Bagamoyo: Mwanamke ashindwa kuzika mwili wa mumewe. Mgogoro wasababisha afunge geti marehemu alikopaswa kuzikwa na kutokomea kusikojulikana

Bagamoyo: Mwanamke ashindwa kuzika mwili wa mumewe. Mgogoro wasababisha afunge geti marehemu alikopaswa kuzikwa na kutokomea kusikojulikana

Mke wa marehemu, Janeth Ikuyumba anataka mwili wa mumewe ukazikwe Moshi mkoani Kilimanjaro alikozaliwa wakati ndugu wa marehemu wanataka uzikwe nyumbani kwake Kiharaka, Bagamoyo mkoani Pwani.

Licha ya kaburi kuchimbwa nyumbani kwake Kiharaka, mwili wa kijana huyo aliyefariki dunia Januari 16 mwaka huu kwenye Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam, haujazikwa.

Mmoja wa mashuhuda wa mgogoro huo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, alidai kuwa kabla ya kifo chake, kijana huyo aliyekuwa Ofisa Viwango TBS, aliomba akifariki dunia, azikwe nyumbani kwake.

"Ijumaa (iliyopita), tuliandaa kaburi ili tumzike Henry lakini mvutano ulizidi kiasi kwamba tulishindwa kuzika. Mke anadai kwamba anataka kuipangisha nyumba, hivyo kukiwa na kaburi, itamkosesha biashara," alidai shuhuda huyo.

Aliendelea kudai kuwa mke amekataa kumzika mumewe kwenye eneo alilochagua kwa kuwa "hata akitaka kuuza nyumba, itakuwa ngumu kuuzika."
Alisema kuwa Masawe ameacha mtoto mmoja wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili.

NIPASHE ilipomtafuta mke wa marehemu, Janeth Ikuyumba kuhusu suala hilo, alikataa kulizungumzia kwa madai kwamba aliyetoa taarifa ya mvutano huo, anayo maelezo ya kutosha.

"Kamuulize huyo aliyekwambia hizi habari, akufafanulie zaidi maana inaonekana anajua kila kitu, mimi sina cha kusema," alisema.

NIPASHE ilimtafuta dada wa marehemu, Sesilia Massawe ambaye alithibitisha kuwapo mvutano huo.

Hata hivyo, alishindwa kutoa ufafanuzi zaidi kwa maelezo kuwa yuko kikaoni na kwa zaidi ya saa tatu alikuwa kikaoni na kila akipigiwa alijibu kuwa hawezi kuongea kwa kuwa kikao kilikuwa hakijamalizika.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kiharaka Magengeni, Simon Kilian alithibitisha kuwapo mvutano huo, lakini alikataa kutoa ufafanuzi kwa njia ya simu.

Jirani wa familia hiyo, Fatuma Chombo, alidai: "Tumeishi na Henry vizuri sana, alikuwa anasalimia mkubwa hadi mdogo, kaburi limeshachimbwa halafu tunaambiwa hatazikwa Kiharaka, tupo hapa hadi azikwe hapa.

"Tunasikia mke anataka asafirishwe lakini ndugu wa mume wanataka azikwe hapa, jana (juzi) tulikuwa hapa tukatangaziwa anazikwa leo (jana), cha ajabu tumefika hapa tunaambiwa hazikwi hapa na kaburi limechimbwa."

Alidai kuwa awali waliambiwa hawawezi kuchimba kaburi hadi kibali kipatikane na walitafuta kibali kikapatikana kwa viongozi wote na kuruhusiwa kuchimba kaburi tangu juzi.

Alidai kuwa kijana huyo alitakiwa kuzikwa Januari 20, mwaka huu, lakini hadi jana mwili ulikuwa haujafika nyumbani.
 
Hivi ukishakuwa na ndoa mwenye haki ya kuzika ni mke au ndugu wa mume?

Naona kama umetukana bila sababu hivi.
Kambaku;
Nadhani hakimu alizingatia wosia wa marehemu. Ikiwa mke ana "nguvu" kuwashinda ndugu wa marehemu anaweza kuchagua pahala pa kuzika. Lakini mara nyingi sana mke huwa mshindwa katika hili, sijui kwa nini!
 
Baadhi ya Waombolezaji kwenye msiba wa Kijana Henry Massawe aliyekua Mkazi wa Kiaraka Magengeni, Bagamoyo Mkoani Pwani, wamelazimika kuvunja geiti la nyumbani kwa Marehemu ili kuingia kumzika baada ya kukuta geiti hilo limefungwa huku Mke wake akiwa hajulikani alipo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Mahakama ya Bagamoyo kuamuru Marehemu azikwe Bagamoyo na sio Kilimanjaro kama alivyotaka Mkewe.

kabla ya kuvunjwa kwa geiti hilo Waombolezaji walikua wamekaa nje wakati wote na baada ya hapo wakaingia na kuuvunja pia mlango wa nyumba ya Marehemu ili mwili uingizwe sebuleni kama ilivyo taratibu za misiba ya kikristo.

Henry Massawe alifariki January 16, 2023 na mwili wake ulisubiri kuzikwa kwa wakati wote huo kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya Ndugu wa Marehemu waliotaka azikwe nyumbani kwake Bagamoyo huku Mke wa Marehemu akitaka azikwe Kilimanjaro kabla ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Vedatus Mwalia kuamua kuwa Marehemu azikwe Bagamoyo ,
Mahakama ya Bagamoyo mkoani Pwani leo January 24 2023 kuamuru mwili wa Henry Massawe kuzikwa nyumbani kwake Kiaraka, Bagamoyo kama watakavyo Ndugu zake na kutupilia mbali hoja za Mke wake aliyetaka akazikwe Mkoani Kilimanjaro, Ndugu Jamaa na Marafiki waliojitokeza kwa ajili ya maziko ya Marehemu Henry wamekuta geti la nyumbani kwake limefungwa huku ikielezwa kuwa Mkewe hajulikani alipo,
Sidhani kama angekuwa mgonjwa hoi angegombaniwa ili atibiwe
 
Mambo mengine ni upuuzi tu, huyo alitaka kujimilikisha msiba Ili akapate michango Kwa ndugu zake huko. Ndugu wa Mume wapo sahihi na wasibabaishwe na huyo mke wao.
Marehemu hakuacha Wosia wowote kuhusu wapi azikwe? Mimi tayari nimeshaambia mke wangu na ndugu zangu kwamba nikifa nikazikwe kwenye makaburi ya ukoo wetu huko kijijini kwetu Moshi, na sehemu ya kuzikwa nimeshawaonyesha kwamba nizikwe hapa.

Kurahisisha kusafirisha mwili nina mpango wa kukata bima ya maisha ya walau milioni 4 (life insurance). Haya mambo ukiyapangilia yanasaidia sana kuondokana na hii migogoro wajameni, hebu tubadilike wakuu.
 
Marehemu hakuacha Wosia wowote kuhusu wapi azikwe? Mimi tayari nimeshaambia mke wangu na ndugu zangu kwamba nikifa nikazikwe kwenye makaburi ya ukoo wetu huko kijijini kwetu Moshi, na sehemu ya kuzikwa nimeshawaonyesha kwamba nizikwe hapa. Kurahisisha kusafirisha mwili nina mpango wa kukata bima ya maisha ya walau milioni 4 (life insurance). Haya mambo ukiyapangilia yanasaidia sana kuondokana na hii migogoro wajameni, hebu tubadilike wakuu.
Marehemu alishaacha wosia azikwe Bagamoyo. Mke ndo amegoma kwa sababu za kibiashara. Mahakama imetoa amri mke ametoroka hajazika mumewe. Na hapo awali mke alishafumaniwa na picha zake zilichafua hali ya hewa kwa mange
 
Haiko hivyo mkuu, mume akifa ukisikia anaenda kuzikwa kwao ujue anaenda alikozaliwa ambako mke hana uhalali nako, hivyo ndugu wa mume watahusika mwanzo mwisho, na mke siku zote anazikwa na mume wake(hapo mwanaume ndiye anaamua mke wake azikwe wapi) hapo mambo ya haki au gender balance hayapo
Upo sahihi mkuu, wenye haki ya kuzika ni upande wa mume yaani ndugu zake, Ila mke akifa mume ndio ataamua kwa kumzika mkewe
 
Baadhi ya Waombolezaji kwenye msiba wa Kijana Henry Massawe aliyekua Mkazi wa Kiaraka Magengeni, Bagamoyo Mkoani Pwani, wamelazimika kuvunja geiti la nyumbani kwa Marehemu ili kuingia kumzika baada ya kukuta geiti hilo limefungwa huku Mke wake akiwa hajulikani alipo ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Mahakama ya Bagamoyo kuamuru Marehemu azikwe Bagamoyo na sio Kilimanjaro kama alivyotaka Mkewe.

kabla ya kuvunjwa kwa geiti hilo Waombolezaji walikua wamekaa nje wakati wote na baada ya hapo wakaingia na kuuvunja pia mlango wa nyumba ya Marehemu ili mwili uingizwe sebuleni kama ilivyo taratibu za misiba ya kikristo.

Henry Massawe alifariki January 16, 2023 na mwili wake ulisubiri kuzikwa kwa wakati wote huo kutokana na mgogoro uliokuwepo baina ya Ndugu wa Marehemu waliotaka azikwe nyumbani kwake Bagamoyo huku Mke wa Marehemu akitaka azikwe Kilimanjaro kabla ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Vedatus Mwalia kuamua kuwa Marehemu azikwe Bagamoyo ,
Mahakama ya Bagamoyo mkoani Pwani leo January 24 2023 kuamuru mwili wa Henry Massawe kuzikwa nyumbani kwake Kiaraka, Bagamoyo kama watakavyo Ndugu zake na kutupilia mbali hoja za Mke wake aliyetaka akazikwe Mkoani Kilimanjaro, Ndugu Jamaa na Marafiki waliojitokeza kwa ajili ya maziko ya Marehemu Henry wamekuta geti la nyumbani kwake limefungwa huku ikielezwa kuwa Mkewe hajulikani alipo,
Huyu marehemu alishawahi pia kuwa TA pale UDSM umeme. Enzi hizo tunasoma back 2011 etc
 
Mhhhh kazi ipo...hivi siku hzi mtu unaweza ukawa unafanya kazi Daslamu na makazi bagamoyo eee...kweli mji umekua

Watu wengi sana wanaishi mbali na wanapofanyia kazi.

Watu wanaishi kibaha kazi posta

Watu wanaishi chanika kazi posta

Watu wanaishi tuangoma kazi posta

Watu wanaishi mbande kazi posta

Watu wanaishi mapinga , kerege, bagamoyo kazi posta
 
Mtu akishakuwa ni mume/mke wa mtu halali mwenzie akitangulia all alobaki ndio wa kupanga ni wapi mume/mke wangu atazikwa! Sio ndugu......ndugu kuingilia kupanga flani azikiwe wapi ndio wana jambo lao
Sio kweli, mwanaume anazikwa kwao means alikozaliwa au popote pale ndugu zake watakapoona inafaa ila mwanamke anazikwa pale mume wake atakapopendekeza. Unadhani mahari ina maana gani?
 
Back
Top Bottom