Bado Trilioni 3 Tu TRA (Tzn) Kuipita KRA (Ken) Makusanyo ya Kodi. Kishindo Cha Tanzania ya Samia Kitapeleka vilio Kwenye Uchaguzi wao 2027

Bado Trilioni 3 Tu TRA (Tzn) Kuipita KRA (Ken) Makusanyo ya Kodi. Kishindo Cha Tanzania ya Samia Kitapeleka vilio Kwenye Uchaguzi wao 2027

Tanzania Kupitia TRA inaenda Kuwapita Wakenya kwenye Makusanyo ya Kodi mwaka 2027 kwani Bado Shilingi Trilioni 3 Kuwafikia.

Hapo kabla Kenya ilikuwa imewekwa Gap la zaidi ya Trilioni 7 lakini juhudi za Serikali ya Samia kuhamasisha uwekezaji na ulipaji Kodi wa hiari zimeanza kuzaa matunda Kwa kupunguza gap kubwa lililokuwepo.

Kwa mujibu wa data rasmi kutoka taasisi hizo za Kodi ulinganishi niliodanya unaonesha kwamba Kwa kipindi Cha miezi 6 ya mwaka wa Fedha 2024/25,TRA imekusanya Shilingi Trilioni 16.5 huku KRA ya Kenya ikikushanya Kshs.1.07 (Tshs.20.T) sawa na tofauti ya Shilingi Trilioni 3.5 tuu.

View: https://x.com/BD_Africa/status/1881778910087557223?t=q-ekZhQFkuEuGSbCwr0NGg&s=19
View attachment 3212166

Kwa mikakati na uwekezaji Unaoendelea Nchini wa kufungua Nchi na hakika mwaka 2027 TRA itawapita Kenya na Kupeleka Kilimo kikubwa zaidi Kwa Kasongo yeye akiwa kwenye uchaguzi.

Mfano miradi ifuatayo ikianza kitema tuu basi wamekwisha.

1.Bomba la Mafuta la EACOP 2026,hapo Kuna zaidi ya Trilioni 1.

2.Ubungo Logistics Centre ,2025

3.Kukamilika Kwa mradi wa Mapipa ya Mafuta Bandari ya Dar 2026.

4.Kukamilika Kwa upanuzi wa Bandari za Dar,Mtwara ,Tanga Kilwa, Zanzibar na zile za Maziwa makuu 2027.

5.Kukamilika Kwa viwanja vya ndege zaidi ya 5 mwaka 2026

7.Utitiri na kumiminika Kwa wawekezaji hasa wa viwanda

8.Kupanuka Kwa Kasi Kwa sekta ya Utalii na Kilimo.

9.Kuanza Kwa biashara masaa 24 jijini Dar

10.Kuanza Kwa uzalishaji kwenye migodi mikubwa ya Madini hasa Kinywe Lindi na Karagwe/Kahama.

My Take
Samia ataandika historia ya kuwa Rais wa kwanza Kuipita Kenya kimapato mwaka 2027 lakini Kuipita Kiuchumi mwaka 2030.

View: https://www.instagram.com/p/DFLeLF6C3Su/?igsh=MWVwanRoZHFmbDNlZg==

Sasa nimeelewa ni kwanini uchaguzi wa TAL na Heche ulikutoa machozi.
 
Lete matokeo ya hizo Kodi kwenye maisha ya wananchi wa Kila siku.


Bima ya afya
Elimu ( bodi ya mikopo). Shule zina madawati ?
Barabara wilayani
Umeme
Ajira zikoje Kwa vijana


Kama Kodi hazina matokeo Kwa hivyo nilivyotaja hata tukusanye matrilion 7000 ya dollar hakuna maana.
 
hayo makusanyo hayana faida kama mpaka leo watoto wana kaa chini ili wasome, wananchi wanauwa mamba ili wapate maji, nchi imejaa wachuuzi na si watengeneza bidhaa
 
Miradi isiyokuwa na continuity haina maana. Mradi unajengwa kwa pesa nyingi ndani na miaka miwili ulishakufa.

Projects nyingi za hii serikali ya kifisadi ni White Elephant Projects.

Choke on it.
Mradi hauna continuity ndio nini? 😂😂

Mbona unatapatapa Mzee tatizo nini? Si ulisema tunagawana pesa saizi unabadili magoli? 😁😁

Bado hujasema Hadi useme.Hapa ni Lindi mabilioni Yako kazini Kwa Wananchi 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFLO6vhtNs0/?igsh=ODEwbXloMW9tZzYw
 
Lete matokeo ya hizo Kodi kwenye maisha ya wananchi wa Kila siku.


Bima ya afya
Elimu ( bodi ya mikopo). Shule zina madawati ?
Barabara wilayani
Umeme
Ajira zikoje Kwa vijana


Kama Kodi hazina matokeo Kwa hivyo nilivyotaja hata tukusanye matrilion 7000 ya dollar hakuna maana.
Matokeo ni zaidi ya extra ordinary across sectors na utambue kama Wananchi wako hoi kiuchumi Serikali isingepata hela .

Kazi inaendelea kama unavyoona 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFKgviaNpSo/?igsh=MWp2MTVjYjFoc3h0dA==
 
Tsh 1 trilion maana yake unaigawana kwa 19 upate KSH.

Tujitahidi hesabu zetu ziwe na uhalisia tunapotaka kufanya mashindano ya kweli.
Hujui kitu wewe ,hesabu ulipata zero bila shaka.

Chukua makusanyo ya Kenya hapo Juu zidisha na 1kes=19Tshs. Utapata jibu.
 
Back
Top Bottom