kwa kifupi ninacho maanisha ni kwamba ukitaka kuleta maendeleo sehemu yoyote ile, basi ni vizuri ukaanza na kujiwekea hali ya kuleta hayo maendeleo, sasa tukirudi kwenye suala la Bagamoyo iwe mlingotini nk , tuanze na barabara ambazo zitaunganisha na sehemu zingine za nchi , kwani suala la kiuchumi ni la kutegemeana, jingine ni kuwa na usafiri wa reli mzuri, ambao baadae uta support hiyo processing zone hapo bagamoyo, maana usitegeme pamba itakuja kwa ndege/tumbaku nk nk, na jingine ni la umeme ambao litachoche elimu bora, uzalisha, na mazingira yote kwa ujumla, maana hata hiyo airport inategemeana na uwepo wa nyenzo kama umeme na watu wenye elimu bora.
kwa hiyo wote tuwekeze akili zetu na nguvu zetu kwenye vitu kama hivyo basi maendeleo mengine yatakuja kwa urahisi na speed inayotakikana bila kuathiri nguzo za kiuchumi ama sivyo tutajiwekea dhana ya kwamba mimi kwetu kumesahaulika nataka hichi nataka kile halafu kikiwekwa hakikusaidi kwa sababu umeacha vitu vya msingi.
kwa hiyo kwenye nia yako au plan naomba uanze na vitu vya msingi, na kama unaukaribu na viongozi/mbunge wako naomba uwaeleze kuwa usafiri bora (barabara, Reli) ambao utatuwezesha sisi wafanyakazi kutoka sehemu mbali mbali za tanzania kuja bagamoyo kufanya kazi au kuleta mali ghafi zetu kwa ajili ya epz na Nguvu za Umeme ndio utachochea maendeleo mengine, iwe bandari, airport nk na vitu hivi sio vinakuja overnight vinahitaji mipango ya muda mfupi , kati na muda mrefu
maelezo mengine naona Mkandara nae kaelezea vizuri suala hili.
Mkulu,
Sitaki ionekane kama tunabishana,nataka kukuambia kwamba mimi nakubariana na sababu zako,hasa zile za msingi ambazo wewe na wachangiaji wengine mmezitoa.
Ila kwako inaonyesha wazi kwamba sababu zako nyingine si za msingi kwani hata jogulafia ya maeneo husika huiju na mipango ya serikali inayoendelea kwa maana ya projects either za barabara na hata za mpango mzima wa EPZA ambao umeshaanza pia hujui au hujaona.
Kwa benefit yako na wengine amabao hawalijui hili inawezekana wako nnje ya inchi,Serikali ilishaanza kujenga miundombinu ya hiyo zone ya EP kwa kushirikiana na nchi wanachama wa EA toka hatua za mwanzao mwazo wa kuunda upya wa umoja wao,awamu ya 3 ya uongozi hapa kwetu.mfano barabara ambayo ilianza kujengwa kwenye mpango huu ni ile iliyokua ikiunganisha mkoa wa Tanga na Mombasa,kuanzia maeneo ya Mabokweni mapaka Horohoro kupitia Duga Mafoloni,hii ilishaanza hata Kikwete hajapendekezwa na NEC kugombea na fasasi ya Urais,let alone Kawambwa
Lengo likiwa kuonganisha Mombasa Tanga na hii EPZ kwa kutumia barabara,kwani reli ya kuonganisha maeneo hayo ipo ila ilihitaji kukarabatiwa tu na kuonganisha vipande vichache vichache ambapo kwa bagamoyo kwenye hiyo zone yenyewe kipande kisicho zidi km 30 kinahitajika kuonganisha.kwa sasa ile reli ya kati iliyo kua ikionganisha Dar na Tanga inapita maeneo ya wilaya ya Bagamoyo sehemu za Kidomole,si zaidi ya km nilizo zitaja hapo juu kutoka maeneo ya EPZ.
Kwa kuongezea pia barabara imeshaanza kujengwa na ipo kwenye hatua za mwisho kutoka Chalinze(ikionganisha mikoa ya kati) kwenda Segera zikiwekwa njia nne(watu walimkosoa kawambwa kwenye hili),na Msata (maungio yanayo uganisha wilaya ya bagamoyo na njia hii kubwa kwenda Tanga) kurudi Bong"wa wilaya ya Bagamoyo ambapo pia imesekana barabara nne zitajengwa mpaka either Mbuyuni njia ya kwenda kunduchi au Mwenge(hii itarahisisha sana usafiri kwenda na kutoka maeneo hayo,na hata wale wenye nyumba ambao wanalalamika kodi kushuka watakua na nafasi tena ya kupandisha) .
Swala la umeme,ingawa Mlingotini kunaweza kua hakuna umeme,lakini ukipita barabarani kwenda bagamoyo utaona Tanesco walivyo fanya kazi nzuri kupeleka umeme maeneo husika ya Mradi huu,maguzo makubwa ya umeme w a viwanda yamepita kwenda huko(umeme huu hauingii kokote zaidi ya sehemu husika,kiasi cha kwamba watu wenye nyumba zo zenyekuhitaji umeme maeneo ya Bunju B hawapati umeme huo inawa umepita maeneo hayo tena juu ya mapaa yao)
Nadhani kwa kiasi furani nitakua nimesaidia kuelewehana kwenye hili la ujengwaji wa mji wa bagamoyo,sio sababu ya kuwepo Kikwete madarakani na Shukuru kama waziri wa miundombino ila ni mpango wa serikali zaidi ya tano sasa,mwanzoni ilikua ni inchi 3.na mpano ni wamuda mrefu hata kikwete hajawa MFALME