Bagamoyo Airport or Extension of JKN Intl. Airport?


Mkuu,
Umenivunja MBAVU. Mwanzo nilikuwa nashangaa huyu jamaa kaandika MADUDU gani? Nilivyokusoma katikati ya mistari nimekupata mkuu wangu. Ni Limbukeni tu anaweza kwenda kujenga uwanja wa ndege Bagamoyo na kutegemea watu watumie kuingia mjini Dar. Kama ile barabara ya Bagamoyo kwa sasa imeshafurika, ukiongeza na watu wanaoenda Bagamoyo? Pia huko ni mbali saana. Itabidi mtu uondoke masaa 5 kabla kama una ndege za jioni.

Nchi nyingi wakijenga viwanja kama hivi basi wanaweza vitu kama Metro au Matrain ya speed kali ili kufikisha watu mjini haraka. Sasa sisi tutabanana wote kwenye hicho kibarabara? Pale ulipo wa sasa ni safi sana ila sema walijisahau kujenga HIGHWAYS walau mbili kuja pale Airport ambazo zinauzunguka mji kutoka Kivukoni hadi Mbezi beach/Tegeta.

Nyie mbona hamtaki kueleze ukweli

hivi vyote vingejengwa Moshi au Arusha ingeonekana its normal

wacha wajenge Bagamoyo wakimaliza wakajenge na ule mradi mkubwa zaidi kule Pemba

sioni tatizo liko wapi

Mkuu GT,

Ili uyafahamu haya mambo, inabidi usome Traffic Engineering na UCHUMI. T.Eng. nimeshasema mara nyingi ni somo ambalo si tu usome na ufaulu ndiyo uwe Mhandisi, inatakiwa UZOEFU. Kutokana na Mkuu Moran75, hawa watu Tanzania wapo wachache sana ambao wengi ni wamesoma na hafanyi kazi kwenye hizo field.

Sasa Mkuu, hii kitu inahitaji kuipa heshima na kuwaacha wataalamu wafanye kazi. Yaleyale ya TANESCO.

Amini usiamini, ndege zote zitakazotaka kutua Bagamoyo zitakuwa na shida sana kupata WASAFIRI kwani wengi watataka kutua DIA. Historia dunia nzima inaonyesha hivyo. Hakuna atakayekuwa tayari kwenda mbali namna hiyo kupanda pipa labda kama hana njia nyingine. Hicho kiwanja kitakufa natural death na atabaki anakitumia yeye na wanae.
 
Yaani hata TESHA anasema kabisa kuwa "viwanja vinaleta hasara" na bado wanataka kuongeza vingine. Mfipa wetu na yeye anataka kujenga Rukwa Interneation Airport.

Yaani linchi ninaendeshwa bila wataalamu kabisa.

 


ukikataa mpango wa kujenga bandari au Air port Bagamoyo,basi pia ukatae mpango wa EPZA ambao wananchi wa bagamoyo wanalia kuhusu malipo ya ardhi zao ambazo serikali inazichukua kwa vijipesa kiduchu.
Ni maendeleo na hatuna budi kuyakubari,bagamoyo ilikuwapo toka 1961 na nyuma zaidi ya hapo,na angalia maendeleo yanakuja lini 2005?hata barabara ya lami imejengwa mwaka 2001.sasa hivi unaenda bagamoyo ya kwa dk 45 zamani tulikua tunaenda masaa 4
 



Kiwanja na bandari hiyo inayo jengwa Bagamoyo sasa hivi sio sana kwa abiria kama wengi tunavyo fikiri,ni kwa ajiri ya EXPORT PROCESSING ZONE ,ambayo proect imeshaanza kushika kasi.
Sasa sijui mnategemea watu wafanye processing Bagamoyo alafu wabebe wapeleke bandari Dar?
 
Sikonge,
Mkuu wangu ukiisoma taarifa nzima kwa makini utagundua kwamba tatizo la nchi yetu ni UONGOZI bora ktk sekta zote..Ikiwa kweli tunashindwa kuvihudia viwanja vyetu hapo vilipo kuna umuhimu gani wa kujenga vipya?..
Uliza nchi zote duniani watakwambia kwamba Ubora wa kiwanja cha ndege na huduma zake ni sababu kubwa ya ndege nyingi kufikia hapo. Ni sawa na Bandari au hata barabara kwani wenye magari wanaokwenda Mwanza kupitia Kenya hawakupenda kufanya hivyo isipokuwa ni kutokana na ubovu wa barabara zetu..

Binafsi swala la Bandari yetu naliunga mkono kabisa, ile bandari yetu pale Dar haifai kabisa na sababu zipo nyingi na wazi. haiwezi kuongezwa wala kuboreshwa kwa malengo ya kuchukua meli nyingi zaidi..Ifungwe kabisa kuhusiana na mizigo na kujengwa sehemu nyingine iwe Kigamboni au Bagamoyo.
Pia wazo la kuboreshwa bandari za Tanga na Mtwara ni muhimu kuondokana na ujenzi mpya wa bandari wakati tunashindwa kuzihuddumia zilizopo hivyo nguvu ya fedha iwekwe ktk Bandari tulokuwa nazo..Hiyo bandari ya Dar abaakie kama bandari ya Utalii (Cruisership) safari za Abiria kwenda Unguja, Pemba, Comoro, Na Mombasani..ramani ya mji mpya wa Dar nadhani imeonyesha wazi umuhimu wa kuuboresha mji wa Dar kwa malengo ya Utalii zaidi ya mizigo.

Lakini kuhusu kiwanja cha ndege kujengwa Bagamoyo kusema kweli hili tunatupa fedha nyingine pasipo sababu kabisa. Uwanja wa JKN unaweza kabisa kuboreshwa na kuchukua hatua kubwa kufikia malengo yoyote yale. Nafasi kubwa bado ipo na hakuna sababu ya msingi kutoiboresha Airport hiyo na ile ya Kilimanjaro.
Pia hizo Airport nyinginezo zinahitaji zaidi ukarabati (Utamaduni tusokuwa nao) kuliko kuingia gharama nyinginezo zisizokuwa namsingi kabisa. Kuna njia mbili muhimu sana za usafirishaji wa mizigo ambazo zinatakiwa kuwekewa maanani kabla ya kufikiria kuhamisha Bandari au Airport nazo ni reli zetu za kati na Tazara kwani mali yote inayokuja kwa ndege au Bandari husafirishwa kwa njia hizo kwenda nchi jirani...Tukihamisha Airport na Bandari kutakuwepo na connection gani baina yao na reli kisha kwa gharama gani?...
Tukumbuke tu faida kubwa ya Usafiri wa ndege na meli hutokana na biashara ya mizigo zaidi ya usafiri wa Abiria. Hivyo ni muhimu wa serikali kuzingatia vyanzo hivyo kwa wafanyabiashara (wenye Ndege na Meli).
 


Naomba nizungumzie jambo hili hapo japo kuweka sawa mambo,

Shukuru Ramadhani Kawambwa sio Rafiki wa Musheshimiwa Rais,na wala wawili hao walikua hawajuani ingawa wanatoka sehemu moja yaani Bagamoyo.wamejuana mwaka 2005
Dk Kawambwa ni msomo mzuri tu na alikua hajishughulishi na maswala ya siasa,ni msomi mfano wa kuigwa kwa Wabagamoyo wote ambako kwetu wasomi wa aina yake ni wachache sana.
waliopita na kusoma Chuo kikuu cha Dar es salaam wanaweza kuwa mashahidi wa hili
 
Mimi swali langu ni: Ule mpango wakujenga "International Airport" nje kidogo ya Dodoma umefikia wapi. Kwani kwangu this makes more sense considering Dodoma ndio "Administrative Capital", pia ita-stimulate maendeleo ya Central Tanzania.

Ila hii ya Bwagamoyo, as they say it "Only in Tanzania" can this be possible.
 
Kabla hujazungumzia Kiwanja jiulize ya Makao makuu yamefikia wapi?
 

Lete evidence kussuport hii hoja

Nasema data na research..uonyeshe ilifanywa na nani na walitumia methodology gani mpaka wakafikia uamuzi huo
 

non sense.....
 
Game theory,

Nakubaliana na wewe kwamaba "enzi ya kuthink small" imeshapitwa na wakati na sasa lets think out of the box. Lakini mi nafikiri wadau wanachohoji zaidi hapa ni allocation hiyo ya resources na infrastructure kama hizo inaonekana kama vile haziko fair na pia zimeegamia upande mmoja. Nakubali Bagamoyo ilikuwa nyuma na pengine bado iko nyuma kimaendeleo na inahitaji namna ili iweze kuinuliwa lakini sio kwa namna hii ya unfair distribution ya miradi? Iweje leo miradi yote hiyo iende Bagamoyo? Kama wadau walivotoa data kiwanja kilitakiwa kijengwe Mkuranga sasa kulikoni tena Bagamoyo? Nakubali kuwa Dar sasa iko congested sana inahitajiak kiwanja kingine nje ya Dar, why not Mkuranga?
Pia wana JF kuwakumbusha tu inaonekana kila kiongozi akiingia anakumbuka kwake tu, Mzee Msuya nasikia Ugweno umeme mpaka kwenye midizi lakini sehemu zingine za Mwaga kiza. Mwandosya naye alipokuwa waziri wa Mawasiliano mradi wa Airport kule Songwe Mbeya ulianza na ulikuwa unaendelea vizuri sana lakini alipotoka wizara hiyo tu, kila kitu kwishinee!

Is our president biased?
 

Game theory,

Nakubaliana na wewe kwamaba "enzi ya kuthink small" imeshapitwa na wakati na sasa lets think out of the box. Lakini mi nafikiri wadau wanachohoji zaidi hapa ni allocation hiyo ya resources na infrastructure kama hizo inaonekana kama vile haziko fair na pia zimeegamia upande mmoja. Nakubali Bagamoyo ilikuwa nyuma na pengine bado iko nyuma kimaendeleo na inahitaji namna ili iweze kuinuliwa lakini sio kwa namna hii ya unfair distribution ya miradi? Iweje leo miradi yote hiyo iende Bagamoyo? Kama wadau walivotoa data kiwanja kilitakiwa kijengwe Mkuranga sasa kulikoni tena Bagamoyo? Nakubali kuwa Dar sasa iko congested sana inahitajiak kiwanja kingine nje ya Dar, why not Mkuranga?
Pia wana JF kuwakumbusha tu inaonekana kila kiongozi akiingia anakumbuka kwake tu, Mzee Msuya nasikia Ugweno umeme mpaka kwenye midizi lakini sehemu zingine za Mwaga kiza. Mwandosya naye alipokuwa waziri wa Mawasiliano mradi wa Airport kule Songwe Mbeya ulianza na ulikuwa unaendelea vizuri sana lakini alipotoka wizara hiyo tu, kila kitu kwishinee!

Is our president biased?
 
Hata mkila majani uwanja wa Bagamoyo lazima utajengwa na ili hili liweze kufanyika JK lazima aongezewe awamu ya pili. Kuna msukumo mkubwa kutoka kwa wanaoitwa wawekezaji - hakika Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu, vinyozi wanafunzi rukhsa. Tumewahi kununua mitambo ya umeme kutoka kwa wauza stationary lakini hili la kiwanja cha ndege lafunga mwaka - yangu macho.
 


- Mkulu PM, with all due respect hebu na wengine waendelezwe pia, I mean sasa akitoka bila kufanya kitu yatakuwa makubwa kuliko haya, kutesa kwa zamu jamani, kwa hili mnyonge mnyongeni tuwaachieni na wengine nao wasogee kidogo!

- Kweli mnataka akitoka Ikulu aende wapi?, Lushoto kama yule mwingine aliyekimbia kwao kwa sababu hakufanya kitu mambo ya utandawazi tu! akhaa kuweni na huruma kidogo!

- Infact, mkulu yupo mjini ngoja nimuwahi kula dataz kidogo, kabla hajaanua!

Respect.


FMEs!
 
mimi sishangai kuona tesha anafanya maamuzi haya kwani alikuwa ni mtu wa hovyo pale UDSM. Tesha amesoma NIT na baada ya diploma hiyo ya NIT alikuja UDSM na akamiliza BSC Mechanical eng. Cha ajabu ni kuwa wahandisi hawa wanatuangusha.

Tesha wewe ulikuwa mchafumweli chumbani kwako pale Hall 5 UDSM, unaendeleza uchafu huo hadi ktk kufanya maamuzi???

Imarisheni JNIA na KIA achananeni na Bagamoyo international airport.
 
Ikiwa ni kweli wanataka kujenga Airport BAgamoyo itakuwa ni aina nyingine ya ufisadi- yaani 60 kms form JKN Airport kuna Airport nyingine na wakati huohuo wanataka kuipanua JKN Airport na wakazi wa Kipawa wameshahamishwa!

Nimekuwa nikijiuliza kwa nini Serikali isiunganishe Terminal 1 (Airport ya zamani) na JKN Airport? Mimi naonaga Aibu sana nikipita Jomo Kenyatta International Airport Nairibo, naona Uwanja wetu wa JKN ni kama Kijiji ukilinganisha na Jiji (Jomo Kenyata Airport). Kama tungeweza kuweka jengo refu ambalo mtu anaweza kupita ndani kwa ndani kutoka Termional One hadi JKN Airport ingekuwa bomba sana.
 
Lete evidence kussuport hii hoja

Nasema data na research..uonyeshe ilifanywa na nani na walitumia methodology gani mpaka wakafikia uamuzi huo

GT,
Peking na mahela yao yote bado wanabanana kwenye kiwanja cha zamani. Mifano iko mingi sana ila mingi kwa sababu fulani siwezi kukupa kwani ni mipango ya nchi kadhaa kufanya jambo kama hilo ila mwisho waliamua kuliacha hadi hapo baadaye na mfano milele umekuwa kiwanja cha ndege cha Montreal kilichofunguliwa mwaka 1975 kwa ajili ya Summer Olympic (soma chini kwa maelezo zaidi).

Hata Berlin kwa sasa wanajenga nje ya mji na kiwanja chao kimoja wamekifunga ila wenzetu kama nilivyosema kuwa wakifanya hivyo basi watajenga Metro, Highways, Matrain ya speed kali hadi Berlin Main Railway Station (Berlin Hauptbahnhof).

Tatizo la Tanzania, sidhani kama hata hiyo REAL highway (ambayo haitakuwa na collitions zozote unapotoka Dar hadi Airport Bagamoyo katika sehemu za Interchange) watafanikiwa kujenga. Kama sasa hivi foleni za Dar zinatushinda, za kutoka Bagamoyo tutaziweza? Mie ikibidi kulipa dola 100 zaidi ili nishuke DIA basi nitafanya hivyo. Huko shamba itakuwa kama vile umeenda kupandia ndege Kilimanjaro au Nairobi.

Haya, umetaka mfano, ngoja nikupe shule ili siku nyingine mambo ya Traffic Engineering uyape heshima. Lowassa aliyaparamia yakamuweka chini pwaa na barabara zake tatu. Alifikiri tatizo ni lanes. Hafahamu kua siku zote tatizo ni makutano ya barabara ndiyo yanaleta msongamano.




Ukitaka maelezo zaidi ya UGOMVI wa hizi Airport mbili ambazo zimekuwa zikiwashutuwa Wahandisi wengi kujenga airport mbili zikiwa karibu karibu na katika mji mdogo basi soma hapa:
http://en.wikipedia.org/wiki/Montréal-Mirabel_International_Airport
 

Mkuu FMes,

Dar hadi Bagamoyo ni km 40 nasikia. Ukiangalia ndiyo distance ya viwanja viwili nilivyowandikia GT. Kimoja kimekufa na kimebaki kilekile cha zamani. Ukweli ni huu niliundika kuwa abiria walikuwa wakikataa kupanda ndege zinazoshukia mbali na mji.

Na kwa hali ilivyo Tanzania, anaweza akaja Membe mwaka 2015 na kusema hataki kushukia Bagamoyo maana ni mbali na akakirudisha kiwanja cha DIA.

Kwa nini wanafukuza wananchi Kipawa na huku wanataka kujenga Bagamoyo? Sidhani kama watalazimisha wenye ndege watue huko. Labda libaki kuwa Cargo airport na pembeni mwake Bandari. Ila DIA bado haijashiba ndege hadi sasa.
 

Attachments

  • Monteal.JPG
    139.6 KB · Views: 61
niliongea na mtaalamu wa masuala ya ndege akasema kwa sheria ( as he told me) uwanja wa ndege wa kimataifa unatakiwa uwe na "alternative landing ground, in case of any thing" akanipa mfano wa KIA na Arusha, na Jomo kinyata na Wiliams sasa sijui ndio maana wanajenga bagamoyo au vipi, ila kwangu mimi bandari na reli ndo priority ila ndo hivyo viongozi wetu n i mabigwa wa rivasi (reverse) kwenye kufikiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…