Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Si tulikua tunajua TU ni movie ndo inatuonyesha baiskeli zikiwa zinapaa, Sasa Rasmi baiskeli ya kwanza yenye uwezo wa kupaa imeachiwa Rasmi.
Inaitwa Volonaut ni baiskeli yenye uwezo wa kupaa Angani ambayo imeonyeshwa kwenye video kupitia slide inayofuata, inafanya kazi kama ilivyo gari la umeme linaloweza kupaa na kutua (Evtol).
๐ก Baiskeli hii imeundwa na kampuni ya Volonaut ikishirikiana na Jetson Aero inaendeshwa na injini ya Ndege ambayo imepunguzwa uzito na kufanya baiskeli yenye Kasi.
๐ก Ina uwezo wa kupaa Angani na kuruka umbali wa mita 50 mpaka 100 kama inavyoonyeshwa kwenye Tangazo.
๐ก Ubunifu huu ni WA kusisimua kwa kuwa unasukuma zaidi uwezo wa watu kumiliki vifaa vinavyopaa ambavyo ni vya kibinafsi.
๐ Haya ni mafanikio ya Jetson ONE naJetson Aero. Walakini, bado kuna changamoto kadhaa:
๐ Inapaa kwa dakika chache pekee 20 TU.
๐ Bei yake ni kubwa mnoo gharama yake ni Dola $92,000 sawa na Tanzania Shilingi milioni 248,289,634/=.
๐ Vizuizi vya kutumia kwani haiwezekani kutumika Usiku kwa usalama zaidi japo hatua zake ni za kusisimua ila sheria yake bado inakataza kuifanya kuwa Ndege za kibinafsi.
Je utaweza kununua ๐ kwa kutoa milioni mia mbili kupata baiskeli ya kupaa badala ya kununua gari tuachie maoni yako?