Badoo inanivunjia uchumba wangu

Bro huyo mwanamke hakufai temana nae usipokubali now subiria HIV ujutie maishani
 
Aii jaman pole sana
Ila haya mambo ya kupimana haya jamani, ila hapana hapo kazidi... Elfu sabini ndo inamtoa roho namna hiyo,ni kweli wanawake tunapenda kusifiwa ila kuna kupima... Huyo kaingia mzima mzima

Hakufai kiukweli
 
Mkuu YAMENIKUTA nakushauri kabla hujafanya maamuzi kama ww ni mkristo tafuta wimbo wa Ambwene Mwasongwe-nguvu ya msamaha***** uusikilize
 
achana nae kiamani tu unaweza fanya hayo ila in return unajua yeye atafanyaje....usitake neno ninge lije kwako..
 
Wewe ni wakiume mkuu, Mungu pia amekuepushia kitu kwa kumgundua, huna haja kbs ya kusambaza picha zake, mjulishe tu wewe ndiwe boyfriend wake wa badoo, mwambie tu unashukuru kwa yooote. Ukianza kumfanyia ubaya huenda ukapatikana na hatia halafu atajiona yupo juu.
 
Ila hizi social network zinaharibu mahusiano kama mtu hujiheshimu.

Huyo dada ana mchumba,lakini bado anacheat mtandaoni. Muache huyo hakufai, hana hata staha Kwa mwili wake.
 
Dah! pole sana kk bt ndo ukubwa huo, ila kama wengi walivyokushauri, angalia mbele...achana naye tu. Aisee huu mtandao wa badoo ni hatari sana, girls wanajirahisisha sana, yaan sio siri huu kuna girls wako kule kwa ajili ya kuuza miili kisasa zaidi
 
Wanaume mkichapiwa mnachonga kwel kwel..
ila nyie mkichepuka mnaona sawa tuu..

anywy bro me niko single njoo tuyajenge kwanza situmii social media zaid ya JF na watsup ko usitegemee kuisikia tena hiyo badoo maishan mwako.
teh teh..
 
Kwa ukweli bro dunia hii hamna aliye msafi sabb Wanawake wana sema wanaume sio wa safi .na ss tuna sema wanawake sio wa safi . Tuko sawa .sasa kwa ushauri mwambie ukweli kama akuerewi achana naye kingine usikubari mwanamke akupande kichwani. And then tatizo umependa sana
 
tumia picha kama ushahidi kumfikishia mashtaka, then achana nae ganga yako baba....
 
Mkuu amua chochote ila usiposti hizo picha za uchi mtandaoni.

Turudi kwenye mada, huyo mtu wako nadhani ni limbukeni sana na hana uzoefu kabisa na mitandao kwa maana ya kutojua kujihadhari au ana fetish ya rangi tofauti au vyote viwili. Inawezekana alitaka kujaribu tu utamu wa dudu ya pink ndio maana akafikia huko. Nasema hivyo kwa sababu elfu 20 au 50 ni hela ndogo sana na sidhani kama inaweza kumchanganya mwanamke yeyote wa mjini tena ambaye yuko badoo.

La msingi mwambie ukweli muache bila hata ya kusambaza hizo picha. Jiulize hata ukisambaza itakusaidia nini?
 
Wanaume mkichapiwa mnachonga kwel kwel..
ila nyie mkichepuka mnaona sawa tuu..

anywy bro me niko single njoo tuyajenge kwanza situmii social media zaid ya JF na watsup ko usitegemee kuisikia tena hiyo badoo maishan mwako.
teh teh..
Kinachomuuma jamaa sio kuchapiwa ni haya hapa chini.
  1. Anamponda jamaa waziwazi kwa mtu ambaye hata hajawahi kumwona.
  2. Anatuma picha za uchi kirahisi sana.
  3. Anashawishika kirahisi mno hadi inakera na kutia hasira.
Kuchapiwa is one thing ila kuchapiwa na mwanamke huyo huyo akuponde na kisha amtumie mipicha ya k yake mchapaji ni jambo lingine kabisa.
 
Mwite mweleze ukweli na katika hiyo meeting tafuta shahidi ndugu au rafiki yake wa karibu mwonyeshe chat na picha zote kisha futa kila kitu anza upya.Usisambaze picha mtandaoni wala kwa Shigongo,inauma sana lakini overtime wewe ndio utakuwa mshindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…