Bahati Bukuku: Baada ya kutoka kimuziki wachumba walikuwa wengi akiwemo mfadhili (sponsor) wangu, nilionywa kuhusu wanaume wa Dar

lord atkin

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
205
Reaction score
769
Msanii nguli wa muziki wa injili Bahati Bukuku amefunguka kuhusu safari yake ya kimuziki toka alipotoka mkoani mbeya na kuja Dar Es Salaam.
Bahati Bukuku anaeleza kuwa aliondoka mkoani mbeya kuja Dar Es Salaam Kwa ajili ya kurisiti masomo yake ya kidato Cha nne baada ya kutofanya vizuri.

Bahati Bukuku alifikia Kwa Baba zake wadogo ambao mmoja alikuwa akiishi manzese na mwingine mwananyamala. Anaendelea kusimulia kuwa alipotoka mkoani mbeya alionywa kuwa makini na wanaume wa Dar, lakini alipofika mjini na kuanza kuimba kanisani alipata mfadhili (sponsor) aliyevutiwa na uimbaji wake na kuamua kumsaidia kimuziki. Sponsor alimpatia laki sita, na akamlipia gharama zote za studio, akamnunulia simu.

Bahati Bukuku mbali ya kueleza jinsi alivyorekodi album ya kwanza na jinsi alivyokutana na muhindi mpaka album yake kufanya vizuri, ameeleza kwamba baada ya kupata jina wachumba walikuwa wengi sana, ndiposa sponsor alipoamua kutupa ndoano yake na kumweleza bahati Bukuku kwamba alifanya yote yale Kwa sababu alikuwa anampenda na angependa kumuoa. Wakati sponsor akisema hayo hofu ya Bahati Bukuku ni Kwa sponsor na siyo yeye kwani hakuamini kwamba Kwa utofauti wa kimaisha uliokuwepo sponsor angempenda yeye.

Bahati Bukuku anakiri kwamba alikuwa na utoto, kutokujitambua na ushamba mwingi sana kiasi Cha kushindwa kutambua nia ya sponsor kutoka mwanzoni.

Baadaye Bahati Bukuku aliamua kumkubalia sponsor na wakafunga ndoa. Alimkubalia Kwa sababu alimpenda na kumuonesha mapenzi ya kweli na kwamba hata yeye baadaye alikuja kumpenda kweli kweli na walipendana. Anasema ni mwanaume aliyempenda bahati siyo huyu tunayemuona kwenye tv, Bali bahati aliyekuwa amechoka hohehahe asiye na jina....

"... Nilimkubali Kwa sababu nilijua ni mtu aliyepigania maisha yangu lakini pia hakuonesha tamaa mbele..." Aliongea Bukuku

MAISHA BAADA YA NDOA

Maisha baada ya ndoa ya Bahati Bukuku mwanzoni yalikuwa ya amani furaha na upendo na alipata Kila alichokihitaji katika maisha.
"Nilikuwa siishiwi pesa" anasema Bukuku, japokuwa miaka hiyo ya 2003 music haukuwa ukilipa sana lakini mume wake alikuwa ni mtu aliyekuwa anajiweza kifedha hivyo alipata alichokitaka.

Baadaye ndoa Yao ilikumbwa na jaribu zito lililotokana na tatizo la uzazi alilokuwa nalo Bahati Bukuku ambapo alikuwa akijifungua watoto wanafariki na wakati mwingine mimba kutoka, baada ya kumtokea hali hiyo mara kadhaa ndipo Sasa wapambe walipopamba moto.

Bahati Bukuku anasema kilikuwa kipindi kigumu mno katika maisha yake
" Usicheze na jaribu la ndoa", anaongea Bukuku
Bahati Bukuku anasema alimpenda mno mume wake na hakuwa tayari kumuacha hivyo ni kipindi alichokuwa karibu na Mungu
"hakuna mtu ambaye hapendi mahusiano yake Ili mradi hakutafutiwa" anasema Bukuku

Bukuku anasema alikuwa kama amechizj hivi nyimbo zote alizoimba kipindi hicho zilikuwa za majaribu tu

"Majaribu yamekuwa sehemu ya maisha yangu eeh baba nisaidie nitie nguvu... Mtu anayeimba wimbo wa namna hii ni mtu mwenye mzigo mzito" anasema Bukuku

Ndoa ya Bahati Bukuku iliyumba mume wake akawa anamuona bahati Bukuku kama kituko, vita Ikawa kubwa sana vyombo vya habari vikawa vinamwandika vibaya sana hasa gazeti la kiu. Bukuku anasema aliondoka na kwenda kuishi Kwa dada yake tabata baada ya mume wake kuwa tayari Sasa ana mwanamke mwingine.

Bahati Bukuku anadai washauri na wapambe walikuwa wengi sana, na wapo waliomfuata na kumshauri atafute wataalamu Ili aweze kumtuliza mumewe huyo kitu ambacho hakuafiki kwani yeye amelelewa kwenye wokovu na siyo katika maswala hayo ya wataalamu (waganga)

ITAENDELEA....

Mi nilijua alirisiti akiwa Meta,kumbe alianza kurisiti akiwa Dar,aisee kichwa chake inaonekana shuleni kiligoma,akagundua kipaji chake,akaachana na shule,saa hizi mambo yake yako njema.Tugunduage vipaji vyetu,tusipoteze muda kusoma.
 
kabisa mkuu ila nchi zetu hizi kugundua kipaji cha mtu ni shida,.
Watu tunaishi tu bora siku zinaenda
 
Msanii nguli wa muziki wa injili Bahati Bukuku amefunguka kuhusu safari yake ya kimuziki toka alipotoka mkoani mbeya na kuja Dar Es Salaam.
Bahati Bukuku anaeleza kuwa aliondoka mkoani mbeya kuja Dar Es Salaam Kwa ajili ya kurisiti masomo yake ya kidato Cha nne baada ya kutofanya vizuri.

Bahati Bukuku alifikia Kwa Baba zake wadogo ambao mmoja alikuwa akiishi manzese na mwingine mwananyamala. Anaendelea kusimulia kuwa alipotoka mkoani mbeya alionywa kuwa makini na wanaume wa Dar, lakini alipofika mjini na kuanza kuimba kanisani alipata mfadhili (sponsor) aliyevutiwa na uimbaji wake na kuamua kumsaidia kimuziki. Sponsor alimpatia laki sita, na akamlipia gharama zote za studio, akamnunulia simu.

Bahati Bukuku mbali ya kueleza jinsi alivyorekodi album ya kwanza na jinsi alivyokutana na muhindi mpaka album yake kufanya vizuri, ameeleza kwamba baada ya kupata jina wachumba walikuwa wengi sana, ndiposa sponsor alipoamua kutupa ndoano yake na kumweleza bahati Bukuku kwamba alifanya yote yale Kwa sababu alikuwa anampenda na angependa kumuoa. Wakati sponsor akisema hayo hofu ya Bahati Bukuku ni Kwa sponsor na siyo yeye kwani hakuamini kwamba Kwa utofauti wa kimaisha uliokuwepo sponsor angempenda yeye.

ITAENDELEA....

muendelezo please
 
Mi nilijua alirisiti akiwa Meta,kumbe alianza kurisiti akiwa Dar,aisee kichwa chake inaonekana shuleni kiligoma,akagundua kipaji chake,akaachana na shule,saa hizi mambo yake yako njema.Tugunduage vipaji vyetu,tusipoteze muda kusoma.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
INAENDELEA

Bahati Bukuku anakiri kwamba alikuwa na utoto, kutokujitambua na ushamba mwingi sana kiasi Cha kushindwa kutambua nia ya sponsor kutoka mwanzoni.

Baadaye Bahati Bukuku aliamua kumkubalia sponsor na wakafunga ndoa. Alimkubalia Kwa sababu alimpenda na kumuonesha mapenzi ya kweli na kwamba hata yeye baadaye alikuja kumpenda kweli kweli na walipendana. Anasema ni mwanaume aliyempenda bahati siyo huyu tunayemuona kwenye tv, Bali bahati aliyekuwa amechoka hohehahe asiye na jina....

"... Nilimkubali Kwa sababu nilijua ni mtu aliyepigania maisha yangu lakini pia hakuonesha tamaa mbele..." Aliongea Bukuku

MAISHA BAADA YA NDOA

Maisha baada ya ndoa ya Bahati Bukuku mwanzoni yalikuwa ya amani furaha na upendo na alipata Kila alichokihitaji katika maisha.
"Nilikuwa siishiwi pesa" anasema Bukuku, japokuwa miaka hiyo ya 2003 music haukuwa ukilipa sana lakini mume wake alikuwa ni mtu aliyekuwa anajiweza kifedha hivyo alipata alichokitaka.

Baadaye ndoa Yao ilikumbwa na jaribu zito lililotokana na tatizo la uzazi alilokuwa nalo Bahati Bukuku ambapo alikuwa akijifungua watoto wanafariki na wakati mwingine mimba kutoka, baada ya kumtokea hali hiyo mara kadhaa ndipo Sasa wapambe walipopamba moto.

Bahati Bukuku anasema kilikuwa kipindi kigumu mno katika maisha yake
" Usicheze na jaribu la ndoa", anaongea Bukuku

Bahati Bukuku anasema alimpenda mno mume wake na hakuwa tayari kumuacha hivyo ni kipindi alichokuwa karibu na Mungu
"hakuna mtu ambaye hapendi mahusiano yake Ili mradi hakutafutiwa" anasema Bukuku

Bukuku anasema alikuwa kama amechizj hivi nyimbo zote alizoimba kipindi hicho zilikuwa za majaribu tu

"Majaribu yamekuwa sehemu ya maisha yangu eeh baba nisaidie nitie nguvu... Mtu anayeimba wimbo wa namna hii ni mtu mwenye mzigo mzito" anasema Bukuku

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom