Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kuhusu changamoto zilizoibuliwa na wananchi wakati wa mkutano uliofanyika tarehe 16 Oktoba 2026, unaendelea kwa vitendo Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.
Wataalamu wa sekta ya Ardhi wakiongozwa na Naibu kamishina Mkuu kutoka wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wameendelea na hatua za kushughulikia changamoto hizo kwa lengo la kupata ufumbuzi wa kudumu, kuboresha utoaji wa huduma na kuhakikisha hoja za wananchi zinapatiwa majibu na hatua stahiki.
Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kusikiliza wananchi, kufanyia kazi maoni yao na kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wake ili kuleta matokeo chanya yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Serikali inasikiliza, inachukua hatua na inatekeleza kwa vitendo.