Uchaguzi 2020 Bado sioni njia ya CCM kushinda huu uchaguzi. Kivyovyote vile, CCM imepoteza mpambano

Uchaguzi 2020 Bado sioni njia ya CCM kushinda huu uchaguzi. Kivyovyote vile, CCM imepoteza mpambano

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Nimetafakari sana huu mchezo unavokwenda, na nimejiridhisha bila shaka, mpaka sasa, CCM imepoteza pambano.

Mtakubaliana na mimi ya kwamba CCM wameshindwa kwenye hoja za kampeni, CCM wameshindwa kutetea chochote walichokifanya miaka mitano iliyopita, ilani yao ya uchaguzi mwaka huu wanaiona kama 'kituo cha polisi', CCM hawajafanya kampeni zozote za maana huu mwaka.

Ni kwa viashiria kama hivo ambavyo vinaniambia kwamba CCM haitoboi huu mwaka.

Mbinu pekee ni wizi wa kura na hujuma, ambavyo naviona pia vikienda kuangukia pua kwasababu CCM ya sasa ina maadui wengi sana wa ndani. Kuna wana CCM wengi sana wameumizwa na huu mfumo kandamizi na wote hao japo kwa sasa hawasemi wazi, wataenda kupiga kura ya haki.

Nimefurahi pia mbinyo wa jumuiya ya kimataifa kwa utawala wa Magufuli, hii inakuambia kwamba, ikiwa Magufuli atajaribu kutumia ubabe, ni wazi shahiri lazima kuwe na consequences.

Zamani CCM walifanikiwa kuibia watanzania kura, lakini tuliwasamehe kwasababu kidogo walikuwa ni waungwana. Ila kwa sasa, hakutakuwa na msamaha wa wezi.

CCM MUST FALL!
 
Inasemekana leo ilikuwa Jumamosi ya mwisho chini ya utawala wa CCM. Ni siku muhimu sana kwa historia ya taifa letu.

Vyovyote itakavyokuwa, 28/10/2020 itakuwa siku itakayoibadilisha Tanzania forever!
 
Unaposema CCM itashindwa uwe na facts ! Kwa vigezo vipi ishindwe ?ccm ina wanachama wapiga kura takriban 15 M ! Wanashindwa vipi?! Mnapeana matumaini bure tu humu!

Kila kona ya nchi hii kuanzia kwenye mashina huko ccm wapo tele! Wanashindwaje uchaguzi!. Chama cha kukitoa ccm madarakani bado hakipo! TUSIDANGANYANE!
 
Kwa njia halali mkuu. Ingetaka njia haramu wangetumia Covid19 kama kisingizio cha kuhairisha uchaguzi na kuchakachua njia zote za uchaguzi
Kwa njia halali CCM hii haiwezi toboa labda wajaribu njia mbadala ambazo ni haramu!
 
Ccm imezoea kushinda kwa hila. Na mwaka huu inaonekana Kuna kundi within the system limejipanga kweli kushinda na kupangua izo hila zote.
Kwa kura za kawaida, hakuna namna Ccm watashinda mwaka huu, kwa hila watu wanejipanga kuliko kawaida.

Kwaheri Ccm, kwaheri ya kuonana

Karibu Ikulu Tundu Antiphas Lissu, karibu Raisi mpya wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
 
Sasa kama tume ni ya ccm wapinzani si mgomee chaguzi zote. Hamueleweki mara nyerere aliwavusha vizuri,mara mkapa jiniasi etc ila mnahesabu miaka yote 60 daah
Kwa kubebwa na tumeccm na polisiccm lakini uchaguzi HURU na wa HAKI maccm hayana chao? Kwa lipi walilolifanya? Miaka 60 ya uhuru Nchi haina chochote cha kujivunia. Wafanyakazi, Wakulima na Wafanyabiashara wote ni vilio tu.
 
Back
Top Bottom