kaka you spoke it all....kabla ya uhuru ufalme wa kilimanjaro tayari ulikuwa na serikali ,baraza la ushauri[mawaziri],ikulu,bunge ....yote ya kisasa ...na hadi sasa rais akiwa kilimanjaro hufikia kwenye ikulu iliyojengwa na wachagga hao...na bunge lao ndio makao makuu ya wilaya..moshi vijijini...
kabla ya uhuru tayari ufalme wao ulikuwa umejenga chuo cha ushirika,chuo cha kahawa,lyamungo,etc..
upande wa afya kwa kushirikiana na mashirika ya dini walishajenga hospitali kila tarafa...hospityali ya kibosho,marangu,na machame....
upande wa elimu ya msingi walikuwa wakisambaza vitabu na madaftari yenye nemmbo yao ya chui....kwa watoto wote ...na walikuwa wakisomesha watoto [scholarships]
upande wa fedha na biashara ..tayari kwa kupitia chama cha ushirika moja ya vya mwanzo afrika KNCU ...WALIkuwa wakiuza kahawa nje....na walikuwa na akaunti za fedha za kigeni nje ya nchi.....
upande wa umwagiliaji ...hata kabla ya uhuru tawala yao ilikuwa imeshajenga mfumo wa umwagiliaji wa mashamba ya mogomba na kahawa kwenye viijiji vyote na ikisimamiwa kimila....
barabara baadhi hasa za vijijini zilishajengwa kwa kujitolea..
Upande wa utalii tayari wakikuwa na hoteli ya mwanzo kabisa tanganyika kuwa na lift .na kuwa ya kitalii...KNCU hotel....
MALI ZOTE HIZI PAMOJA NA AKAUNTI ZA FEDHA ZA KIGENI ZILITAIFISHWA NA SERIKALI NA WATU WA MKOA HUO WALA HAWAJAWAHI KUONGELEA KUDAI PESA ZAO ZA KODI WALIZOKUWA WAKILIPA KWA MANGI ZILIZOJENGA VITEGA UCHUMI HIVYO KWA SERIKALI!!
ndio maana huwa haingii akilini na ni kama tusi kusema wananchi wa kilimanjaro kuwa wameshapata upendeleo na serikali ......kwa kuwa ni kweli HATA AKIFUFUKA MTU ALIYEKUFA MWAKA 1967....HATAKUTA MKOA UMEBADILIKA SANA zaidi ya idadi ya watu na ukame kuongezeka ..NA HASA DHELUJI YA MLIMA KUENDELEA KUPOTEA KUTOKANA NA SHUGHULI ZA KIBINADAMU......ni wazi kuwa kama upendeleo wowote ungefanyika kilimanjaro basi...leo hii labda ingeweza kuwa mbele zaidi na tofauti ingeonekana dhahiri.....leo hii majengo mengi mazuri yanajengwa na vijana wanaoamua kuwekeza kwao...kwani kwa watu wa kule hona aibu sana ....familia kukosa maendeleo....na sasa utashangaa baadhi ya vijiji tayari wanaona ni kila familia inatakiwa kuwa na ghorofa.....!!..
nadhani watanzania tushindane kwa maendeleo.....ni vema wakazi wa maeneo mengine nchini wakatembelea maeneo ya vijijini kilimanjaro na kuona wakazi wa huko wamewezaje kujiletea maendeleo kuanzia ngazi ya familia bila kungoja serikali......badala ya kufikiria vinginevyo!!