Bahati ya mtende ilipotuangukia

Bahati ya mtende ilipotuangukia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ilikua Jumamosi, tulikuwa kwenye container moja mitaa ya nyumbani tuna burudika. Mziki na vinywaji, story na vicheko. Na joto la Dar upate kinywaji cha baridi iwe Fanta, Heineken, Ndovu au Coca-Cola.

Mara ilipita pick up nyeupe, ilipack pembeni. Alitoka dada mmoja alituambia kama tuna sahani twende atugaie vyakula. Hatukua na sahani lakini Wamachinga wanaouza vyombo walipata soko. Kila mtu alinunua sahani. Tulikwenda kule, yule sada alikua caterer na alipika chakula cha sherehe. Hatujui walikosana nini na mteja wake lakini aliamua kugawa chakula na kuondoka. Alikua na hasira sana hakutaka kuongea mengi.

Tulipata pilau, machalari, nyama ya ng’ombe na ya kuku. Baada ya kula wengine hata sahani walimuachia mwenye container.

Hivi ndibyo bahati ya mtende ilivyotushukia Jumamosi hiyo.

1624996630414.jpeg
 
Back
Top Bottom