Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Hatuna nia mbaya ya kuwasema Watanzania wengine ila kiukweli daraja la Kigongo - Busisi hakuna kiongozi ndani ya nchi hii mwingine yeyote yule ambaye angechaguliwa akubaliane na ujenzi huu. Hili daraja limejengwa ili tu fulani na watu wake waulazimishe uwanja wa Chato uwe mbadala wa uwanja wa ndege wa mwanza! Ni hilo tu!

Zinatumika fedha nyingi za walipakodi pasipo mipangilio mizuri. Hizi kodi tunalipa watanzania wote hivyo ni lazima zitumike vizuri na siyo haya tunayoyaona sasa!

Hata kama wanachato watakasirika kwa sisi kuusema ukweli basi na wakasirike ila kiukweli mambo haya hayakubaliki!

Gharama za ujenzi wa hili daraja ni kubwa mno. Ni mradi wa hasara na unafanyika ili tu matakwa fulani yatimie. Haiwezekani miradi miwili tu ya uwanja wa Chato na daraja la kuufikia uwanja huo kwa urahisi vigharimu Tshs zaidi ya trilioni moja! Hapana!

Screenshot_20200918-081635_Maps.jpg
 
Ulitaka lijengwe wap? Yaan watu waendelee kuvuka Kwa mitumbwi, mbna watu mna ukabila sana aisee, wewe ukipata kazi nzur kwenu utapasahau? Mbna wachaga walipata Elimu wa Kwanza wakapata nyazifa serikalini wakajenga kwao, barabara, maji umeme na wakajiwekea Kilimanjaro international Airport, Leo daraja kujengwa mwanza imekuwa nongwa, watu mna roho mbaya Sana!

Hata mfalme Daud alipopata ufalme alihamishia makao makuu Yerusalemu mji wa kwao wa kabila la Yuda, na kamanda mkuu wa majeshi akawa mtoto wa dada akee.

Biblia inasema mtu anayewasahau wa kwao ni mtu mbaya kuliko asiyeamin. Watanzania tupunguze wivu na chuki.
Kwahiyo kwasababu kiongozi fulani kwakuwa ana mamlaka ya kutumia kodi za Watanzania basi azitumie atakavyo hata kama watu watapigika? Hapana!
 
Huyu jamaa ana wivu kweli. Miaka ijayo Mwanza itakua ni moja ya makini makubwa na Population ya watu inaongezeka KILA leo,
Mwanza NI kitovu cha Biashara Kwa mikoa zaidi ya nane!!

Mikoa hiyo INA jumla ya wakazi Milion 15.
 
Kwahiyo kwasababu kiongozi fulani kwakuwa ana mamlaka ya kutumia kodi za watanzania basi azitumie atakavyo hata kama watu watapigika? Hapana!
Daraja lile ni muhimu sana
 
Huu upumbavu wa kujenga miradi ya matrilioni isiyo na faida ni wa kupingwa na kila mtanzania anayejitambua!
 
Kwan hzo kodi zinatumika Uganda? Chato na mwanza sio watanzania , unataka watanzania wa wap?
Kwahiyo kwakuwa ni Tanzania basi tutumie tu hovyo hovyo?
 
Ultimately dictator is no friend to anybody except himself!

A good dictator is only the dead one!
 
Ni heri angelipa madeni ya ndani ili ku stimulate uchumi na kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Daraja hio sio priority kwa kweli.
 
Hilo daraja litakuwepo kea miaka 600, kila siku likiingiza 10m kwa miaka 600 si ni faida? Hizi ferry zinaendeshwa kea hasara safari mmoja unatumia mafuta ya 5m wakati nauli ni mianne kea kichwa huoni hiyo hasara?
Unajua watu wengine hawajui faida yake na jinsi litakavojilipa.ikiwa siku mmoja litaingiza sh million 10 kwa siku,kwa mwaka ni siku 365 mara 10,000,000=3,650,000,000 ni biliion 3.65

Basi kwa mapato ya daraja hili miaka 50 litaweza kujenga madaraja nchi nzima bila kutegemea serikali.
 
Sasa ngoja hilo daraja likamilike uone watakaopita hapo kama watakuwa wengi kuzidi feri. Hivi unajua kurudisha bilioni 700 wewe! Hizo hela ni nyingi sana kwa kuelekeza kwenye mradi kama ule. Anyway ila Jiulize kwanini hata yeye Magufuli anahisi alifanya kitu kisicho na tija hadi anahimiza waharakishe ili Rais mwingine asije akaufuta huo mradi.
Wajinga ni wengi! Unataka daraja lirudishe pesa hizo kwa nani? Hiyo ni biashara?
 
Back
Top Bottom