SoC02 Bado upo umuhimu wa mtoto wa Kiume kuelimishwa kuhusu hedhi ya mtoto wa Kike

Stories of Change - 2022 Competition

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
Nini maana ya hedhi,

Hedhi ni kipindi au muda katika kila mwezi ambapo mwamke mwenye umri wa kuzaa hutokwa na damu kwenye uke ili kuanza mzunguko mwingine wa yai la uzazi. Kamusi ya kiswahili (karne ya 21 Toleo jipya) uk wa 147.

Nakumbaka mwaka 2007 ni kiwa darasa la tano ndani ya darasa letu kulitokea jambo lisilo la kawaida na ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuliona. Binti aliyekuwa anatuzidi umri alikuwa akitokwa na machozi akiwa ameinama kwenye dawati lake huku vijana wa kiume waliotazama chini ya dawati lake na kushuudia matone ya damu walianza kunongona huku wengine wakitoa maneno machafu ya Kebehi na vicheko kuwa “anavuja”. Ambao walikuwa na moyo wa huruma walionyesha uso wa huzuni na kumpa pole, hakunyanyuka kwenye dawati lake mpaka wanafunzi wote walipotawanyika na waliofika nyumbani walimuita baba yake na kuja kumchukua hapo shuleni.

Hatukujua nini maana yake kulinga na umri tuliokuwa nao hasa vijana wa kiume, iliisha hivyo bila kupata mwendelezo.

Mwaka 2008, 2009 tulianza kuona vikao vingi vya Mwalimu wa kike akivifanya kila mara na mabinti, ila hatukujua wanaongea nini na tuliweza kuwa na mabunio yafuatayo;

1.Kuna walimu wa kiume wanatembea na wanafunzi wa kike (wanamahusiano ya kimapenzi hivyo wanakatazwa. (bunio la vijana wa kiume).

2. Wanaenda kupimwa mimba kwani kulikuwepo na tetesi za kushikwa tumbo na “matroni wao”. ( bunio la vijana wa kiume). Hata wao walipotoka huko walikuwa wanaweka usiri mkubwa juu ya walichokuwa wanaongea.

Kama matone ya damu yangelikuwa yanaendelea kutokea basi hile hali ya kuchekwa isingelikoma kwani hatukujua ni nini kwa sababu ya usiri uliokuwepo hata wengine walikuwa hawaji kabisa shuleni, uenda walifanya hivyo pale walipohisi hali ya siku hizo kukaribia hivyo waliikwepa hiyo aibu kutoka kwa wavulana na wakawa wanahesabika kama watoro.

Mtu anaweza kubeza kuwa bado niko sana nyuma kuzungumzia matukio ya miaka kumi nyuma lakini myororo huu uliendelea hivyo hivyo na bado hadi sasa vijana wa kiume hawajui haya mabadiliko kwa usahii na hata kama hayawahusu lakini vyema wajue jinsi gani ya kuyapokea bila ya kuwacheka.

Mwaka 2010/2013 nikiwa sekondari matuko ya kubadilika kwa nyuso za mabinti, kujihisi upweke na hali ya ugonjwa vilionekane waziwazi na waliokuwa wanabaini hali hizo ni vijana wachache wa kiume. Wasichana waliendelea kuona tukio hili ni la Aibu na upweke pale waliposikia na kuhisi minongono ya chini chini pale vijana wa kiume walipokuwa wanawaongelea wao kuhusu hali zao huku wasiojua kile kinachowasibu wakitaka kukijua.

Zilipita kampeni za kuelimisha na kukusanya michango ya kuwanunulia mabinti nguo za kuwasitiri wakiwa katika siku zao huku wale wa maeneo ya vijijini wakiwasisitiza kutumia vitambaa safi vinavyopatikana kwa urahisi. Kempeini hizi zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na kuleta matokeo chanya na mimi kwa kipindi hicho nilikuwa chuo na ndipo nilpoanza kurejesha kumbukumbu zangu nyuma na kuyakumbuka matukio yale yaliyokuwa yakitokea nilipokuwa kwenye ngazi ya elimu ya msingi na Sekondari.

Nilipitia kwenye chuo cha Ualimu lakini sikupata elimu sahihi ya kuwaelimisha vijana wa kiume jinsi ya kuyapokea mabadiliko haya kwa upande wa wenzao yaani walione ni jambo la kawaida na nila kimabadiliko katika ukuaji, hata pia kwa upande wa kuwaelimisha vijana wa kike jukumu linabaki kwa walimu wa kike na kuoneka kama ni jambo la Aibu kuongelewa na mwalimu wa kiume. Je ni shule zote nchi nzima zina walimu wa kike.

Hata wenzetu wa kike tuliokuwa nao chuoni licha ya kupevuka kiakili tulipokuwa tunataka kuwadodosa katika hili walikuwa wanakuja juu na kudai hayo ni maswala ya kike na ni siri yao.

Baada ya kuhitimu chuo, Siku moja nilikuwa nakagua begi la mpwa wangu (binti) wa darasa la tano na niliyekua namuona bado ni mdogo kwenye makuzi na mabadiliko ya kimwili na kukuta kanga, niliposhangaa kuikuta huku nikisema labda anaitumia kwa michezo ya kibinti binti yaani kujiremba na kuigiza umama, lakini nilipoitoa na kumuuliza binamu yangu (mama yake) alinijibu kiaibu kuwa amemwekea kwa ajili ya mvua.

Nilipohoji kuwa msimu wa mvua umeisha kata, ndipo alipogundua sijaelewa na kujibu tu kifupi kuwa huyu binti yetu ameisha kua hivyo yeye ndiye anayemwekea hiyo kanga kwa ajili ya tahadhari, hapo alinifungua akili na macho lakini majibu yalikuwa ni mafupi aliyokuwa akiyatoa kama vile mimi kijana wa kiume sina haja ya kuwa na ufahamu wa hili jambo.

NINI KIFANYIKE
Sina nia ya kua kijana wa kiume afundishwe jinsi ya kuandaa na kutunza nguo za hedhi salama bali afahamishwe kuwa badiliko hili ni la kawaida katika upande wa ukuaji wa mtoto wa kike hivyo awe mstari wa mbele kumwondolea “shambulio la aibu” ili mabinti wajihisi wapo salama katika siku zao na kulichukulia jambo la kawaida bila kukatisha masomo yao hasa maeneo ya vijijini ambako hakuna redio wala televisheni za kuhabarisha kwa watu wote kuhusu ili jambo.

Hili likifanyika Mabinti watajisikia huru ata wakiwa kwenye siku zao kwani hawata waza tena kuhusu shambulio la aibu kutoka kwa vijana wenzao wa kiume na hawatokosa baadhi ya vipindi kwa kubaki nyumbani, hata kama si kwa kuwekwa kwenye mitahala na kwenye vitabu lakini walimu wote wapewe ujuzi wa kuwaelimisha pia vijana wa kiume kuhusu hili jambo hasa kwenye ukaziaji wa maarifa pindi watakapokuwa wanafundisha mabadiliko ya ukuaji kwa mtoto wa kike na kiume hususani mada ndogo ya balehe.

IMG_20220811_101805_556.jpg
 
Upvote 6
Hili andiko ni la msingi sana kwa watoto wa kiume na sisi wote wanaume. Mfano, mtoto wa like huumia sana akiona hakuna anayejali hali yake.
 
Tulipokee chanya kwa kuwaondolea shambulio la aibu
Ili wajisikie huru.
 
NINI KIFANYIKE.
Sina nia ya kua kijana wa kiume afundishwe jinsi ya kuandaa na kutunza nguo za hedhi salama bali afahamishwe kuwa badiliko hili ni la kawaida katika upande wa ukuaji wa mtoto wa kike hivyo awe mstari wa mbele kumwondolea “shambulio la aibu” ili mabinti wajihisi wapo salama katika siku zao na kulichukulia jambo la kawaida bila kukatisha masomo yao hasa maeneo ya vijijini ambako hakuna redio wala televisheni za kuhabarisha kwa watu wote kuhusu ili jambo.

Hili likifanyika Mabinti watajisikia huru ata wakiwa kwenye siku zao kwani hawata waza tena kuhusu shambulio la aibu kutoka kwa vijana wenzao wa kiume na hawatokosa baadhi ya vipindi kwa kubaki nyumbani, hata kama si kwa kuwekwa kwenye mitahala na kwenye vitabu lakini walimu wote wapewe ujuzi wa kuwaelimisha pia vijana wa kiume kuhusu hili jambo hasa kwenye ukaziaji wa maarifa pindi watakapokuwa wanafundisha mabadiliko ya ukuaji kwa mtoto wa kike na kiume hususani mada ndogo ya balehe.
Nimependa andiko lako,
Nimekumbuka niliyoyaona
 
Back
Top Bottom