ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Wanajiolojia wamethibitisha kuwa bahari mpya inaundwa barani Afrika ambayo italigawa bara hilo nusu.
Inasemwa kuwa ufa wenye urefu wa maili 35 ulionekana katika jangwa la Ethiopia eneo la Afar mwaka 2005 na pengine ni mwanzo wa bahari mpya kabisa.
Ukurasa wa The Archeologist umeandika kuwa Jarida la Geophysical Research Letters linalotumia data za tetemeko na utokeaji wa nyufa linasema utengano wa bara la Afrika ulianza taratibu takribani miaka milioni 30 iliyopita.
Mataifa 54 barani Afrika yamegawanywa kulingana na wanajiolojia wanaotafiti juu ya tectonics ya sahani za bara hilo. Ufa wa Afrika Mashariki, unaotenganisha nchi za pwani ya mashariki kama Kenya na Tanzania kutoka sehemu kubwa ya bara, unapitia Msumbiji kutoka eneo la Afar kaskazini mwa Ethiopia.
Chanzo: TBC
--------------
Moja kwa Moja kwenye mada.
Wanajiolojia wanasema Bara la Afrika litagawika kutokana na Bahari Mpya inayoenda kujitokeza.
Kwa Mujibu wa Wataalamu hao Kuna ufa unaoendelea kukua na ulioandia Ethiopia unaozidi kuongezeka kadiri ya Miaka inavyokwenda na hivyo kusababisha matetemeko makubwa ambayo yatakuja kupelekea Drifting ya Bara la Afrika na kuzaa Kisiwa Kipya kikubwa kitakachotenganishwa na Bahari Mpya.
Tanzania itakuwa sehemu ya Kisiwa hicho kikubwa sanjali na Nchi zingine za Afrika Mashariki..
My Take.
Mambo haya sio ya kupuuza ila pia hayazuiliki maana maafa yatakayokuja kutokea itakuwa simulizi ya Dunia,hiyo ya Uturuki na Syria ni maandalizi tuu.
Ukiangalia Mwenendo wa Matetemeko na Volcano za mara Kwa mara Kwenye milima ya DR Congo Mashariki na matukio ya hivi karibuni ya mauji uji ya magma liyojitokeza kwenye uso wa Dunia hasa Dar na Shinyanga ni viashiria tuu vya mambo hayo makubwa yanayotisha yatakayotokea Duniani.
Maandalizi pekee ya hali hii ni unyoofu wa Moyo vinginevyo ni vilio na Wala hakuna sayansi ya kuzuia nature,kama tuu mabara yalivyotokea ndivyo itatokea pia miaka ya baadae.