Bahari mpya kuligawa bara la Afrika, Tanzania kuwa sehemu ya Kisiwa

Bahari mpya kuligawa bara la Afrika, Tanzania kuwa sehemu ya Kisiwa

Yaani likitokea hilo watu wengi sanaaa watakufa na hatuwezi kuzuia chochote.

Yaani watakufa na pakuzika patakua hapapo, Waombolezaji Wataombeleza na kuwalia nduguNa Watu wasiowajua na kuwasahau kabisa pia Kuna Baadhi ya Mataifa yatafutwa katika uso wa Dunia.

Mungu saidia lisitokee miaka ya hivi karibuni [emoji2969]
 
Haitakuja kutokea mtutsi kumtumikia Mhutu
Hapo Katoro,Bwanga na maeneo ya jirani mpo mmejazana mnachunga ng'ombe kwa kuajiriwa na mshahara ni chakula na sehemu ya kulala tu.Mnaongeaga utadhani wote mna uwezo kumbe idadi kubwa ni maskini wa kutupwa.
 
Mmechungishwa Sana ng'ombe tabora na kufanya kazi ndogondogo mabwege nyie
Katoro huko maporini mpaka leo kazi yao ndiyo hiyo hiyo kuchunga ng'ombe,ni kazi wanayoiweza nankuipenda ili mradi awe na uhakika wa kunywa maziwa tu basi
 
mpaka haya yatokee Tanzania haitakuwepo, maana inatafunwa kwa kwa speed ya mwanga
 
Yaani likitokea hilo watu wengi sanaaa watakufa na hatuwezi kuzuia chochote.

Yaani watakufa na pakuzika patakua hapapo, Waombolezaji Wataombeleza na kuwalia nduguNa Watu wasiowajua na kuwasahau kabisa pia Kuna Baadhi ya Mataifa yatafutwa katika uso wa Dunia.

Mungu saidia lisitokee miaka ya hivi karibuni [emoji2969]
Mkuu haya mambo hayatokei kwa usiku mmoja, ni very vey gradual process.

Bahari hupanuka au kupungua kwa mwaka 0.01 hadi 1cm kwa mwaka. Na hilo bonde la ufa linazidi kuongezeka kila siku na baada ya miaka mingi sana ijayo (50M) litajazwa maji na kuitwa bahari. Na kujazazwa kwake maji process yake ilishaanza, humo utakuta madimbwi, vijito, mabwawa na mwisho maji yata colonize. Kipande kitazidi kujitenga kidogokidogo na kujisogeza mashariki. Hii process inaambatana na matetemeko, milipuko ya volcano n.k.
 
Umbali kwenda unguja na pemba utapungua nadhani na kodi za magari kutokea Zanzibar pia shughuli za utalii bahari zitahamia Kigoma
 
Sisi tunaosoma Biblia na kuelewa NENO la MUNGU, tunasema that will never happen, haitakaa itokee.

Sababu ni kwamba, Biblia imetabiri matukio yote makubwa yatakayotokea duniani. Tukio la kugawanyika kwa bara la Africa ni tukio kubwa mno na halijatabiriwa kwenye Biblia.

Tukio kubwa lililotabiriwa ni tetemeko kubwa la ardhi litakaloikumba dunia yote kwa mara moja na kusababisha milima yote kudidimia na kufutika kabisa kwenye uso wa dunia. Pia, visiwa vyote vitatoweka sababu ya tetemeko hilo. Miji yote, majiji yote ya duniani yataanguka, majumba na maghorofa yote yatakaa chini.

Na baada ya tetemeko hilo kuu, ndipo KRISTO ataonekana akishuka kutoka mawinguni, akija na malaika wengi mno na sauti kuu ya parapanda itasikaka duniani kote.
Kama na watu watakufa bas itakua ni ukatili wa Hali ya juu Zaid kuwahi kutokea Maishani!!
 
Hizo ni dalili za mwisho za kiama hata kwenye qu_rani imeelezewa kila kitu na kisiwa cha mwanzo kuangamiya ni tanzania kitafudikizwa na bahari kipotee kabi
 
Hizo ni dalili za mwisho za kiama hata kwenye qu_rani imeelezewa kila kitu na kisiwa cha mwanzo kuangamiya ni tanzania kitafudikizwa na bahari kipotee kabi
Mkuu

Qur'an imeitaja TANZANIA kwenye hilo!!?

Tuambie Qur'an ngapi na sura Gani imetaja hilo!!?

Acha Kuleta taharuki nchini!!
 
Tena mshahara wao mkubwa ni kuhakikishiwa tu kunywa maziwa,chakula na sehemu ya uhakika ya kulala

Na mkambala(tumbaku iliyosokotwa kama kamba).

Ila ndoto za Alinacha hazijawahi ondoka vichwani mwa watu
 
Kama na watu watakufa bas itakua ni ukatili wa Hali ya juu Zaid kuwahi kutokea Maishani!!
Gharika wakati wa Nuhu na moto wa Sodoma na Gomorah vilikuwa ni ukatili wa hali ya juu?

Dunia na vyote viijazavyo ni mali ya MUNGU. Yeye ndiye aliumba dunia na viumbe vyote ukiwemo na wewe mwanadamu pia ni mali ya MUNGU, tena wewe u kazi ya mikono yake.

Ikiwa wewe unaweza kusafisha nyumba yako, ukaua panya na mende wote walioko ndani ya nyumba yako, viumbe ambao hujawaumba wewe. Je, MUNGU aliyeumba hana haki ya kuisafisha dunia yake na uchafu wote kuuchoma moto????
 

Wanajiolojia wamethibitisha kuwa bahari mpya inaundwa barani Afrika ambayo italigawa bara hilo nusu.

Inasemwa kuwa ufa wenye urefu wa maili 35 ulionekana katika jangwa la Ethiopia eneo la Afar mwaka 2005 na pengine ni mwanzo wa bahari mpya kabisa.

Ukurasa wa The Archeologist umeandika kuwa Jarida la Geophysical Research Letters linalotumia data za tetemeko na utokeaji wa nyufa linasema utengano wa bara la Afrika ulianza taratibu takribani miaka milioni 30 iliyopita.

Mataifa 54 barani Afrika yamegawanywa kulingana na wanajiolojia wanaotafiti juu ya tectonics ya sahani za bara hilo. Ufa wa Afrika Mashariki, unaotenganisha nchi za pwani ya mashariki kama Kenya na Tanzania kutoka sehemu kubwa ya bara, unapitia Msumbiji kutoka eneo la Afar kaskazini mwa Ethiopia.


Chanzo: TBC

--------------

Moja kwa Moja kwenye mada.

Wanajiolojia wanasema Bara la Afrika litagawika kutokana na Bahari Mpya inayoenda kujitokeza.

Kwa Mujibu wa Wataalamu hao Kuna ufa unaoendelea kukua na ulioandia Ethiopia unaozidi kuongezeka kadiri ya Miaka inavyokwenda na hivyo kusababisha matetemeko makubwa ambayo yatakuja kupelekea Drifting ya Bara la Afrika na kuzaa Kisiwa Kipya kikubwa kitakachotenganishwa na Bahari Mpya.

Tanzania itakuwa sehemu ya Kisiwa hicho kikubwa sanjali na Nchi zingine za Afrika Mashariki..

My Take.

Mambo haya sio ya kupuuza ila pia hayazuiliki maana maafa yatakayokuja kutokea itakuwa simulizi ya Dunia,hiyo ya Uturuki na Syria ni maandalizi tuu.

Ukiangalia Mwenendo wa Matetemeko na Volcano za mara Kwa mara Kwenye milima ya DR Congo Mashariki na matukio ya hivi karibuni ya mauji uji ya magma liyojitokeza kwenye uso wa Dunia hasa Dar na Shinyanga ni viashiria tuu vya mambo hayo makubwa yanayotisha yatakayotokea Duniani.

Maandalizi pekee ya hali hii ni unyoofu wa Moyo vinginevyo ni vilio na Wala hakuna sayansi ya kuzuia nature,kama tuu mabara yalivyotokea ndivyo itatokea pia miaka ya baadae.
Hadi itokee hio none of us will be alive, not to mention the Earth itself 🤣🤣
 
Back
Top Bottom