nashukuru mzima
JF-Expert Member
- Jul 11, 2017
- 1,014
- 1,903
Baadhi ya Waombolezaji kwenye msiba wa Kijana Henry Massawe aliyekuwa Mkazi wa Kiaraka Magengeni, Bagamoyo Mkoani Pwani, wamelazimika kuvunja geti la nyumbani kwa Marehemu ili kuingia kumzika baada ya kukuta geti hilo limefungwa huku Mke wake akiwa hajulikani alipo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Mahakama ya Bagamoyo kuamuru Marehemu azikwe Bagamoyo na sio Kilimanjaro kama alivyotaka Mkewe.
Kabla ya kuvunjwa kwa geti hilo Waombolezaji walikuwa wamekaa nje wakati wote na baada ya hapo wakaingia na kuuvunja pia mlango wa nyumba ya Marehemu ili mwili uingizwe sebuleni kama ilivyo taratibu za misiba ya kikristo.
Henry Massawe alifariki January 16, 2023 na mwili wake ulisubiri kuzikwa kwa wakati wote huo kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya Ndugu wa Marehemu waliotaka azikwe nyumbani kwake Bagamoyo huku Mke wa Marehemu akitaka azikwe Kilimanjaro kabla ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Vedatus Mwalia kuamua kuwa Marehemu azikwe Bagamoyo.
Mahakama ya Bagamoyo mkoani Pwani leo January 24 2023 kuamuru mwili wa Henry Massawe kuzikwa nyumbani kwake Kiaraka, Bagamoyo kama watakavyo Ndugu zake na kutupilia mbali hoja za Mke wake aliyetaka akazikwe Mkoani Kilimanjaro.
Ndugu Jamaa na Marafiki waliojitokeza kwa ajili ya maziko ya Marehemu Henry wamekuta geti la nyumbani kwake limefungwa huku ikielezwa kuwa Mkewe hajulikani alipo.