Bado una ndoto za kuzamia Ulaya?

Bado una ndoto za kuzamia Ulaya?

Bora mkienda huko Ulaya msiache kubeba vumbi la congo Ili maisha yakiwachapa mnaweza mkaonewa huruma na vibibi vya kizungu na nguvu ya vumbi ikawaokoa. Wale ni wapweke wanataka mtu wa kuwafariji.
 
Afrika hata ukienda zako Morogoro .ukatafuta bonde heka 5 ukapanda miwa baada ya miaka 2 sio mwenzetu unakuja kuuza Dar vijjwe vya juice, au unafungua vijiwe vya kuuza juice ya miwa.
.Unapanda minyonyo, mibono,milonge,miarobaini baada ya miezi tu unakamaua mafuta unatengeza sabuni unauza.
.Una kijiwe wilayani cha kufyatua tofauti za kuchoma unachoma kwa oil chafu watu wanajenga KILA siku Mungu akupe nini.
.Unaenda porini unaangua mibuyu kisha unatengeneza unga na mbegu unakamua mafuta unauza.
.Unalima mihogo, mtama unaweka kwenye magodown unasubiria msimu unauza unga, minadani Mungu akupe nini.
. Unanunua marobota ya mitumba Kazi yako kutembea kwenye minada unauza nguo, ukipata pesa unanunua mbuzi unaleta mjini, ukitoka mjini unachukua marobota ya mitumba unarudi nayo.
.Fungua vijiwe vya chai,kahawa,vitafunwa wilayani, vijijini,huku unawawekea tv wachek mpira bure unatoka
Fursa bado zipo tele afrika ni kuchanganywa tu ubongo,maana shida uleta akili.
Naona watu wataenda kulimia meno au sio..

Kilimo bila mtaji ni maumivu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naona watu wataenda kulimia meno au sio..

Kilimo bila mtaji ni maumivu.

#MaendeleoHayanaChama
Ukisubiri upate mtaji ndo ulime utasubiri sana.
Tumia kanuni ya kichina inasema usisubiri jembe ndipo uende Shamba anza hata kwa mikono jembe litafata.
Huku pwani watu wanapiga moto vichaka,kuna maeneo vipara tena hayana mvua wala rutuba mfano shinyanga,manyara, Dodoma,nk unapiga moto tu unapanda minyonyo,ndani ya miezi 3 unavuna mbegu tena minyonyo ustawi kwa umande haitaji mvua unapanda hata mvua ya mwisho, unapata mafuta ni wewe tu uuze soko la nje au utengeneze sabuni.Hata tu kufuga nyuki ushindwe Ili utoke.
Achaneni na kilimo cha complicated mfano kulima mahindi,ngano,viazi nk yapo mazao ni costless mfano kunde,mtama,karanga,nk uhitaji mbolea wala dawa.
Hata kufyatua tu tofali mbichi upate maisha nayo itakushinda.Tofali ya udongo mbichi uza hata sh 50 kwa tofali.
Chochote huwa ni kigumu kama ukitanguliza ugumu huwa,mbona wachina wao uona fursa kwann sisi tusizione.
 
Kule mwizi auliwi wala kuchomwa moto sio Buguruni kule
Bora uwe machinga kuliko kuwa mwizi.
Ukienda vijijini ulaya au nje ya mji utapata Kazi za kuchuma matunda,maua,kulisha ng'ombe,ufagizi,kutoa barafu,nk.Ukishajichanga unatafuta ujuzi mfano udereva unalipa ulaya. Mimi huwa nawashauri watu ni bora uzamie ulaya uwe na angalau ujuzi wa vitu viwili vitatu hivi angalau kapenta, rangi, ujenzi, welding, mechanics, au unesi. Taaluma haimtupi mtu taaluma ni kinga. Unaweza pata mtu anataka akusaidie atakuuliza who are you yaani una kipawa gani.
Ukienda Kavu Kavu utaolewa kwa maana ya ether mbili kuolewa na mwanamke au mwanaume, kule Hakuna mjomba au pa kugongea msosi.
 
Kutoboa Ulaya ni rahisi sana kuliko kwenye nchi za kimasikini

Hapo unawaona wanaingiza zaidi ya machinga wa huko
Na utakuta ana mipango yake mingine
Kupanga barabarani ni siku kadhaa tu sio kila siku sehemu zingine
Kwa hiyo utakuta wana kazi zingine na kukosa kazi Ulaya ni uzembe tu

Vijana msikariri maisha kila mahali unaweza kutoboa kama una malengo ya muda mrefu ila tatizo wengi wanataka kuwa matajiri kwa mwaka mmoja tu atakaopata kazi tra au uhamiaji [emoji23][emoji23]
 
Hii ni thd ya kujifariji kwa wale waliojikatia tamaa na waoga wakujaribu,

Napiga box mbele na maisha yapo poa kabisa,

Hako kakundi kadogo ka wamachinga ndio kana wakilisha Diaspora wote?

Endeleeni kujifariji,maisha ni popote,muhimu ni kujituma na kujiwekea malengo tu.
 
Mara kumi mtu akawe machinga ulaya kuliko maisha ya bongo
 
Huyu mtoa thread anayajua Maisha ya Mbongo kweli
99% ya watz Ni maskini wakutupwa.
 
maisha ya maskini wa Paris sio sawa na maskini wa Tanzania.

maskini wa Ulaya anaweza tumia Usd 20 ama zaidi (elfu 46 za kibongo) kwa siku wakati kwa Bongo huo ni mshahara wa meneja wa Tanesco kwa siku 1[emoji23][emoji23][emoji23]
Wewe ni sawa na wale wanaosema Bora kuwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa binadamu Africa

Hivi unajuwa kuandaa safari hadi kufika ulaya ni dola ngp?

Hizo pesa hazitoshi kufungua shughuli zozote hapa bongo na ukatoboa?
Kuliko kupoteza muda miaka 10 ulaya?
Visa $ 1500 ulaya.

Nauli $ 900- $1000

Jumla $ 2500.
 
Ila Bora ulaya.[emoji16][emoji16][emoji16].
Mchunga ng'ombe wa ulaya sio sawa na wa tanzania
 
Back
Top Bottom