiba hamjui mwenye njaaa ee mungu muongoze Rais wetu akue na busara mingi
 
Watu km nyie ndio mnatakiwa muwe JF wengine wamekaaa magetoni halfu wanachangia
 
Huyu mtu alikua najsi kabisa alaaniwe huko.alipo.
 
Tanzania ukiwa kiongozi na ukataka kumfurahisha kila mtu, nchi haiendi; wapingaji kama wewe wapo tu, na wengine hupinga kwa sababu lilijengwa wakati wa Magufuli, lingejengwa wakati wa Kikwete au Samia huenda wasigentoa lawama hizo.

Inaonekana unaangalia daraja like kwa lenzi ndogo inayoona kuunganishwa kwa Busisi na Kigongo tu. Hujui kuwa linahudumia pia mikoa ya Kagera, Geita, na nchi jirani za Uganda na Rwanda. Kuna siku hapa mama Tibaijuka alilalamika mkoa wa Kagera kuwa wa mwisho kimaendeleo na sababu yake ni hiyo ya usafiri baina ya mkoa wa Kagera na Mwanza kuwa magumu sana. Meli zimepunguza tatizo hilo kidogo lakini huwezi kulinganisha na huduma ya barabara. Matumizi ya feri hayawezi kutatua changamoto za usafiri eneo hilo, mpaka sasa hivi kuna feri pale Bisisi-Kigongo, na Kamanga lakini hazitoshelezi; kwanza zinafanya kazi mchana tu. Ukifika hapo saa 12 jioni, itabidi ulale hapo hadi kesho yake.

Daraja lina urefu wa zaidi km 3 likiwa ni refu kuliko yote Tanzania, kwa hiyo gharama ya $300m ni wastani wa $100m/km ambayo ni chini ya gharama iliyotumika Tanzanite Bridge ($121/0.63) kwa kila km.
 
Ach
A siasa uchwara
 
Kwa hiyo hela ungeweza kununua feri zaidi ya mbili kama zile za kivukoni na kujenga hospitali kubwa kama Muhimbili kule kule Kigongo. Yani haiingii akilini hata kidogo.
Shida hapo siyo wagonjwa tu,fery haziaminiki na muda unaotumika ni mwingi mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…